Mabalozi Wapya - Utamaduni wa kuzungusha viongozi!

Unaju ani lazima uelewe tabia za JK kabla hujaelewa matendo yake ambayo ni pamoja na chaguzi zake za viongozi,

(1). JK ni mtu simple sana kuliko wachangiaji wengi wanavyomuandika humu, halafu ni mtu anayependa sifa na kukubalika na wengine, halafu ni mtawala anayetaka kuhusika na kila uamuzi hata uwe mdogo kiasi gani ni lazima ahusike, na issue nyingi alishazifanyia uamuzi siku nyingi kabla hajawa rais, kwa hiyo zikitokea yeye huamua tu bila hata kujali matokeo. Sasa kwa sababu ni mtu simple basi na marafiki zake wa kweli ni watu simple, na hata ukiangalia mistress wake siku zote ni wale wale simple simple, kwa hiyo msishangae kuona kuwa kunakuja viongozi wengi ambao ni simple simple kama yeye!

(2). Baada ya kuwalipa Mtandao kwa kuwapa vyeo vikubwa, sasa umefikia wakati wa kuwaweka viongozi royal kwake binafsi katika sehemu zote nyeti, nao watakuwa ni Wakwere au kutoka kabila lolote la karibu na Wakwere, walioko sehemu za Pwani, sasa hivi kuna nafasi ya Uslalama, inakuja august, na Jeshi. Makamba, Ditopile, Abdulaziz, Sisco, Balozi Idd, Shamuhuna, Khatibu, Mapuri, na the likes, hawa sasa ndio wenye nafasi kubwa ya kuwa watawala wa bongo, sasa ukiangalia hayo majina utaelewa ninachosema, kwani hawa ndio waaminifu wa kweli kwake, uwezo wao kikazi sio neno kwani siku zote kuna wasaidizi!

(3). Je kuna udini? Swali linapaswa kuwa according to our experience as a nation, nini faida na hasara ya viongozi kuwa wadini? Hili lilianza na Mwinyi matokeo yake by the time anaondoka tukajionea maandamano, kuchomwa mabucha, na mauaji ya Mwembe chai, cha ajabu ni matatizo toka upande mmoja tu! Sasa here we are, Jk anaanza tena kuchagua waisilam tu, I mean huwezi kusema eti sio tija, Hell NO! katika nchi yenye dini sensitivity kama bongo huwezi kusema viongozi watano wakichaguliwa Waisilam ni ok, suala la uwezo hilo halina ubishi kwani ni kwa nini walitolewa huko walikokuwa? Adadi kwa nini alitolewa kule polisi? Mapuri kwa nini hakupewa uwaziri tena? Kwa hiyo sio siri kuwa hawa watu hawana uwezo wa uongozi, kuwapeleka huko nje ni kutudhalilisha wabongo!

JK tayari ameshaanza kukubali pole pole kwa matendo yake kuwa na yeye uwezo wa kuongoza kama rais ni mdogo, tena sana, unapoanza kuchagua viongozi wasiokuwa na uwezo ili mradi tu wakusifie basi ni dalili za ngvu ya soda kuwa inaanza kufikia mwisho. Viongozi wengi wanaoelewa kinachoendelea sasa hivi hawataki tena kumsikia Mkapa, maana ndiye chanzo cha haya mauza uza! EL peke yake hawezi kuleta mabadiliko, kwani sasa hivi ndiye anaye-run serikali technically, otherwise Watanzania tutajiongoza wenyewe for thr next ten years kama vile enzi za Mwinyi!
 
Mzee ES ,

Let me use this oppurtunity to commend you for healthful contribution , to make a long story short your right on the money and i can't agree with you more !
 
Mkandara labda tu nikuambie kuwa hii issue sijaianzisha mimi kuna mahali nimeikuta wanaizungumzia Mwanakijiji najua unafahamu hilo. Swala ni kwa nini watu wanazungumzia udini ambao hatuwezi kuthibitisha umetumika? Hii ni kutokana na watu kushindwa kujua hao ni sababu gani zilizomfanya watu waliojaa damu za binadamu na wengine walikuwa wanachelelea ukiukaji wa haki za binadamu.
Rev. please, tumekuwa tunagombania ubalozi kisiwe cheo cha kisiasa mpaka sasa watanzania wameona ni hivyo pamoja na wewe Rev. please this is war and were are loosing na wewe unachekelea. Kwa miaka mingi watu wanaokosa ubunge hupozwa na ubalozi badala ya kupeleka watu wanaojua kazi za kibalozi. Jamani nchi yetu ni masikini we have to be a liitle bit serious, sitashangaa nikija kuambiwa Mangula amekuwa balozi ili wanamtandao wachukue chama.
 
sam said:
Mkandara labda tu nikuambie kuwa hii issue sijaianzisha mimi kuna mahali nimeikuta wanaizungumzia Mwanakijiji najua unafahamu hilo. Swala ni kwa nini watu wanazungumzia udini ambao hatuwezi kuthibitisha umetumika? Hii ni kutokana na watu kushindwa kujua hao ni sababu gani zilizomfanya watu waliojaa damu za binadamu na wengine walikuwa wanachelelea ukiukaji wa haki za binadamu.
Rev. please, tumekuwa tunagombania ubalozi kisiwe cheo cha kisiasa mpaka sasa watanzania wameona ni hivyo pamoja na wewe Rev. please this is war and were are loosing na wewe unachekelea. Kwa miaka mingi watu wanaokosa ubunge hupozwa na ubalozi badala ya kupeleka watu wanaojua kazi za kibalozi. Jamani nchi yetu ni masikini we have to be a liitle bit serious, sitashangaa nikija kuambiwa Mangula amekuwa balozi ili wanamtandao wachukue chama.

Hivi Mchungaji Stith alikuwa ni career diplomat? what about Sarakikya, Mwakalindile, Nyang'anyi?

Kilio kiwe ni kupeleka watu incompetent to be effective siyo kuwa eti si technocrat.

Mapuri kama nilivyosema ni strategy ya Kichama, China Peoples party kinaendeleza ujamaa huku kikifanya mapinduzi ya uchumi na kuendelea kuwa chama tawala.

Do I approve that, heck no but you and I have no control but to observe and learn and teach wananchi 2010!
 
Kwanza inabidi nianze na Mzee Es,
nakubaliana kutokubaliana na sababu zangu ni kama ifuatavyo with facts!
Mwinyi hakuleta Udini kama unavyodai bali alisababisha udini kwa sababu zake bianfsi.
Nakumbuka wakati wa Nyerere mijadala ya waislaam ilikuwepo na ikiendeshwa bila fujo, walionekana machale tu wakitafuta umaarufu kwa kujaribu kuichambua Biblia kulingana na mtazamo wao. Haikuwashtua roho akina Rev. na wakristu wengi ambao waliendelea kushirikiana na waislaam kama jamii moja. Tena basi wizara muhimu ya mambo ya ndani ilikamatwa na waislaam kuliko wakristu.
Alipoingia Mwinyi, alijaribu kurekebisha mambo kwa kuweka usawa wa mijadala hii bila kuelewa hapo ndipo alipoanzisha zaga la watu kuanza kutazama tofauti zao. Matatizo ya waislaam hayakutokana na uchaguzi wa waislaam ktk nyadhifa bali matukio yote yalitokea wakati Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani ya mkuu wa Polisi Mahita ambao wote hawakuwa na udini isipokuwa CUF ilianza kutumia waislaam na misikiti kama njia ya kuiangusha CCM..CUF ilikuwa ndio hutuba ya miskitini, yote ikiwataka waislaam kutokubali kutawaliwa na CCM na kukiita chama cha wakristu. Hilo ndio kosa lao la kwanza na hatari ya kushindwa kwa CCM ilikuwa wazi hata kama Mwinyi ni muislaam. Ukweli utasimama kwamba CCM hakikuwa chama cha Udini hadi Mkapa alipoingia.
Sam,
Udini unaletwa na wananchi wenyewe wanapoanza kuhesabu rangi ama dhehebu la mhusika kutoa maamuzi yao. Udini ni pale mmoja wetu anapoitumia dini kukandamiza waumini wa madhehebu mengine. udini ni pale kiongozi anapochagua watu kwa sababu ya kulinda maslahi ama kuleta maendeleo ya dini yake.tanzania hatujawahi kuwa na Udini ila udini tunao sisi wananchi ambao tumefikia kuanza kutoa maamuzi yetu kwa rangi za dini.
Nakuombeni sana mnipe qualifications za mabalozi kisha tutazame elimu zao ktk maswala hayo. Hivi nani kati yetu alitegemea Powell ama Condelese Rice wangekuwa hapo walipo? je, hii ni ktk kuwaonyesha ulimwengu kwamba Bush hana Ubaguzi wa rangi? au watu hawa walifaa kushika nafasi ile bila kujali matatizo ya rangi ndani ya Marekani. Na inakuwaje bado watu weusi wengi hukichagua chama cha Demokratic ambacho hakijawahi kumpa mtu mweusi nafasi kubwa kama hizo. Jamani, jamani tukianza kutazama vitu kwa rangi zake sijui kesho ttutakuwa wageni wa nani. Mzee Es inabidi nianze kukugopa! samahani lakini.
 
Rev. naona umejijibu mwenyewe, huko ndiko tulikotoka, watu walikuwa wanapewa ubalozi kisiasa wakati ubalozi uwakilishi chama cha siasa unawakilisha nchi. Kama ndiyo mipango yenu ya kumpeleka china kuimalisha chama huo ni wizi wa mchana. China ni nchi muhimu sana kwa uchumi wa Tanzania bado tunaitegemea ili tusimame wima, lazima mtu anayepelekwa au kidogo zinamtosha.
Angalia kwenye wizara nyeti ni watu wa dini gani wanashikilia? Kwa nini watu hawakusema ni udini? IGP ni mkwere kwa nini watu hawakulalamikia uteuzi wake? Nakuakikishia kama angeteua waislamu watano wanaojua kazi basi hakuna mtu angeongea lolote hapa, kama nilivyosema mwanzo watu wameanza kulalamika baada ya kuona hao watu hawatufai.
Mzee ES, nimesoma hotuba ya dk. mzugaji ngasongwa na mama fweza nimeona kwa kiasi kikubwa wamemshukuru sana Dr. Kigoda kwa msaada wa kutengeneza bajeti ya fweza na mipango. Hivi Kigoda bado ni mshine ya uchumi wanayoitegemea? Tupe vitu.
 
Matatizo ya udini na hasa dini ya kiissilamu kuonewa au kuchoma mabucha yameanza enzi za Mwinyi, yakaisha baada ya Ben kuingia,

back to the point kuchagua viongozi watano waisilamu leo bongo, ni dhihaka kwa taifa, halafu lazima uelewe hata Kibello aliyehamishwa ni Muisilamu pia, kwa hiyo ni SITA kwa mpigo, hizi ni dalili za uwezo mdogo wa rais katika kufikiri au kuelewa siasa,

sasa kama rais haelewi, je wananchi itakuwaje?
 
Mzee ES, unayosema ni kweli tupu!

Huyu jamaa, ngoja tusuburi tena uteuzi mwingine! Nimesikia watu wanasema eti Rostam Aziz amekuwa mtunza hazina na pia Makamba aemechukua nafasi ya Mangula je ni kweli?.

Kama ni kweli je nini nini tofauti kati ya Makamba na Mangula kwa mfano?
Toka ameingia madarakani ukiangalia stastics sijafanya utfizi zaidi ila kwa kusikia tu ninadhani ameteua sana waislam. Lakini Kama ni kweli ana mpago kama huo unaosema wa kuteua Wakwere na marafiki. Ninadhani atakuwa anajiweka katika mazingira mazuri ya kukigawa chama mapema! Na hapo tunaweza kupata strong chama cha siasa toka humo.


Wapinzani labda nao wanaweza kuanza mikkatati ya kujiimarisha ngoja tuwasubiri maana kila kukicha utwasikia wakisema tunampa JK miezi sita sasa wao tuwape miaka mingapi kuamka? Ni kweli kabisa kuna CCM wengine kama ES, sam etc akina mimi tunataka upinzani imara kwa maslahi ya taifa.
 
Hivi ni wakati gani chini ya utawala wa Ben Mkapa watu walianza kuzungumzia mambo ya Udini? Kuwa Mkapa anaanza kuwapendelewa wakristu? Kwa muda wote wa miaka kumi ya utawala wake ni wakati gani katika uteuzi wowote aliteua wakristu peke yake?

Ninachotaka kusema ni kuwa, Rais Kikwete lazima awe mwangalifu sana kwenye suala la udini. Sisemi kuwa anaangalia watu kwa dini zao, ila anaacha taswira ya udini pale ambapo anapotaja nafasi za watu sita aliowateua wote ni Waislamu!!! Bila shaka yeye alikuwa na vigezo vingine, lakini natumaini kati ya hivyo dini haimo.

Suala la dini kama lilivyo la ukabila si la mchezo, wala la kufumbia macho! Siyo jambo la kuzoeleka au kutolewa udhuru ni lazima likomeshwe mara moja kwani minong'ono yake inakula taifa kwa chini chini!! Hatari yake ni kuwa siku akiingia Mkristu tena madarakani, na akafanya uchaguzi wenye kuleta hisia za kuwapendelea wakristu... mtasikia maandamano, na kina Sheikh Khalifa Khamisi wakipiga kelele!!!

Hata hivyo, Kikwete anaweza kufanya mambo kadhaa yanayoweza kuondoa hisia hizi kati ya raia wetu, kati yao ni haya.

- Wakati wowote anapofanya uchaguzi wa zaidi ya mtu mmoja kwa mkupuo ahakikishe kuwa majina yao hayaonyeshi udini, ukabila, au usehemu!

- Anapofanya uteuzi mmoja mmoja basi ahakikishe majina yanapokezana. Kama leo kateuliwa Juma basi kesho awe Petro, kama leo ni Hanifa basi kesho awe Regina. Kwani kama leo ni Juma, Suleiman, Khadija, Bakari, Hamza halafu kesho ni John watu watajiuliza.....

Ninachosema ni kuwa, Mhe. Kikwete aangalie sana kwenye hili kwani watu wakianza hiyo minong'ono mtasikia watu wamepigana kilabuni, shuleni au kazini kwa sababu ya kutetea au kupinga hoja zao juu ya hili suala! Yangu macho!!!
 
Last edited by a moderator:
hapa nami niseme tuu kuwa uteuzi una harufu ya udini kwani hata ukiangalia uteuzi wa sekretariati ya ccm aliyoipendekeza jana utawaona kina makamba ,rostam na wengine ila tusiwe na double standards kwani kama kuna udini basi tujadili . nitatoa observation zangu baadae jioni ya leo baada ya kupitia teuzi zote zilizofanya na mh.tangu aingie madarakani.
 
Wandugu Heshima yenu.
Kwanza naanza kwa kusema kwamba mtu anayesema kwamba Karume alikuwa Balozi bora kuliko wote na kwamba kasikia habari hizo namshauri afanye uchunguzi tena .Karume alikuwa ni mzigo wa Taifa .Karuma hakuwajali Watanzania wa Ujerumani na Karua alikuwa anafanya kazi toka Zanzibar .Ujeuri na kuto kujali kwa Karume kulipelekea watumishi wote wa Ubalozi pale Berlin kuwa miungu watu .Kwa ushahidi tu ni kwamba baada ya tabia za Karume kuwa za ajabu na hana maasa Watanzania wa Ujerumani waliamua kwenda kuomba PP zao Brussels .Sasa nataka ujue usemayo kwamba alikuwa balozi bora ni uongo na watumishi walikuwa ni hovyo .

Swala la udini naona mnaanza kubishana kama vile nyie si wasomi wala hamna mamcho wala hamijui Tanzania .Naomba angalieni majina ya aliyo yateua juzi ya kuingia kwenye kuna Jaka na nani mwingine ??? Ndiyo uone kwamba JK ni mdini na atatumaliza .Kuwa serious huyu jamaa anaigawa Tanzania na wala si CCM pekee .Kuna mikoa yake na mingine hataki kugusa kabisa .

Mimi yangu macho
 
I told you guys kuhusu makama it happened! Haya angalieni hii timu halafu mniambie, ila haya ni mambo ya CCM tuwaachie wenyewe wanavyojimaliza.

WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM

Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Yussuf R. Makamba
.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Ndugu Jaka Mwambi
.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar)
Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz
.
Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Taifa
Ndugu Rostam Aziz
.
Katibu wa Organaizesheni wa CCM Taifa
Ndugu Kidawa Hamid
.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa
Ndugu Aggrey Mwanri.

Katibu wa ISiasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM Taifa
Dr. Asha Rose Migiro.
 
Wanabodi,
Nitaendelea kuwapeni somo pale inapohitajika kwa kutumia facts sio mapenzi ya dini kama mnavyofanya. Tanzania ina mabalozi wasiopungua 28 nchi za nje. Wakati wa Mkapa kulikuwa na mabalozi wengi wakristu na sijasikia mtu akidai kuwa ilikuwa udini. Leo hii JK kachagua mabalozi wapya sita imekuwa nongwa hali kati ya hao walioachwa wamo waislaam.
jamani mnaanza kupoteza mbona busara zenu kwa mvuto wa imani. Je, tukikuta bado wakristu wengi mtambatiza JK?

Hiyo SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM inawahusu nini nyie msiokuwa wanachama wa CCM?... Je, hii haizidi kuwapa nguvu zaidi kwamba CCM leo hii wanachagua watu wasiofaa ndani ya chama chao!.. nadhani hii ni furaha kwa Chadema na CUF kwa sababu Makmba hapendwi na watu wengi toka kila dhehebu na kabila. Watu wa kwao wenyewe walimtema itakuwa nyie?. Mkorofi kama Mkapa na ana dharau sana kulingana na habari nilizozipata. Kichama wao wanafahamu faida zake kwao CCM. Binafsi simfahamu vizuri ningependa sana kumchambua kama angekuwa akipigania kiti cha kitaifa. Sekretarieti ya CCM ni ni ileile toka Mkapa isipokuwa kumebadilika kidogo. Rostam alikuwa na wadhifa huohuo toka Mkapa. Kamuondoa muislaam - Ngwilizi na kumweka Jaka Mwambi sehemu muhimu sana ya kichama.

Mwanakijiji,
Kuhusu Mkapa na Udini nitakwambia kilitokea nini. mwalimu Nyerere mwenyewe marehemu alisema kwamba Mkapa kaeneza Udini nchini sasa sijui kama Nyerere nae alikuwa muislaam. Pili, matokeo ya maonezi yote aliyoyasema Mzee Es pale juu ilikuwa wakati wa Mkapa sio Mwinyi isipokuwa nachosema mimi Mwinyi ndiye aliyeruhusu cheche za udini kuanza, Mkapa akazipamba kwa kupuliza. Mkapa alikuwa Mdini wala hakufanya kuficha na ndoto yake ilikuwa muislaam asije kamata kutawala nchi. Mawazo kama haya tu yanadhihirisha mdini acha matendo na visa vyake vya wazi. Ndiye aliyesema mbele wa wana - CCM kwamba Salim hafai, mwarabu hawezi kutawala nchi. Hilo neno pekee kwa kiongozi kama yeye hakutakiwa kulisema ikiwa hakutaka kueleweka kama mbaguzi. Mimi mwafrika na sipendi waarabu lakini sintaweza kusema hivyo hata kama sio mapenzi yangu kwa mwarabu kutawala. Hasa kwa nafasi kama yake... ubaguzi unapozidi akilini hata busara hupotea. Unaposema jambo lazima limekukaa kooni na hisia yako juu ya kundi fulani.
Nimesema mtayasema mengi na bado!..
 
Kwanza namshukuru Mzee ES kwa maelezo mazuri, na nakubaliana naye. Time does indeed make a difference. Mwanzoni, Mzee ES alimsifia sana JK.

Invincible amemlinganisha Mapuri na Zombe. That is unfair to Zombe. Sina wasiwasi kwamba lengo la JK kumpeleka Mapuri China ni kumridhisha Mapuri, na sio kwa faida ya Tanzania. Teuzi nyingi za JK hadi sasa ni kwa faida ya wanaoteuliwa.

Nafasi za kazi za kitaalamu huwa zinatangazwa, na anayefaa kuliko wote anapewa. Hakuna kuangalia dini yake wala anakotoka. Nafasi za kisiasa ni tofauti. Hazitangazwi. Rais anapashwa kufanya chaguzi za nafasi za kisiasa kwa kuzingatia uwezo na usalama wa taifa. Hili la usalama wa taifa linazingatia uwiano mzuri wa dini, jiografia na jinsia.

Haifai Rais akateua wanawake peke yao au wanaume peke yao. Lazima anazingatia uwiano wa kijinsia. Rais hawezi kuteua mawaziri wote toka sehemu moja ya nchi. Anaangalia uwiano wa kijiografia. Rais alikosea kuteua mabalozi Waislamu tu. Ilibidi aepuke kuleta minunguniko ya udini. Kufanya kile kinacholeta minunguniko kama hiyo ni kuhatarisha usalama wa taifa.

Mkandara anauliza uongozi wa sekretariati ya CCM unatuhusu nini sisi tusio wana CCM. This is an extraordinarily weak point. CCM inatutawala hata sisi tusio wanachama wake. Isitoshe, kama udini ukiingia CCM, basi usalama wa taifa zima (na sio usalama wa wana CCM tu) unahatarishwa.

Augustine Moshi
 
Sababu kubwa iliyokifanya chama cha CUF kionekane cha kidini ni safu yake ya uongozi. Sio siri viongozi wengi wa juu wa CUF ni waislamu. CUF wamejaribu sana kulifunika hili hata kwa kuteua wachungaji lakini bado sura ipo palepale. Kwa utaratibu anaoenda nao Kikwete katika uteuzi wa vyeo mbalimbali katika serikali na CCM itafika mahala ataonekana mdini. Lakini nafikiri yeye anakwenda mbali zaidi. Watu waliopo karibu naye wanasema "hataki ujinga wa Mkapa wa kuacha watu wa kwao nyuma"; yeye atateua sana wale watu anaoamini wamekuwa nje ya mfumu kwa muda mrefu wakiwemo kutoka uzaramoni na ndugu zake. Nakumbuka tuliambiwa mkuu mpya wa Polisi wameoa nyumba moja. Yetu macho; tumpe muda kabla hatujatoa hukumu nzito hii ya udini.
 
Hofu yangu ni kwamba hisia za upendeleo wa kidini, hata kwa kiasi kidogo, zinaweza kuleta machafuko. Namshukuru Mzee ES alivyotukumbusha jinsi hisia za upendeleo wa kidini zilivyojitokeza wakati wa Mwinyi, na jinsi zilivyoleta uchomaji moto wa mabucha na Mauaji ya Mwembe Chai.

Ni vema walio karibu na Kikwete wakamuonya mapema kwamba kama hatakuwa makini kuweka uwiano mzuri kwenye teuzi zake za kisiasa, basi ateweza kuleta matatizo makubwa sana.

Inawezekana vile vile kwamba ni kweli JK anapendelea watu wa kwake. Kwa mfano, kazi muhimu ya kupanga uchumi ambayo Kigoda alishaonyesha kuimudu vizuri sana, JK amempa Ngasongwa. Ngasongwa alionyesha uwezo mdogo mno wakati akiwa kwenye viwanda.

Augustine Moshi
 
Nitawaambia kitakachotokea lakini msiniite mtabiri!

Siku moja kwa jiwe fulani karibu na soko au kigenge cha vijana, vijana wawili ambao wamekufa marafiki na washikaji wa siku nyingi watakuwa wanapiga gumzo. Kama unavyojua tena mada za vijiwe zinaanzi mademu, siasa, mpira, n.k na kuishia tena kwenye mademu. Wakati wakijadiliana mara mmoja anasema "JK amewapendelea waislamu kwenye teuzi zake mbalimbali" huyo ni kijana wa kikristu. Yule wa kiislamu atabisha. Yeye (muislamu) atasema "mbona wakati Nyerere anateua wakristu huko nyuma hakuna aliyesema"? Mkristu atabisha, mabishano hayo yataendelea huku kila mmoja akijaribu kutoa mfano wa kuhalalisha maamuzi ya viongozi wetu. Hawa wawili wakiendelea kubishana kiustaarabu ndo jamaa mmoja asiyejua mwanzo wala mwisho wa kinachozungumziwa atakuja na kusema "Waislamu wote ni wapumbavu" au "Wakristu wote ni makafiri" Hapo ndipo yule atakayehisi dini yake imetukanwa atakapovurumusha ngumi...

Ngumi itajibiwa kwa ngumi... mara watu wanaanza kuchagua upande... waislamu wanajaribu kumuokoa muislamu mwenzao.. wakristu wanajaribu kumuokoa mkristu mwenzao... wakiendelea kusukumana, mara mtu anapigwa na ubao.... ndipo gumzo linapogeuka varangati!!!


Wakitawanyika, mtu asiyejua kilichokuwa kinabishaniwa.. anaenda na kusema "wale vijana wa kikristu wa mtaa fulani, wamemtukana Mtume wetu mtukufu"... ndipo shehe na maalim fulani wakati wa swala ya Ijumaa wakahamasisha waumini wao ili kupinga matusi dhidi ya Uislamu... wanaamua kuandamana kuelekea lilipo kanisa fulani... kutokana na hamasa.. vijana waanza kurusha mawe na mwishowe kanisa hilo linachomwa moto...

Vijana wa kikristu nao wanakasirika kwa sababu wanaambiwa vijana wa kiislamu wameenda na kukojoa ndani ya kanisa lao ...

hatimaye hadi mwisho wa mambo yatakapotulia... Watanzania wapata 100 watakuwa wamepoteza maisha yao.... mamia kadhaa kujeruhiwa... makanisa 20 kuchomwa moto na misikiti 39 kuvunjwa ......

tutakapokaa chini na kujiuliza nini kimetokea... jibu halitakuwa gumu....!!!

baada ya kusema hayo.... natema mate kando "Mungu aepushie mbali"..!
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Back
Top Bottom