Mabere Marando awania Uspika kupitia CHADEMA

Safi sana marando kuingiza jina. Ila hofu yangu kwa jinsi wabunge wa ccm walivyo chenge akipita wanampa hata apite kichaa watampa tu
 
JF analysis has become quite sub-par in the last 2yrs to be honest. People just write anything, I guess ndio "Uhuruuuu wa kuongeeeea!!" lol

Samwel Sitta for Speaker of the House.
 
Sina uhakika kuwa kura za kumpata Spika zinaendeshwaje, kwa siri au ni za wazi? maana kama ni za wazi CC ya CCM hata ikimpitisha Chenge, kwa woga wa chama wabunge wao watampitisha hata kama mioyo yao haitaki, ila kama ni wa kura za siri basi kosa lolote litakalo fanywa na CCM kuleta fisadi atatwangwa na wa CCM wenzake wenye idadi kubwa na kuacha mgombea wa upinzani akipeta.
 
ni marando kupitia Chadema, ana jazba, hasira na hamaki. hawezi kuwa spika wa bunge letu hili.
atanaweza kupitisha miswaada ya hasira na kutuingiza taifa ktk mitafaruku hasa kwa majirani zetu.
mfano wa kusimama kwenye majukwaa na kukashifu baadhi ya viongozi wetu ni wazi moja ya kasoro ya Mh marando.
kwani inaonyesha endapo atakwaa kiti hicho yale yajwangani na kwengine kuonekana bungeni ambapo kunaweza kuifanya tz yetu isambaratike kwa amani.
We muone quinine akudunge drip manake naona ushaanza. unawezaje kumtetea chenge kuwa spika ilhali mataifa ya magharibi (ISO) walishamtuhumu na yuko kwenye black list?? sh**##^^)) zako we
 
Kama aliwatukana viongozi mbona hawakumfikisha mahakamani? kama waliogopa kumfikisha mahakamani basi aliyosema ni kweli. Na kama aliyosema ni kweli then anafaa kuwa spika wa bunge la JMT.
 
ni marando kupitia Chadema, ana jazba, hasira na hamaki. hawezi kuwa spika wa bunge letu hili.
atanaweza kupitisha miswaada ya hasira na kutuingiza taifa ktk mitafaruku hasa kwa majirani zetu.
mfano wa kusimama kwenye majukwaa na kukashifu baadhi ya viongozi wetu ni wazi moja ya kasoro ya Mh marando.
kwani inaonyesha endapo atakwaa kiti hicho yale yajwangani na kwengine kuonekana bungeni i.
MS acha ya Marando, mie CHAKAZA kama ningepewa u Spika wa bunge hili hali nadhani ingekuwa mbaya zaidi. Wale wabunge wa CCM wanaopoteza muda wa bunge kumwaga Pumba, kuropoka yasiyo na msingi na kutetea waziwazi mafisadi baada ya kuhongwa scholarship kwa watoto wao na visenti kidogo, wallah ningekuwa spika wa kwanza duniani kuwa nashuka toka kwenye kiti na kumlamba makofi mbunge wa aina hizo. We fikiria mfano wabunge wa CCM wa 2005-2010, kwa kweli kama ni kuwachapa makofi labda ungewaacha wabunge wasiozidi 20 tuu.
Marando ndiyo aina ya Spika tunayemtaka TZ hii iliyojaa ufedhuli wa viongozi
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimempendekeza wakili maarufu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Mabere Nyaucho Marando kugombea nafasi ya spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


kama kweli wabunge wote wakiangalia maslahi ya taifa basi wanatakiwa wampe Mabere Uspika na sio Chenge, wanajamii mnasemaje kwa hapo!!!!
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimempendekeza wakili maarufu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Mabere Nyaucho Marando kugombea nafasi ya spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Is this confirmed now?
 
Mabere Nyaucho kuna biashara nzuri hapa kwa Chadema ambayo kama ungeichachamalia wakati huu ungeiongeza nguvu Chadema katika bunge hili; biashara hiyo ni:-
1: Kuawaondoa bungeni wabunge wote wa thithiemu walioingia bungeni bila kuchaguliwa na wapiga kura wa majimbo yao.
2: wabunge wa waoem walioingizwa kwa kupora kura za wanachadema.

Hapa kuna zaidi ya majimbo 40; biashara nzurie!!!!!!!!!!!!
 
Nina wasiwasi na Mwakyembe na Kilango; hawa wanadandia hoja hii lakini si wapambanaji. Wapambanaji ni Shibuda na Mpendazoe!!!!!!!!!
 
Spika wa Bunge hapaswi kuwa na Uchama, hata kama ana chama. Hapaswi kuwa mdini, mkabila na hapaswi kuwa mwenye visasi.

Anapaswa kuwa mwenye huruma, mtu mwenye moyo mkuu, ambaye hawezi kurubuniwa na fedha au ulaghai wa aina yeyote. Kama aligombea ubunge, basi anapaswa kuwa ni yule ambaye hakuchakachua. Mtu wa namna hiyo (mchakachuaji) atalazimika kufanya hila na ubinafsi ili arudishe mtaji alioweka kwenye uchakachuaji.

Hata hivyo, Mungu yupo
 
Ni dhahiri
Mtu Mmoja, CCM mpaka sasa tayari wana candiadtes 12 tofauti na miaka yote. Ushindani Mkubwa unaonekana utakuwa kati ya majina makubwa kama: Samuel Sitta; Andrew Chenge. Anna Abdalah na Anna Makinda.

Kama ushindani ukiwa mkubwa na ukaweka makundi ambayo hayavunjika, kuna hatari ya kupiga kura za chuki na kuupa upinzani ushindi.

Hata hivyo hili linaweza kutegemea na upinzani kama utakubaliana kutoa candidate moja.

Kama nilivyosema, kama muujiza huu utawezekana, then Tanzania yenye neema, ile ya Asali na Maziwa inaweza kuzaliwa!

Itakuwa busara zaidi upinzani ukawa kundi moja katika kupendekeza jina moja kwa nafasi ya Spika hata kama Chadema inaweza kusimamisha peke yake. Hii itakuwa hatua muhimu ya kuanza kuandaa ushirikiano/umoja wa dhati wa upinzani katika uchaguzi wa 2015.
Ni dhahiri CCM watajaribu kila njama kuvunja uwezejano wa umoja huo lakini ndio njia bora na rahisi ya kuivunja CCM.
 
marando hafai kabisa kuwa spika ni mtu wa majungu na ndie aliechangia kwa kiasi kikubwa kusambaratika kwa upinzani miaka ile ya 90 wakati alipokuwa na mgogoro wa kugombea madaraka yeye na lyatonga mrema!
Pili ni msaliti mkubwa kwa upinzani wakati wapinzani walikuwa na chaguo lao la mbunge wa afrika mashariki cha kushangaza huyu marando alipigiwa debe na ccm na kuibuka mshindi!!!

Sasa kama yeye ni miganaji mbona alisambaratisha nccr na baadae kukimbilia chadema tena karibia na uchaguzi?
Kama alikuwa na hamu yauspika kwanini hakugombea ubunge ktk jimbo la uchaguzi ili apate ridhaa ya wananchi na ndipo aje kugombea uspika lakini anangojea kapu maalum!!!

Rafiki Marando hakusambaratisha NCCR. Cjui kwanini watu hawamuelewi Marando wakati ni mpiganaji cku zote. Wapinzani nao wana matatizo yao. Wamejaa siasa za maji taka kama CCM. Marando aliwashinda wenzake live na wachambuzi wa siasa kipindi hicho waliokuwa wanalalama kuwa Marando kachukua nafasi hiyo kuwa Marando aliwazidi uwezo hata kama asingechaguliwa na CCM basi wenzake tu kwenye upinzani wangemchagua. Wenzake walitaka waonewe huruma kwa vile ni wapinzani pasipo kuwa na uwezo.

Kwamba Marando anafaa kuwa Spika au siyo huko siko lakini kwamba alivuruga upinzani wasitafute mchawi wao zaidi ya CCM, uongozi wao usio wa kidemokrasi na kung'ang'ania madaraka kwa viongozi wao.
 
ni marando kupitia Chadema, ana jazba, hasira na hamaki. hawezi kuwa spika wa bunge letu hili.
atanaweza kupitisha miswaada ya hasira na kutuingiza taifa ktk mitafaruku hasa kwa majirani zetu.
mfano wa kusimama kwenye majukwaa na kukashifu baadhi ya viongozi wetu ni wazi moja ya kasoro ya Mh marando.
kwani inaonyesha endapo atakwaa kiti hicho yale yajwangani na kwengine kuonekana bungeni ambapo kunaweza kuifanya tz yetu isambaratike kwa amani.

Malaria Sugu una matatizo kweli. Marando hajamkashifu mtu ila kawaambia walichokifanya. Kama ni kashfa wanafungua kesi kam ni ukweli wanakaa kimya.
Hayo mawazo yako ungeongea nchi kama Kenya kuwa kumwambia Kibaki au Raila kaiba kama kweli kaiba ni kashfa watakudharau watu wale make kiongozi si
 
Back
Top Bottom