Mabalozi wetu Saudia na Roma

Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
9,788
14,872
Kumbukumbu zangu zinanionyesha kuwa mabalozi wetu katika nchi za kislamu huwa ni waislamu tu. Ingawa hakuna nchi inayojitambulisha kama nchi ya Kikristo, ila balozi wetu Italia huwa pia ni balozi katinka nchi ya Vatcan, ambayo ni ya kikristo. Kwanini hekima inayotumika kuteua mabalozi katika nchi za kislamu kama saudia nk isitumike kuteua mabalozikatika nchi kama Italy, Enland nk?
 
Kwani kuteua mabalozi waislamu kwenda kwenye nchi za kiislamu ni "hekima?" Kaazi kweli kweli!
 
hayo ni mambo ya intercultural-relation,sometimes lazima uwe flexible kucopy na culture ya mwenzio kwa mahusiano bora.Nchi nyingi za kiislamu hazitenganishi dini na siasa,so ni muhimu kumpeleka mwislamu kule.Lakini kwa nchi kama Italy ambayo inatenganisha dini na siasa unaweza kupeleka yeyote.Nadhani Vatcan ni nchi inyojitegemea na ina balozi wake hapa nchini,sina hakika kama na sisi tuna balozi vatcan lakini ilitakiwa iwe hivyo na kwasababu ni nchi isiyotenganisha dini na siasa basi balozi wetu kule angekuwa padre au askofu.
 
udini unakusumbua tu. Kila kitu mnataka kukiweka katika misingi ya kidini. Kwani huyu balozi wa sasa Italy ni wa ngapi mwisilamu?
 
kwakuwa nchi nyingi ni zile zinazoitwa za kikristo,
na kwakuwa kwa mtindo huo pia mabalozi wengi watakuwa wakristo,
basi mtakuja na hoja ya udini katika uteuzi wa mabalozi na mtasema wakristo wanapendelewa.
 
Kumbukumbu zangu zinanionyesha kuwa mabalozi wetu katika nchi za kislamu huwa ni waislamu tu. Ingawa hakuna nchi inayojitambulisha kama nchi ya Kikristo, ila balozi wetu Italia huwa pia ni balozi katinka nchi ya Vatcan, ambayo ni ya kikristo. Kwanini hekima inayotumika kuteua mabalozi katika nchi za kislamu kama saudia nk isitumike kuteua mabalozikatika nchi kama Italy, Enland nk?

Italy na Vatican ni nchi mbili tofauti kihusiano wa kimataifa. Balozi anaewakilisha Italy pia anawakilisha na Vatican(multiple accreditation) kama alivyo Balozi wetu wa Saudi Arabia akiwakilisha Bahrain na Qatar.
Ama hili la kumchagua Muislamu kuwa Balozi Saudin Arabia logic yake ni kuhakikisha kuwa hakwazi katika utendaji wake wa kazi kwani kuna sehemu ndani ya Saudi Arabia haziruhusiwi asiye Muislamu kuzifikia. Ziko nchi zinazohisi kuwa uwakilishi wao sehemu hizo si lazima kumuhusisha Balozi hivyo huteuwa mabalozi wasio Waislamu. Hawa hutegemea Mabalozi wadogo walioko Mjini Jeddah kushughulikia masuwala katika hizo sehemu takatifu.
 
Nilifikiri sehemu zisizoruhusiwa ni misikiti tu kumbe kuna sehemu nyingine? Nchi za kiislamu kwa ujumla ni wabaguzi!
 
Serikali yetu haina dini. Kwa hiyo sioni mantiki ya kupeleka Mwislamu peke yake kuwa balozi Saudi Arabia. Balozi wetu Italia hivi sasa ni Karume. Mara ya mwisho niliangalia hakuwa Mkatoliki.
 
Mtanzania yeyote anaweza kuwa Balozi kokote bila kujali anasali wapi.
 
On a different note,

As far as I know, balozi wetu wa Germany ana serve pia kama balozi wetu Holy See (Vatican)

Balozi wa Tanzania Italy si balozi wa Tanzania Vatican, ingawa vatican iko Rome.

Hii ilitokana na matatizo ya kidiplomasia kati ya Vatican na Italy.

Nikitaka kutafuta information zaidi kazi kweli kweli, embassies hazina websites, wengine hawajalipa bill, basi tabu tupu.

Hebu ona hapa www.tanzania-gov.it

Halafu tunataka ku promote utalii, embassies zetu ungoogable!
 
Nilifikiri sehemu zisizoruhusiwa ni misikiti tu kumbe kuna sehemu nyingine? Nchi za kiislamu kwa ujumla ni wabaguzi!

Unaposema Nchi za KIislamu ni Wabaguzi ukihusanisha na sehemu tukufu za Maka na Madina una maana gani? Sehemu hizo mbili ziko Saudi Arabia peke yake na hizo sehemu ni za kidini. Sasa sijui kama kuna kosa kwa dini fulani kuweka masharti juu ya watu wa dini nyengine.

Mzee nafikiri jipange upya katika hoja yako.
 
Serikali yetu haina dini. Kwa hiyo sioni mantiki ya kupeleka Mwislamu peke yake kuwa balozi Saudi Arabia. Balozi wetu Italia hivi sasa ni Karume. Mara ya mwisho niliangalia hakuwa Mkatoliki.

Bado udini unawasumbua. Sijui kama umeona suala la logic ya kumchagua Muislamu kama nilivyoeleza. Mwakilishi kwenye nchi huangaliwa vigezo vingi ili kuona uwakilishi wake hautokwazwa na mambo madogo madogo. Pengine ungeuliza kwanini maafisa wa kike hawapelekwi huko nchi za Kiarabu na ungeuliza pia kwanini maafisa wasio Waislamu hawapendelei kupelekwa huko.

Masuala ya utashi hayana nafasi katika suala la kuendesha shughuli za uwakilishi na kama ambavyo sehemu kama Geneva itakuwa na kigezo kwa kupelekwa kama muwakilishi basi sehemu nyengine pia zitakuwa na vigezo vyake hivyo hivyo Saudi Arabia..
 
Balozi wa Tanzania Italy is not accredited to the Vatican. Balozi wa Tanzania kwa Vatican ni Balozi wa Tanzania aliyeko Berlin, Germany. Kufuatia makubaliano kati ya Vatican na nchi zote za dunia kama nchi haiwezi kufungua ofisi za balozi mbili Roma [moja for Italy na ya pili for the Vatican] basi inashauriwa ku accredit to Vatican balozi wake aliyeko nchi nyingine yeyote isipokuwa yule aliyekuwa accredited to Italy. Indeed nchi nyingi za Kiafrika ambazo zina ubalozi Roma huwa wanachagua mabalozi waliopo London/Berlin/Paris/Brussels/Geneva kama balozi wao Vatican. Kwa Bwana Ali Karume hatambuliwi huko Vatican. Nchi zinazo jiweza [e.g USA] huwa na Balozi tatu tofauti huko Roma ya kwanza accredited to Italy; ya pili to Vatican; na ya tatu to UN Agencies in Rome kama vile FAO; IFAD and WFP]
 
Back
Top Bottom