Mabere Marando awania Uspika kupitia CHADEMA

Mkuu Superman so far unazungumzia hypothetical nyingi sana. Hizo hypothetical zote zinatoa control nje ya Chadema kwa maana inabidi wabaki wakisubiria kama conditions zitakua nzuri. Umezungumzia kama CCM wakiwa na makundi.....je wakivunja makundi? Umezungumzia kama upinzani ukiungana.....je wasipo ungana?

Hizi habari mkuu ni sawa sawa na kwenye makundi ya mtoano kwenye mpira ambapo timu ina tegemea fulani ashindwe ndiyo labda wao wapite. Je tunaweza zungumzia concrete strategies ambazo zina weza kumpa huyu bwana mkubwa uspika bila kutegemea mpaka wengine wateleze?
 
Baada ya CC ya CCM kujitwanga risasi ya begani kufuatia uteuzi wa wanawake wanaofahamika kwa udhaifu wa kutopambana na ufisadi...........nyota ya gwiji wa kupambana na ufisadi Mheshimiwa Mabere Marando yaelekea kuwa na mvuto mkali kwenye kinyang'anyiro hicho.............

Ikumbukwe Marando aliwahi kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki na wabunge wa CCM walimwona ndiye anayefaa kuiwakilisha kambi ya upinzani...........

Wabunge karibu wote wa upinzani watamchagua Marando na wabunge vijana wa CCM wanatarajiwa kufanya hivyo kwa nia ya kutuma ujumbe mzito kwa wapigakura bunge hili halitaki utani na ufisadi kama CC ilivyojidhalilisha............

Mheshimiwa Anna Makinda pamoja na kuwa alikuwa Naibu Spika lakini anafahamika kwa kuvunja mijadala mizito ndani ya bunge hilo..................kwa visingizio vya kanuni za bunge au maswali kutoka nje ya sera husika................wabunge wengi hawampendi kwa sababu ya kuliendesha bunge hilo kwa ridhaa yake binafsi au kuwafurahisha wanamtandao..................Ikumbukwe mwaka 1995 alikuwa Mwenyekitebe wa Kampeni za JK na jina lake lilikuwa linatajwa kuwa angelikuwa PM....................yawezekana hizi sasa ni wakati wa kulipwa fadhila ............

Anna Abdallah ni mkongwe wa siasa lakini wengi wanamwona hana upeo wa kuhimili matarajio ya wapigakura wa Karne hii ya 21..........Hivyo hauziki hata kidogo........

Kate Kamba ni msomi mzuri lakini katika Ukatibu Mkuu wake wa UWT hajawahi kupambana na ufisadi au hata kuukemea na hivyo si jemedari wa kutumainiwa..........................

Kama nia ilikuwa ni wanawake mbona mpambanaji mzuri wa ufisadi Mheshimiwa Anne Kilango mbona kaachwa?

Sababu nzito ya wabunge wa CCM kuyakataa mapendekezo ya CC ni kupinga udikteta wa wazi wa kugeuzwa mhuri kwa wabunge wa CCM.................ungelitegemea CC ya Karne ya 21 kuwaachia wabunge wenyewe wajichagulie wampendaye lakini hizi mbeleko za hao akina mama zina lenga kudhoofisha vita dhidi ya ufisadi na huu ni uthibitisho mwingine JK ni kinara wa ufisadi hapa nchini na kamwe tusimtegemee kuutokomeza................
 
sasa nimeanza kuamini kuwa mwaka huu mabadiliko yapo, namuombea mungu marando apite japo ccm wana nguvu bt itajulikana hiyo kesho
 
Hapa hakika Marando ana uwezekano mkubwa,japo kwa namna yoyote naona si rahisi ccm wakamkubali kutokana tu ushabiki. Anna Makinda ni aina ya dikteta wa kike, ambaye namwona ndiye mwenye nafasi kubwa kutwaa kiti hicho kutokana na uzoefu wake.
 
Tafadhali wapinzani wote twawaombeni muungane mumpe kura marando, hata nyie wa sisiem wapinga ufisadi piga kura kwa Marando, bila hivyo naliona bunge la sasa kuwa baya sana kama enzi za chama kimoja, mtakuwa kama picha tu mnayesubiri kupewa posho tuu.
 
Asante Rutashubanyuma, nina swali dogo.....ni kwa nini CCM wanaruhusiwa kuchagua watu watatu kugombea na upinzani wanatoa mmoja tu?

Clarification kidogo itasaidia sana kuelewa hili suala kwani nilitegemea CCM wasimamishe mtu mmoja.
 
Kaka hii inaonyesha kabisa kuwa nchi yetu ina udikteta wa halin ya juu sana! Sitta kaachwa? Ni nani ambae hajui kuwa huyu jamaa alikuwa anaendesha mijadala kwa maslahi ya nchi yetu? Hata kama wewe ni mwanachama wa ccm tafakali hili jiangalie kipato chako halafu tupe jibu.Wameona wakimsimamisha mwanamme mwingine Sitta atalalamika! Lakini macho yetu yote tuyaelekeze kwa wabunge wa ccm kuona kuwa je wako pale kwa maslahi ya taifa au ya chama? Mungu ibariki Tanzania
 
Kitu ambacho ninajua kwa Uhakika: Hata Marando akishinda kura bado zitachakachuliwa ili Makinda ashinde.

Hongera Anna Makinda in advance Spika wa Kwanza Mwanamke.

Shida niliyonayo ni kuwa sijaona record yake yoyote ya utendaji inayonifanya nivutiwe naye.

Anna Abdalah, is just another Pius Msekwa. I hope Uspika si Ufalme. Nimemsikia toka naanza Primary School miaka ya nyuma sana. sijui mpaka leo anafanya nini kwenye siasa. Uroho wa Madaraka ndiyo huu, in an original terms.
 
Habari hii imenukuliwa na TBC sasa hivi kuwa ni kwa mujibu wa naibu katibu mkuu Mh. Zitto Kabwe
 
Kwa kuwa ndani ya ccm wapo wengi hawakuridhika na uamuzi wa cc, watampigia Marando na mungu atakuwa pamoja na sisi.

GO MARANDO GO MJENGONI!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hapa sasa wapinzani waungane pamoja na kumpa Marando manake hawa mafisadi washazigawa kura zao. Ila wale wapinzani wa Zenji, kuna uwezekano wa kutuangusha!
 
Anaweza kushinda kama wapinzani wote wakimpa kura na wale wa CCM wanaoitakia mema nchi yetu bila kuangalia chama chao.
 
ivi m/kiti wa ccm anaangalia tu wakati watu wanachakachua chama??!inabidi Marando apite kwa kishindo ndipo watakapoelewa maana ya people's power!
 
Atashinda maana CCM wamefanya kosa kama la jimbo la Iringa kura za maoni, wenyewe wamempendekeza Anna Abdala, Anna Makinda na ...... hivyo sidhani kama ni watu ambao tunawahitaji kwa sasa.
 
CCM ni chama kinachisifika kwa ushabiki!! Mimi nahisi Makinda atashinda kwa ushabiki ilhali wanajua hawezi hiyo kazi!!!:doh:
 
Marando ni ccm na mtu wa usalama, kwa hiyo atawapoteza chadema. Wawe waangalifu, wangempa muda wa kumchunguza kwanza.
 
Acheni kujidanganya.

Kwanza majina hayo matatu yakitoka hapo yanakwenda katika caucas ya CCM ambapo watachangua mtu mmoja tu na ni wazi atakuwa Anna Makinda. Ukweli ni kuwa kati ya wote hao ni Anna Makinda tu mwenye uwezo, ukomavu na uhusiano mzuri na wabunge walio wengi kiasi cha kumuwezesha kushinda katika party caucus na pia bungeni

Pili, baada ya kuwatukana, kuwakejeli na kuwakashifu CUF kwa miezi yote hii na sasa mnalazimisha bingwa wa utengano katika upinzani Mbowe kuwa kiongozi wa upinzani bado mnajidanganya kuwa CUF hao hao ndio watakaowabebea mgombea wa wenu..Marando?

Acheni siasa za kujidanganya...
 
Acheni kujidanganya.

Kwanza majina hayo matatu yakitoka hapo yanakwenda katika caucas ya CCM ambapo watachangua mtu mmoja tu na ni wazi atakuwa Anna Makinda. Ukweli ni kuwa kati ya wote hao ni Anna Makinda tu mwenye uwezo, ukomavu na uhusiano mzuri na wabunge walio wengi kiasi cha kumuwezesha kushinda katika party caucus na pia bungeni

Pili, baada ya kuwatukana, kuwakejeli na kuwakashifu CUF kwa miezi yote hii na sasa mnalazimisha bingwa wa utengano katika upinzani Mbowe kuwa kiongozi wa upinzani bado mnajidanganya kuwa CUF hao hao ndio watakaowabebea mgombea wa wenu..Marando?

Acheni siasa za kujidanganya...


Nenda kalale wasomi tuendelee kujadili mustakbali wa nchi hii. Kama huna usingizi zima computer ukaangalie katuni acha upumbavu. Anayedanganywa ni wewe unayeongea shombo.
 
Back
Top Bottom