Elections 2010 Mabere Marando kuibukia CHADEMA?

Acheni utani jamani Mabere siyo ajenti wa TISS na wala hajawahi kuwa ajenti wa TISS.. kama makumi ya watu ambao wamekuwa wakijipitisha kuwa ni maajenti wa TISS.. ni wale wanaoitwa huku "starving artists"

sawa lakini that doesnt clean Mabere na kumfanya awe trusted!!!! How can CHADEMA welcome such a negative energy into the party??? its simple, they are desperate to score in a cricket game that that take whatever throw sent

Kusema ukweli, Mabere is not a face of opposition, he is a puppet!!
 
Tumpe muda; tutaona mwisho wake; na Chadema haitasambaratika kwa sababy ya mtu mmoja; i propose akagombee au akapige debe rorya maana ni mpiga debe na mwenye sauti mzuri
 
siasa mchezo hatari saana, jamani ni kwa sababu ya milioni mia moja? Cku zote walikuwa wapi hawa? Au ndo kuhaha kwenyewe?

Audax,
Acha utani. 100M ni pesa ambayo kwa mapenzi yake, anaweza kukusaidia bila hata kukudai Marando nimjuaye. 1e.g KIWANDA CHA MAVAZI YA JIMREX (CHINA), Jimrex chain stores Kariakoo, Jimrex property inayojengwa pale Mwenge sokoni ni mali za Marando.
 
sawa lakini that doesnt clean Mabere na kumfanya awe trusted!!!! How can CHADEMA welcome such a negative energy into the party??? its simple, they are desperate to score in a cricket game that that take whatever throw sent

Kusema ukweli, Mabere is not a face of opposition, he is a puppet!!
Ndugu yangu De Novo, kweli unamjua Mabere? - Mabere Marando aliyekuwa na jeuri ya kumwambia Mwalimu kuwa kafilisika kisiasa wakati wa kudai vyama vingi, Mabere Marando aliyemkatalia Raisi Mwinyi kumteua kwenye kamati aliyoiita ya kufuja kodi ya wananchi kuwauliza kama wanataka haki yao ya kidemokrasia, Mabere Marando aliyeichachafya Bunge kwa hoja nzito nzito kati ya 1995 - 2000, Mabere Marando aliye.. Duh, De Novo humjui Mabere Nyaucho Marando. Huwezi kuongelea mageuzi ya mwanzoni mwa mwaka 1990 bila kumtaja Mabere.
 
Chadema epukeni ku- recycle politicians... Mabere Marando, Prince Bagenda, Augustino Lyatonga Mrema... ni TISS! Kwanini Marando anataka kuwa kwenye Kampeni Machinery za Dr. Slaa? Ili avujeshe siri za mikakati kwa waajiri wake...CCM! Tumshtukieni! Mwacheni abaki mwanachama wa kawaida tu!
 
Wanabodi wengi tu humu wanajiandikia vitu kwa kufuata mkumbo, hakuna lolote wanalolijua. Eti Chadema wamkatae Marando...kwa sababu gani hakuna anayeweka hoja zozote zenye akili!!!

Mabere Marando ni Mwana Mageuzi halisi. Amekuwa akipigania vyama vingi tangu mwishoni mwa 1980's.

Watanzania wanashindwa kuelewa kuwa katika chama au jumuiya yoyote ni lazima kuwe na timu inayoweza kuendesha chama katika mapinduzi mbalimbali bila ya kuangalia maslahi ya mtu binafsi. NCCR walikosea hapo, walipoangalia maslahi ya Mrema badala ya chama mambo yote yakaenda kombo...hakukuwa na Timu tena kulikuwa na watu wachache wanao angalia maslahi yao.

Naamini kabisa Marando ni asset kubwa sana kwa Chadema na upinzani Tanzania hasa katika kulipigania jimbo la Rorya lilirudi upinzani. Mabere angejitosa tu kugombea tena Rorya, alishinda 1995 tena kwa kura nyingi tu...itakuwa leo. Mbunge wa sasa wa Rorya Prof Sarungi ameshajichokea.

Chadema ni chama makini na kina muelekea mzuri sana wa kuwa chama imara mbadala.

Jambo moja tu linaloonyesha wana utaratibu mzuri wa kuongoza Chama chao. Hebu jiulizeni ni nani ndani ya Chadema aliyewahi kugombea uraisi zaidi ya mara moja?

Kuna mashushu wengi tu wamekuwa mstari wa mbele kupigania mageuzi. To mention a few ni kuwa James Mapalala ni ofisa usalama wa Taifa aliyekuwa mstari wa mbele kupigania "mageuzi", Harold Jaffu ofisa usalama wa taifa mzuri tu aliyefanya kazi nzuri sana ya kuhakikisha TLP haipati nguvu hata kidogo, mabere marando amefanya azi nzuri sana ya kuhakikisha NCCR Mageuzi inakuwa kopo tu. Huwa Mabere hashindwi assignments zake, TISS wanajua kuwa yeye ni mtu smart na capable. He will deliver the goods and CHADEMA will go to their knees sooner than later.
Serikali iliposema inaruhusu vyama vingi vya siasa, ilifanya hivyo ili kuwaridhisha donors lakini ukweli ni kuwa haitaki na wala haikutaka. Mpaka leo watu wa usalama wa Taifa wanaambiwa kabisa kuwa mama ni CCM (sio Tanzania) so at any cost CCM itaendelea kulindwa na kuhakikisha inapata ushindi. Mnaosema kuwa mapandikizi ya CCM sasa hawako active TISS mnaota ndoto za mchana, just ask George Liundi atawaeleza. So if you think Marando is harmless you are dreaming, just wait and see.
 
Watu wenye mawazo kama yako ni sumu katika maendeleo ya aina yoyote achilia mbali siasa.

Huna hoja zaidi ya kuendekeza imani potofu ya woga ili mradi woga uliotokana na uzushi wa vijiweni.

Historia ya NCCR inajulikana wazi imewekwa hapa na wanabodi mbalimbali ambao wanamfahamu Marando na wapinzani wengine tangu miaka ya 1980's...kana kwamba hiyo haitoshi imefafanuliwa hapa kuwa kifo cha NCCR kilikuwa na sababu za msingi za kimuundo, ubinafsi n.k sababu za kisomi kabisa...lakini bado mnakuja na hizo hadithi za alfa ulela. Hadithi za kumtafuta mchawi anayeuwa upinzani.

Kalaghabaho...kwa fikra hizi CCM itaendelea kuwa madarakani milele.
 
Mimi najua Chadema are smart enough to know anybody with bad intention kwenye chama, they also have their own Security System, kama Marando kaja kuua chama atajulikana tu, na watanzania wengi atakuwa hajawatendea haki yao ya kimsingi. Marando, karibu Chadema tuendeleze mapambano huenda ndo waziri wa sheria ajaye (2011 -2015). Kila la kheri chadema.
 
Watu wenye mawazo kama yako ni sumu katika maendeleo ya aina yoyote achilia mbali siasa.

Huna hoja zaidi ya kuendekeza imani potofu ya woga ili mradi woga uliotokana na uzushi wa vijiweni.

Historia ya NCCR inajulikana wazi imewekwa hapa na wanabodi mbalimbali ambao wanamfahamu Marando na wapinzani wengine tangu miaka ya 1980's...kana kwamba hiyo haitoshi imefafanuliwa hapa kuwa kifo cha NCCR kilikuwa na sababu za msingi za kimuundo, ubinafsi n.k sababu za kisomi kabisa...lakini bado mnakuja na hizo hadithi za alfa ulela. Hadithi za kumtafuta mchawi anayeuwa upinzani.

Kalaghabaho...kwa fikra hizi CCM itaendelea kuwa madarakani milele.

Mkuu maoni yako nayaelewa vizuri sana, lakini I am entitle to my opinion whether am from kijiweni or mlimani. Kama unaona ni bahati mbaya CCM iko madarakani pamoja na mafyongo yote inayofanya utakuwa uanafanya makosa makubwa. If you think structural weaknesses are responsible for the demise of NCCR then you are dreaming. To tell you the truth, almost every party in this country, CCM included, have a lot of sturctural problems, can you tell why are they still kicking? We are living in really world, you need to be in the game to feel the heat of how is it being played. Waulize CCJ they will tell you. Ligthen up mkuu.
 
Mageuzi hayaji kwa kuletewa mezani kwenye sahani, historia inatufundisha kuwa mageuzi yoyote ya kweli yanakuja kwa misuko suko yenye mchanganyiko wa ushindi, kushindwa, kujifunza na kuvumilia.

Leo hapa tunaviangalia NCCR, TLP, UDP n.k kama somo la kwa nini upinzani una hali mbaya Tanzania, kabla ya 1992 na bila juhudi za kina Mabere Marando tusingekuwa na NCCR wala chama cha kukiongolea. Sasa unapotaka kutushawishi tuachane na sababu za kisayansi na badala yake tukubali kuwa vyama vya upinzani vinakufa kwa sababu vimejaa Wapelelezi wa usalama wa Taifa bila ushahidi wowote ni kuturudisha nyuma.

Wanabodi wameweka hapa structural problems zilizojionyesha NCCR (kuwepo Mrema juu kuliko chama), sasa iwapo unaona hata CCM, Chadema etc na wao wana hizo structural issues; tuwekee hapa nina uhakika wanabodi watachangia kufanunua kwa nini NCCR imeumia lakini CCM bado inazidi kuwa imara.
 
Ni vigumu kukataa mtanzania asijiunge na chama chochote cha siasa. Ni vigumu sana kukataa mwanachama wa chama cha siasa asigombee nafasi ndani ya chama cha siasa mara anapokuwa mwanachama. Ni vigumu sana kuwazuia wanafiki au wazandiki wasifanye wayatakayo wanapokuwa wanachama wa chama husika.

Mabere Nyaucho ni mtanzania mwenye haki sawa na mtanzania yeyote bila kujali kazi au wadhifa wowote alionao. Atakuwa anajidanganya kama kweli ametumwa kuendeleza kazi ya ushushu ndani ya Chadema na serikali ya CCM, siamini. Misukosuko ni moja ya kukuza demokrasia, usalama wa taifa ni watanzania nao wanapata adha kama watanzania wengine, kukosa maji huduma za afya duni, shule mbovu, barabara mbovu, umeme taabu na umasikini unaozidi kila kukicha, usalama wa taifa ni kazi kama ualimu, polisi, jeshi, daktari nk. wao ni sehemu ya tanzania. Msaliti anaweza kuwa yeyote kati ya wote.

Hakuna haja kumwogopa Mabere tumkaribishe, Chadema usalama wa taifa wapo wengi ila hawawezi kushinda nguvu ya wananchi. Tutazoea pale Chadema itakapotwaa dola kwani itahitaji na kutumikia watu wote,ikiwa ni jeshi na usalama wa taifa.

Karibu Mabere kwenye Chama makini, tunahitaji busara zako, jua tu watanzania tupo makini na huo usalama wa taifa ni kazi tu. Chadema sio mahala pa kunusa tusaidie kuwafichua mafisadi sio kuwalinda. ongeza nguvu na si kupunguza nguvu, Chadema hakuna makundi wala ugomvi tunaomba uitunze amani utakayoikuta.
 
Kwanza we Bujibuji kwanini hukuwa patient kuliko kusaga, hatimaye huyo kaenada sasa. Kwa kweli CHADEMA Ipo mbioni kuvurugwa kwa ufupi wamkatae na kama ni Upinzani apigane huko huko NCCR alipo
 
Kwanza we Bujibuji kwanini hukuwa patient kuliko kusaga, hatimaye huyo kaenada sasa. Kwa kweli CHADEMA Ipo mbioni kuvurugwa kwa ufupi wamkatae na kama ni Upinzani apigane huko huko NCCR alipo

Chama makini hakiogopi mtu,sera makini na uongozi makini ndio nguzo. Sote ni watanzania nyote tunawakaribisha Chadema habaguliwi mtu.
 
Karibu Wakili Marando... jamani jamani jamani hivi kweli lini tutakuwa na mabadiliko ya kweli kwa kuogopa mtu? kweli kiasi hiki?

Katika watu makini Tanzania, Marando yumo. Ni fedheha kumfananisha Marando na watu kama Prince na Mrema. Mnamvunjia heshima, unayavunjia heshima mageuzi ya Tanzania.

Kutokubaliana na mtu ni sehemu ya kusimamia yale unayoyaamini.
 
Hivi ninyi mnaomhukumu Marando kama vile ni mkimbizi-mvurugaji, mnajua keshafanya mangapi ya kimkakati yaliyonufaisha Chadema hata kabla ya kuja hadharani kutangaza kuhamia? Nijuavyo mie, kama uanachama sio kadi basi Marando ni Chadema toka kitambo kidogo.
 
Tumpe muda; tutaona mwisho wake; na Chadema haitasambaratika kwa sababy ya mtu mmoja; i propose akagombee au akapige debe rorya maana ni mpiga debe na mwenye sauti mzuri

Jamaa akileta habari zake za longolongo kwa Chama aondolewe sina imani na hili jamaa hata kidogo
 
Chonde chonde CHADEMA, Marando ni pandikizi linalokuja kuvuruga chama kuweni na tahadhari na huyu jamaa hata ikibidi kumnyima kadi ya uanachama mnyimeni hafai kuwa katika wanamageuzi
 
Back
Top Bottom