Mabikra wawili wananichanganya tafadhali nisaidieni ushauri.

Mwana komaa tu zidi kumuomba Mungu kitaeleweka, watoto wa huko nasikia ni wazuri sana kaaaazi kwelikweli
 
ooooops nimeishia aya y ila umejitahidi mkuu kwanza mi sio mpenzi saaana wa hadithi hadithi ila sikukatishi tamaaa hebu wasiliana na shigongo ili akupe safu moja kati ya magazeti yake ya udaku,kila la kheri

Asante mkuu kwa kuziweka sawa mbavu zangu

hyena-laughing.jpg
 
hhahaha! kweli ni ndefu, mimi nimejigeuza geuza kwenye kitanda na laptop yangu hadi kumaliza!
ila jibu naona nitampa kesho, maana ni ndefu sana aisei!!
 
Habari mkuu,
hii story imenibamba sana!ila mi nakushauri kitu kimoja tu,kwamba kati ya hao wawili lazima kuna mmoja unayempenda zaidi ama sivyo?kama ndio basi oa mmojawapo?wasichana ni wengi sana huku duniani na bado wanazaliwa wengi tu,unaweza kuoa leo kesho ukaona mwingine mzuri zaidi ukatamani tena.





habari za kazi ndugu zangu wana jf?kwakweli nimepatwa na msongamano mkubwa wa mawazo amabyo mimi binafsi nimeshindwa kufanya maamuzi sahihi hivyo basi nimeona nilete matatizo yangu hapa jamvini kwani nina imani kubwa nitasaidiwa kimawazo kupata ufumbuzi wa mikasa hii nilionayo kwasasa.

Mimi ni mtanzania mwenzenu ninaeishi kigali rwanda, baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo kikuu, huko nje nilirudi africa na pia baada ya mambo kutoniendea vizuri hapo dar, ndipo nikapatwa na wazo la kuja rwanda kutafuta ajira kiukweli namshukuru mungu nikafanikiwa kupata kazi, sababu mojawapo ya kuja rwanda nikwamba mama yangu mzazi ana asili ya huku na wazazi wake walikimbilia tz mwaka 1959 wakati wa genocide ya mwaka 1959.

Ndugu mwaka jana nilipata bahati ya kukutana na binti mmoja wa kinyarwanda amabe nilivutiwa na e na hivyo sikusita kumwambia kua nimempenda ambae kwa upande wake ilikua vigumu kukubali hivyo basi nikamuomba namba ya simu akasema haa sim nimuomba basi nimnunulie sim aka kataa na kudai kuwa anaogopa wazazi wake wakimuuliza ameitoa wapi hatokua na jibu sahihi, nikampa busness card yangu na kumuomba tuwasiliane kama akipata simu baada ya miezi mi3 alinipigia na kuniambia tayari ameisha pata simu ila hayupo tayari kuwa mpenzi wangu bali tunaweza kua marafiki wa kawaida baada ya hapo akawa ananiomba nimpatie bongo movies kwani anazipenda sana na kwao wote wanaona filam za tz, baada ya muda flan akaniambia kuwa yupo tayari kua mpenzi wangu, kiukweli nilifurahi sana. Then akaniambia kuna mtu anahitaji kuongea na mimi hivyo atanipigia sim, hazikupita siku 3, shangazi yake akanipigia simu na kunialika lunch nyumbani kwake, baada ya kwenda nilikaribishwa vizuri sana kwani mama huyo anajua kiswahili vizuri na hua anakuja tz kibiashara, then akaniambia sababu kuu ya kuniita kwake nikutaka tujadili kuhusu huyo binti, aliniuliza mara kadhaa kama kweli nampenda au nina nia nyingine nikamwambia kiukweli nampenda sana then akaniambia binti huyo ni yatima na wazazi wake wote pamoja na dada na kaka zake waliuawa wakati wa genocide, na hivyo kama kweli nampenda nihakikishe simuumizi kwani yaliomkuta ni makubwa katika maisha yake na pia yeye mwenyewe kamthibitishia kua ananipenda sana, kiukweli nilikubali na baada ya siku chache nikampeleka kwa babu yangu mdogo wake na baba wa mama yangu ambae ni mnyarwanda na kumtambulisha rasm, woote walimpenda sana na kutushauri kua makini na pia hasa mimi ambae ni mkubwa kua nimuongoze vizuri kimasomo na akimaliza shule tuangalie ustarabu mwingine.
Tumekua na utamaduni wa kutembeleana na nimekua nikimsapoti mahitahji ya shuleni na siku moja alikuja kwangu jioni then nikahitaji kufanya nae mapenzi akakataa na kudai anaogopa na hajawahi hata siku moja na aliponiona nimekua disapointed ikabidi akubali na kudai kua hapendi kuniudhi ila tutumie condom, kiukweli baada ya kujaribu nikagundua kua ni bikra, nilifurahi na nikaamini kua ni binti muaminifu ikabidi niachane na wazo la kufanya mapenzi na matokeo yake nikampa zawadi na ku promise sintohitaji tena mpaka atakapokua tayari,
mambo yanaenda vizuri na hatukutani mara nyingi kwani nakua bize sana na kazi,

upande wa pili wa story ni kwamba siku moja tulikua semina katika moja ya hoteli zilizopo remera hotel tek, hapo tulikutana watu wa makampuni mbalimbali ndipo dada mmoja mtoa mada mrembo na nilivutiwa na mitazamo yake na kwa bahati wakati wa lunch tulijikuta meza moja na katika hali ya kutaka kufahamiana ndio tukapeana facebook adress na namba za simu, kiukweli mwanzo tulikua tunashauriana mambo mbalimbali hasa jinsi ya kuandaa report kwa kiingereza za kampuni yao kwani yeye ni managing director, siku moja alini alika dinna kwake, theni tukaongea sana na mimi nikamualika lunch kwangu weekend iliofuatia, baada ya hapo tukawa tunapigiana simu mara kwa mara na siku moja aliniita gafla akidai kua ana tatizo na pia anaamini nitaweza kumsaidia ufumbuzi, nilipofika kwake ndio akanisimulia story yoote ya maisha yake na pia wazazi wake pamoja na kaka zake wa5 wealiuawa kwenye genocide na yeye alisalimika kimiujiza na pia amelelewa na mama yake mkubwa kiukweli alipata shida sana mpaka alipomaliza degree yake ya saikolojia na ushauri na akaapa maisha yake yoote atafanya kazi za kusaidia yatima, na pia imemchukua muda merfu kufikiri ni nani atakaemfaa kua mme wake na amekua akiwakataa wachumba wengi hasa wanyarwandaukizingatia kifedha na kielimu anajiweza na anaogopa kuishi na mtu ambae atakua na maslahi binafsi pia akaniambia anaipenda sana tz na wa tz pamoja na tamaduni zetu kwani tunapenda amani na pia ni watu wazuri, then akaniambia kama nipo tayari na kama ninahitaji mke yupo tayari muda woote tufunge ndoa na ahitaji chochote kutoka kwangu zaidi ya mapenzi ya kweli, nilishikwa na butwaa kisha akaniambia kua yeye ni bikra na haja wahi kulala na mwanamme na pia x boy friend wake walishindana kwakua alikua anahitaji sex badala ya kujadili mipango ya ndoa, nikamuuliza swali kua ana uhakika gani kama mimi ndio chaguo lake sahihi? Akasema amenichunguza kwa muda mrefu na sasa anaamini mimi ndie mwanaume aliekua anamsubiri muda woote.
Kiukweli mimi kiumri nina miaka 29 na yeye ana miaka 31 ila anaonekana mdogo na aliponiambia miaka yake siku amini mpaka aliponionyesha vitambulisho vyake, nikamuomba anipe muda nifikirie then tamjibu next time tukionana, ki ukweli nihitaji kumwambia haiwezekani kwani tayari nina mtu mwingine, nilipo mpigia simu kumwambia hivyo alilia sana na matokeo yake kesho yake nikapigiwa simu kutoka hospita kua amelazwa hospital na dr anahitaji kuongea na mimi, nilishikwa na butwaa then nikakimbia hospital na hali niliomkuta nayo niliona huruma sana dr akaniambia anasumbuliwa na msongamano wa mawazo na chanzo ni mimi kwani inaonekana kauli yangu ya kumwambia haiwezekani kumuuoa ndio ilio sababisha madhara yoote na pia ni muhanga wa genocide kuna uwezekano mkubwa kumbukumbu mbaya za wazazi wake zikamrudia kama nisipokua tayari kumfurahisha na kua karibu nae.

Ndugu zangu nilihisi kuchanganyikiwa na mwisho wake nikamwambia dr hakuna tatizo takua karibu nae na baada ya siku 3 aliruhusiwa kurudi nyumbani kwake.
Nimekua karibu nae sana na pia amekua na furaha muda wote ninapokua nae.

Sasa jana usiku mida ya saa 5, nilimpigia simu yule girl friend wangu kumtakia usiku mwema then nikashangaa kumsikia akiwa mchangamfu mida hiyo wakati nilitarajia kua atakua kitandani, then akaniambia yupo sebuleni peke yake na wote wamelala ila yeye anaona mpira kwani ni fan wa manchester united, kiukweli sikuamini na nikapata mshangao mkubwa kwani hata mimi mwenyewe ni fan mkubwa wa football na club ni chelsea ili kutaka kujua zaidi nikamuomba anitajie wachezaji wa man u anaowahusudu ndio akanitajia berbetov, chicharito, nani pamoja na rooney, nilifurahi sana kuona tunahobie zinazo fanana, ndio nikapata wazo la kumuuliza kuhusu birth day yake ni lini hapo ndio nikachanganyikiwa kabisa kazaliwa tareh 18 mwezi wa 8 na hiyo ndio tarehe niliozaliwa, kiukweli sikuamini mpaka leo nimemfuata shule ili nione kitambulisho chake na ku prove ni kweli then nikamuonesha passprt yangu nayeye akazidi kushangaa, nashindwa kuelewa kwanini mambo yoote haya yananitokea tena ndani ya muda mfupi.
Ndugu zangu kwa heshima na taadhima naombeni ushauri wenu nifanyeje? Ki ukweli nampenda sana huyu binti wa kwanza na pia sijui nitumie njia gani kumueleza huyu wa pili ili anielewe.

Karibuni sana nahitaji michango yenu.
 
Hapa inaonesha kama hii Hadithi ulisimuliwa na wewe ukaamua kutuandika maana hakuna uwiano wa miaka 1959-2011=51 kwa hiyo wote ni sawa na mama zako.
 
mimi ni mtanzania mwenzenu ninaeishi kigali Rwanda, baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo kikuu, huko nje nilirudi africa na pia baada ya mambo kutoniendea vizuri hapo Dar, ndipo nikapatwa na wazo la kuja Rwanda kutafuta ajira kiukweli namshukuru mungu nikafanikiwa kupata kazi, sababu mojawapo ya kuja rwanda nikwamba mama yangu mzazi ana asili ya huku na wazazi wake walikimbilia Tz mwaka 1959 wakati wa genocide ya mwaka 1959.


Hiyo bluu sina kumbukumbu sana umesema huyo binti wa kwanza na wa pili wazazi wao walifariki wakati huo au??

Mwaka waliofariki wakwe zake hajaongelea, samahani kumbe hujaniuliza mimi!
 
Ndugu yangu pole sana,Kama GAGA alivyosema,njia pekee ni kumtegemea Mwenyezi MUNGU.Mke mwema hutoka kwa BWANA,sali sana sana sana sana na Bwana hatokuacha.
 
Haya sasa mkuu unaendeleaje na hilo movie lako tunasubiri mpaka sasa hakuna ambaye umeshamtoa hata mmoja...!!!:decision:
 
Back
Top Bottom