Mabenki na mikopo ya biashara kwa wahitimu

Nadhani kuna tatizo moja kubwa sana na hii idea.
Vyeti vya mtu mwingine havina market value! Wewe unaweza kukithamini cheti chako kwa millioni 100, good for you, ila mimi hata buku sikupi maana hakuna ninachoweza kufanya na cheti cha mtu mwingine.

Hii ni tofauti na gari au nyumba ambazo zinauzika katika soko.

Ndo maana cheti hakiwezi kukubaliwa na benki.
 
Nadhani kuna tatizo moja kubwa sana na hii idea.
Vyeti vya mtu mwingine havina market value! Wewe unaweza kukithamini cheti chako kwa millioni 100, good for you, ila mimi hata buku sikupi maana hakuna ninachoweza kufanya na cheti cha mtu mwingine.

Hii ni tofauti na gari au nyumba ambazo zinauzika katika soko.

Ndo maana cheti hakiwezi kukubaliwa na benki.
Hili la cheti kutokuwa na market value nimeshalizungumzia kabla lakini jambo la msingi la kujiuliza, ni kwanini bank inadai collateral! Ukiangalia haraka haraka, ni rahisi kuona kwamba lengo la benki kuchukua collateral ni ili iweze kuiuza pale unaposhindwa kulipa mkopo... YES, it's true lakini msingi wake ni kumfanya aliyekopa awe careful na mkopo aliochukua huku akifahamu kwamba kitu chake cha thamani kinashikiliwa as a collateral! Ndio maana nikasema kabla kwamba best collateral sio ile tu yenye market value bali ambayo pia mwenye nayo hayupo tayari kuipoteza kirahisi!

Wakati nipo bank, niliwahi kufanya kazi wilayani! Unakuta mtu anakuja kuomba mkopo... unamfanyia interview kila kitu kisha unampa karatasi aandike mali alizonazo!!! Ilikuwa ni kawaida sana kuona mtu anaandika mali kibao including mashamba lakini nyumba haiandiki! Ukimuuliza nyumba mbona huandiki, atakujibu kwamba nyumba sitaki iwepo kwenye hiyo list!!! Lakini wala usidhani kwamba hiyo nyumba ndo ina thamani kubwa sana kuliko labda hayo mashamba lakini, wengi hawapo tayari kupoteza nyumba... WHY? Embarrassment ya kuuzwa nyumba yako yenye thamani ya sh. milioni moja ni kubwa kuliko embarrassment ya kuuzwa shamba lako lenye thamani ya milioni 5! Sasa mtu ukichukua nyumba as a collateral basi huyo debtor atakuwa extra-ordinary careful na mkopo wake kuliko kama ungechukua shamba as a collateral! UKichukua collateral only kwa kuangalia market value bila kuzingatia how reluctant your debtor is willing to forgo/sacrifice his/her collateral, at the end of the day utajikuta unasusiwa na milundo ya dhamana ya wateja wako na hatimae bank kugeuka kampuni ya udalali ya kuuza mali za wateja!!!

Turudi kwenye academic certificates... YES, has no market value lakini ni nani yupo tayari kuishi kwa mashaka kuhusu cheti chake alichokitafuta kwa miaka 15+? Huyu akishindwa kulipa deni huwezi kusema uuze au kuzuia cheti chake, NO! Lakini huyu mtu na elimu yake tayari ni valuable asset... ni future employee huyu! Mathalani, kunaweza kuwa na sheria kwamba, kunakuwa na special credit reference bureau itakayoingiza wakopaji wa mpango huu peke yake! Na mwajiri yeyote yule, kila anapoajiri lazima ahakikishe ana-cross check na hii bureau kuhakikisha kwamba huyu mwajiriwa mpya sio defaulter arising from the above program! Kama ni defaulter, ataajiriwa kama kawaida lakini kuanzia hapo, itabidi mshahara wake uwe unakatwa kwa ajili ya kulipia mkopo ambao alichukua! Njia za ku-handle ili ku-minimize risk zipo sana tu...
 
Ukweli mtupu huu jamani kwani CHETI kitamsaidiaje mhe. Wa benki kama mkopaji hameshindwa kulipa ...haa sasa huu ndio ule wizi...
 
Back
Top Bottom