Mabasi ya crdb yako wapi?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Katikati ya mwaka jana,Benki ya Maendeleo ya Jamii(CRDB) ilitoa mabasi kadhaa kwa ajili ya kurahisisha au kupunguza adha ya usafiri kwa wanafunzi katika jiji la Dar es Salaam.Mabasi haya yalikabidhiwa kwa Manispaa husika.Yalitakiwa kutoza sh 150 na kupandisha wanafunzi tu.Yalitumika kwa muda mfupi.Sasa hayaonekani mara kwa mara.

Je,CRDB wameyachukua mabasi yao? Je,Serikali imeyafisidi?
 
Huo mradi ulifanikiwa tu kuipa sifa CRDB, ambalo lilikuwa lengo kuu. Vinginevyo ulifeli palepale mwanzoni. Nani asiyejua kwamba hakuna taasisi ya umma Tanzania ingeweza kuyaendesha mabasi hayo kiendelevu?
 
ni hivi ngoja nikusaidie mkuu......yale mabasi waliyaleta kwa kigezo cha kubeba wanafunzi ili mradi pale bandarini yasilipie kodi......ikwa kigezo cha kuchukua wanafunzi......ila kwa sasa yale mabasi yanabeba wafanyakazi wa benki ya crdb.....na ule ulikuwa mpango uliondaliwa na wakuuu wa mabenki crdb
 
mi mwenyewe sio mwanafunzi wala mfanyakazi wa crdb lakini nayapanda kwa mia tatu yangu.
 
ni hivi ngoja nikusaidie mkuu......yale mabasi waliyaleta kwa kigezo cha kubeba wanafunzi ili mradi pale bandarini yasilipie kodi......ikwa kigezo cha kuchukua wanafunzi......ila kwa sasa yale mabasi yanabeba wafanyakazi wa benki ya crdb.....na ule ulikuwa mpango uliondaliwa na wakuuu wa mabenki crdb

Unaongea usichokijua.

Hayo mabus yalikabidhiwa kwa UDA na hata sasa yapo yamepark kwenye yard Kurasini.
Kuna kiwango cha pesa UDA wanatakiwa kuwalipa CRDB kila mwezi ingawa wao walipata ujiko kwamba wametoa mabus kwa wanafunzi.
CRDB ipo kisiasa na kimaslahi zaidi, siku mkurugenzi wa sasa akiondoka ndo mtajua hata faida inayotangazwa miaka yote ni ya kupika zaidi.

Hivi mlitarajia mabus 6 yaondoe adha ya usafiri kwa wanafunzi dar? Watanzania tuna taabu ndio maana tunawapa wajawazito bajaji badala ya kujenga vituo vya afya
 
Back
Top Bottom