Mabere Marando:Jambo hili ni zito,Werema sharti asikurupuke

JUST FOR CURIOSITY hivi kama CDM ikichukua nchi 2015, Je itaendelea na huyu AG au inaweza kumchangua mtu mwingine? Jamani sheria zinasemaje?

Maana nasikia kwa mfano CJ akishachaguliwa basi imetoka hadi mda wake wa kustaafu ufike. Je na kwa AG ni hivyo pia? Because I can't imagine serikali makini ya CDM kufanya kazi na foolish Werema.
 
Jamani siyo kwamba Mabere Marando amemkataza Werema kwenda mahakamani,ila ameamua kumpa onyo ili afanye utafiti kwanza kabla hajakurupuka. Ni mara kadhaa CCM imewahi kuwatoa watu sadaka na kuwatelekeza.Kwa mtazamo rahisi ni vigumu kutoamini kwamba hatumiki kisiasa na CCM.

Ukiachana na kupinga umuhimu wa katiba mpya, utagundua kuna masuala mengi ambayo anatumika kuyaficha. Ili mradi tunajua Werema anatakiwa kutenda haki mbona, hakuwahi kutoa kauli ya kuwakamata waliowashambulia na kuwajeruhi wabunge wa CHADEMA jijini Mwanza? Lakini hili suala la message linaonekana kuwa lina uzito zaidi.

Mi nadhani ifikie wakati tuweke itikadi pembeni,mbona dada yetu Magdalena Sakaya alidhalilishwa na askari magereza na alisema bungeni kuwa ushahidi anao lakini Werema alikuwa kimya huku kukiwa na taarifa kwamba CCM ilihusika. Siwatetei wabunge wa CHADEMA ila naona kuna haja ya kudai kushitakiwa kwa watuhumiwa wengine wa ufisadi.
 
Tatizo linakuja; mahakama zilizopo ni kwa ajili ya nani? Zinahukumu kwa kufuata sheria au kwa kutaka kuliridhisha kundi fulani la watu?
 
Mabere marando ni kilaza kama vilaza wengine kwa mantiki hii kama kweli anuhakika na huo mtambo kwanini asitaje mahali ulipo na huyo mtoto wa kigogo anayedai anamiliki? atuletee vithibitisho kwa ameamua kuweka mambo wazi.pili hii inatupa picha kamili ya kwamba swala hili CDM wamingia ubaridi kama wanajiamini na maneno ya marando kwanini hawakuacha kesi iende mahakamani ili pale ndo waiumbue CCM? kwamba wao wanatumia maneno ya vitisho kwa CCM ili wasiende mahakamani,huu ni ukilaza na kutaka kupotosha umma kwa kujitafutia wafuasi.Toka lini adui yako ukamtahadharisha juu ya hatari mbele yake?"Eti we mwizi usithubutu kuingia ndani kwani nina SMG na risasi 30"CDM sikuhizi mmeishiwa mnabaki kutumia mbinu chafu za CCM

Sasa we Kisanga jr kumbe ndiye kituko! yaani Marando akuletee vithibitisho halafu? na mahakama ipelekewe nini au wewe ndiye jaji Kisanga
 
Hakuna cha kuogopa mtu yeyote na hili sasa si suala la mtu binafsi wala Chama chochote cha Siasa (si CCM wala CHADEMA). Ni kesi ya jinai yenye maslahi ya umma na inabidi Serikali iingilie kati mara moja.


Maneno aliyoyasema Wakiri Marando ni tuhuma nzito sana. Maana kama kweli kuna mtambo huo ambao unaingilia mawasiliano ya watu ni wa hatari sana na unaweza kuhatarisha usalama wa Taifa letu.

Marando aitwe mbele ya mahakama mara moja pasipo kuchelewa na alete ushahidi na kama ikidhihirika basi MWENYE HUO MTAMBO NA YEYOTE aliyeshiriki wachukuliwe hatua kali sana bila kujali wanatoka wapi na ni akina nani hapa nchini. Na kama Marando kazusha basi rungu la Hakimu limurudie mwenyewe maana hapo atakuwa si whistle blower bali mzushi wa hatari sana.

Ni mategemeo yangu kuwa hizi ndio aina ya kesi zinazotakiwa kwenda kwa kasi sana na coverage za media zote ziwepo kuwajulisha wananchi. Hatutaki kusikia kuwa bado shitaka linakamilishwa au ushahidi unakusanywa maana haya ameyasema kwa wazi na kutamka kuwa . anaoushahidi.

Hili ni jambo kubwa sana na pia tukumbuke kuwa pia linahusu Taifa lingine la Israel katika tuhuma aliyoitoa Marando. Anatakiwa kuitwa mbele ya sharia ili aondoe sintofahamu hii ambayo ameimwagwa mbele ya wananchi.

Hata Waziri nwenye dhamana ya Mawasiliano hatakiwi kukaa kimya maana hili linaogopesha sana kwamba mtu mwenye uwezo anaweza kwenda nje na kununua mitambo wa mawasiliano na kuuingiza nchini bila kuusajiri na kuanza kuingilia mitandao ya mawasiliano ya watu.


Je huyo ‘mtoto wa mkubwa’ akiamua kuingilia frequency za mawasiliano ya majeshi yetu itakuaje? Karne hii hatuwezi kuwa tunasikia mambo makubwa kama haya halafu yanayeyuka tu kama umande pindi jua linawaka!
 
Sijui sheria ila Werema mweupe sana.....nadhani ni miongoni mwa vilaza wa magamba!!
 
prakatatumba said:
Hili jambo lipo mahakamni lisijadiliwe, hah Hii ndo mbinu iliyotumika mara kadhaa na kupelekea tusijue hatma ya Richmond (Dowans), EPA, Minara miwili ya BOT, Meremeta, Malipo ya wafanyakazi hewa n.k
 
Kama watu wanaweza kuiba password ya email, na kutuma message kwa watu wengine, kwenye simu watashindwa? Hivi watu hana email lakini? Au zimeshafungwa! Yaani hii haihitaji hata gia ya kutumia mtambo wa Israel, only simple reasoning could do!
 
Tatizo linakuja; mahakama zilizopo ni kwa ajili ya nani? Zinahukumu kwa kufuata sheria au kwa kutaka kuliridhisha kundi fulani la watu? Hayo ni matokeo ya muundo mzima wa mfumo wa mahakama zetu,huu ni mhimili unaotakiwa kuwa huru lakini utagundua kuna mkono wa serikali ndani ya mahakama haswa kwenye uteuzi wa majaji.Nadhani tunatakiwa tuliangalie upya suala hili katiba mpya.
 
Hivi kwa nini CDM Wakituhumiwa kwa jambo fulani, huja na taarifa kwa kiintelijensia za kupika na kutanguliza kusema mtuhumiwa akitaka na aende mahakamani? Mimi naona CDM kama wako weupe sana katika masuala mazima ya kisiasa. Mbona wao wametuhumiwa kwa mambo mengi sana kwa nini hawakwenda mahakamani kwa kudhalilishwa? au wao hawajui mahakama zilipo?.

Monitor lizard! Maji yamekauka kwenye mabwawa lazima uje Nchi kavu kushuhudia mgao mkali wa umeme
 
Kazi ya CHADEMA ni kupotosha watu haswa vijana. Mnyika lazima apande kizimbani

kijana mzima na akili zako timamu unajua kuchambua pumba na mchele, kama wewe unaona CDM inakupotosha achana nayo fuata hao MAGAMBA vijana hawajapotoshwa na CDM bali ni hali halisi kuwa MAGAMBa wamechokwa
 
Kutokana na baadhi ya program walizodokeza wanajf nimegundua kuwa kuna 80% ya madai ya Marando kuwa sahihi.Huu mchezo unaonekana kuwa wa kawaida sana ila tunapata shida kuamini kutokana na udogo wa uelewa wetu kuhusu teknologia hii.

Kuna program kadhaa zimetolewa na kuonekana kufanya kazi hiyo ambayo kina Nchemba na Nape waliifanya.Baada ya kupima hoja, nimegundua siri ya Nchemba kulizungumzia suala hilo bungeni ambako alijua atapata nguvu ya hoja toka kwa spika na wabunge wa ccm na siyo kufanya mkutano na vyombo vya habari.

Mi nawaomba wanasiasa wa vyama vyote, fanyeni kazi mliyotumwa na wananchi wenu.Pia ni vema serikali ikawa na uelewa kwamba serikali imara inatokana na nguzo imara ya upinzani hivyo hakuna haja ya kuweweseka kiasi hicho.

Pili, bunge ni sehemu inayotakiwa kuwa mfano wa demokrasia ya vyama vingi licha ya kwamba viongozi wake ni wa chama kimoja.Naamini ujumbe umewafikia wahusika na wanajf kwa ujumla.
 
Hii movie itakuwa nzuri ikienda mahakamani cuz kule zitaachwa siasa na kudeal na facts na patakuwa patamu kweli
 
Uwezo wa Werema ni mdogo. Nina uhakika huenda hata katiba ya JMT hajawahi kuisoma yote, yet amesha-conclude kwamba haihitaji mabadiriko. Huyu bwana ni Attorney General wa Chama cha Mapinduzi
 
kijana mzima na akili zako timamu unajua kuchambua pumba na mchele, kama wewe unaona CDM inakupotosha achana nayo fuata hao MAGAMBA vijana hawajapotoshwa na CDM bali ni hali halisi kuwa MAGAMBa wamechokwa

CDM ni wazushi tu kijana mtaumia Wana agenda ya siri hao wanawapotosha vijana muichukie CCM kiasi kwamba vijana wengi sasa hawatafuti kazi wala kujiajiri kisa ukiuuliza wanasubiri CDM iingie madarakani shauri yenu mtanikumbuka CDM haina uwezo wa kuzalisha ajira wala kutoa ajira ikiingia madarakani cha muhimu ni sisi wenyewe kwa kutumia elimu yetu tujiajiri mbona fursa nyingi tu
 
Unadhani mnyika akipanda kizimbani ccm itaachwa na nguo? jaribu uone.

Hivi wewe unadhani CCM inaogopa wazushi wa CDM? inawapotezea tu mi nakuambia Mnyika hana la kusema wala huyo mabere marando woga tu umewashika
 
Back
Top Bottom