Mabango ya waganga wa kienyeji kwenya nguzo za umeme na simu

kikahe

JF-Expert Member
May 23, 2009
1,350
282
Hivi haya mabango ya waganga wa kienyeji kwenye nguzo za umeme na simu ynalipiwa kodi kwenye halmashauri/manispaa husika? Yamezidi na yanachafua miji. Hakuna sheria kudhibiti hii hali?
 
Hivi haya mabango ya waganga wa kienyeji kwenye nguzo za umeme na simu ynalipiwa kodi kwenye halmashauri/manispaa husika? Yamezidi na yanachafua miji. Hakuna sheria kudhibiti hii hali?

tena wengi wanajitangaza wametoka nigeria. Ina maana wamepata vibali uhamiaji? Tz kweli jalala!
 
Yaani wamezagaa kila kona hasa Dar es salaam, Arusha na Mbeya ndiyo nimeona kwa wingi. Uhamiaji nao wamekaa kimyaaaaaaa!!!
 
Viongozi wote wanawategemea kulinda nafasi zao za utawala, ni vigumu sana kuguswa na mamlaka zilizopo.
 
tena wengi wanajitangaza wametoka nigeria. Ina maana wamepata vibali uhamiaji? Tz kweli jalala!

Kuna wengi wao wanasema wantoka kule kwetu Sumbawanga, Mpanda, Namanyere, Katumba, Nkasi. Nilijaribu kuwachunguza kwa kuwasalimu baadhi yao 'posuta' cha ajabu wengi wao hawawezi kujibu wanadai 'wazazi wangu ndiyo wametoka huko Ufipani, mimi sikukulia huko na hivyo lugha siijui'. Wanadai kuwa wazazi walilowea huko Tanga, Arusha, Zanzibar, bla bla!!! Ni wasanii tu. Hata hiyo Nigeria ni kuzuga ili wagange njaa.
 
Yaani wamezagaa kila kona hasa Dar es salaam, Arusha na Mbeya ndiyo nimeona kwa wingi. Uhamiaji nao wamekaa kimyaaaaaaa!!!

Ina maana mıkoa hıyo mıtatu ndıyo yenye wateja wengı zaıdı wa waganga?
 
Back
Top Bottom