Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipoanzishwa mwaka 1977 kilikuwa chama cha wakulima na wafanyakazi (chama cha watu wa vijijini na mjini). Na wengi wetu tulifanikiwa kupata elimu na huduma zingine za jamii bila ubaguzi kutokana na sera zake zilizolenga Watanzania wote. Hapa nasemea CCM iliyokuwa chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere.
Baada ya Mwalimu, kimekuwa chama cha matajiri tu huku kikiendelea kuwatumia wakulima na watu maskini kupata kura za kukifanya kiendelee kuongoza serikali. Nasema hivi kwa kuangalia jinsi CCM kinavyotumia fedha kwa mambo ambayo hayaleti maendeleo kwa jamii. Mfano, nikiangalia mabango ya kukitangaza chama hiki hapa Dar es Salaam, hela yake ingeweza kuleta mabadiliko katika maisha ya Watnzania walio wengi. Yaani chama kinajitangaza utafikiri kimeanza leo kwa kuweka mabango kila sehemu na yenye thamani ya mamilioni ya hela? Na hii ni Dar es Salaam tu sijui mikoa mingine hali ikoje. Nimekuwa nikijiuliza: je, ni kweli CCM hakijulikani kiasi cha kuweza kuweka mabango ambayo naamini ni mamilioni ya hela karibu kila sehemu ya mji wa Dar es Salaam au ni kutaka kuonesha kuwa ni chama cha watu wenye uwezo kifedha na hivyo wanaweza kutumia fedha wanazopata jinsi wanavyopenda? Nadhani hata waangalizi wa uchaguzi kutoka nje watashangaa kwa nini tuendelee kuomba misaada kama tunatumia fedha hovyohovyo kiasi hicho! Wasiposhangaa nitawashagaa mimi.
Utawezaje kugharimia mabango yote hayo halafu baadaye uende tena kuomba fedha za maendeleo kwa wafadhili? Na matumizi mabaya ye fedha za umma ndiyo sababu inayoifanya CCM iamini huduma za afya na elimu bure au kuondoa kodi kwenye vifaa vya ujenzi haviwezekani. Lakini vyama shindani vinavyosema huduma hizo zitatolewa bure zinatumia takwimu na vyanzo vya kuingiza fedha kama serikali ya CCM inavyofanya.
Yaani, kwa bajeti ya serikali ya CCM yenye matumizi makubwa yanayotafunwa zaidi na vigogo, huduma za afya na elimu bure haziwezekani! Lakini chama chenye sera za kusimamia vizuri vyanzo vya mapato na matumizi ya serikali, huduma muhimu za jamii kutolewa bure inawezekana. Kenya, kwa mfano, wameonesha mfano huo upande wa elimu licha ya kwamba hawana raslimali (vyanzo vya mapato) nyingi kama ilivyo Tanzania.
Ni suala la utashi wa kisiasa na siyo kutowezekana. Kwa hiyo, mabango ambayo CCM imeweza kuweka karibu kila kona ya jiji la Dar es Salaam, inaonesha wazi, CCM hawawezi kutumia raslimali vizuri ili kuleta maendeleo bali kufuja mali kwa matumizi mabaya. Haya matumizi mabaya ya fedha yamewapofusha kiasi cha kuona kwamba haiwezekani kupunguza hayo matumizi ili kuleta maendeleo zaidi. Vyama shindani vimekuwa vikitoa bajeti mbadala bungeni kuonesha jnsi gani inawezekana kuleta maendeleo zaidi ya watu na vitu.
Hata walioibua ufisadi ni vyama shindani na siyo chama kinachoongoza serikali kwa sasa licha ya kwamba walipingwa vikali kuwa ni habari za uongo! Isingekuwa vyama shindani sasa hivi zingekuwa zimetafunwa fedha nyingi sana bila kujulikana. Jamani Watanzania wenzangu tulete mabadiliko na tusikubali kuendelea kudanganywa kuwa viongozi wa CCM wana uzoefu kuliko wa vyama vingine na wanachokisema ni kweli kabisa na kile kinachosemwa na viongozi wa vyama shindani si kweli.