Mabasi ya mikoani kugoma kesho Dar

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,822
KUNA uwezako mkubwa wa abiria nchini kesho kukosa kusafiri kutokana na madereva wa mabasi yaendayo mikoani kutangaza mgomo kwa kile walichodai kulipwa mshahara ambao haulingani na kazi wanayofanya.

Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti baraza la wadhamini Umoja wa madereva wa mabasi Tanzania, Chrizant Kibogoyo amesema kuwa madereva hao wamechoshwa na tabia ya wamiliki kuwanyanyasa madereva kwa kuwalipa viwango ambavyo vinafanana na wafanyakazi wa ndani.

"Madereva wamekuwa wakilipwa mishahar ambayo hailingani na kazi wanayofanya na pia wamekuwa wakifanyakazi kwa muda mrefu bila ya kupewa malipo ya ziada, " amesema mwenyekiti huyo.

Amesema kuwa viwango vya mishara wanavyolipwa madereva ni kati ya sh. 50,00 hadi sh. 120,000 badala ya sh. 2000,000.

Pia amesema kuwa madereva wamekuwa wakitumishwa kwa siku saba badala ya sita bila ya likizo jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Amesema ili kilio chao kiweze kuwafikia wamilikini bora kukandaliwa mgomo ambao kwa namna moja ama nyingine unaweza kuwatatulia kilio chao.

Hata hivyo mwenyekiti huyo aliitupia lawama SUMATRA kuwa ndiyo inayosababisha kuwepo wka hali hiyo kutokana na kuendelea kutumia mikataba feki ya madereva na kutoa leseni za usafirishaji wa abiria kwa wamiliki wa mabasi kinyume cha sheria.

Kutokana na kuwepo kwa taarifa hizo Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Usafiri (SUMATRA) inatarajia kutoa tamko rasmi kuhusiana na kuanza kwa mgomo huo.

Akizungumza na gazeti hili ofisa uhusiano wa SUMATRA, David Mziray amesema kuwa wamepata taarifa kuhusiana na kuanza kwa mgomo hivyo wanatarajia kutoa tamko leo.

"Hivi ninavyozungumza na weqwe tunaelekea kwenye mkutano wa dhahrura ili kuzungumzia hilo kwani kuna kila idara inayohusika, " amesema Mziray.

SOURCE: DAR LEO
 
Kila anayefanya kazi anastahili hali bora ya kazi na malipo halali kwa kazi anayofanya. Sasa suala ni je wanamgomea nani, ni mwajiri wao au abiria? Najaribu kuangalia endapo hakutakuwa na hatua yoyote kwa wamiliki wa magari na kuamua kuajiri watu wengine hasa ikizingatiwa kwamba hicho chao sio chama halali cha wafanyakazi itakuwaje? na mwisho wa mgomo utakuwaje? Utata mtupu.
 
Back
Top Bottom