Mabalozi wajuta kuwakilisha Tanzania nje

lakini kiukweli balozi zetu zinatia aibu sana niliingia beiljing china huwezi amini kama ni ubalozi wetu yaani ni aibu sana. yaani mpaka nyasi mlangoni sijui wameshindwa hata kuajili mtu wa kufanya usafi kwa mazigira ya nje. balozi zetu ndio nchi nchi yetu tukiwa ughaibuni ila ukweli huwezi amini kama ni balozi za tanzania ninayotoka au la!

Tumezoea vya bure hata nyasi serikali ikate, nyumba ifagiliwe na mtumishi, serikali imnunulie chakula kana kwamba hapati mshahara.

Angalia aveta yangu huyo Mkulu wa White House Marekani, hakuenda sokoni kununua maboga kama maonyesho, ni kawaida yake kufanya hivyo. Majuzi tu shule zinafungua kawachukua mabinti zake kwenda kuwanunulia vifaa vya kwenda navyo shuleni.

Marais wengi wa Marekani wananyoa ndevu zao zote, kwa maana kwamba wanajipitisha vijembe wenyewe badala ya kuajiri mtu maalumu kwa ajili ya kutengeneza ndevu kila siku kama bongo tufanyavyo. Bongo watumishi wa wakuu ni wa kumwaga ambao hulipwa na serikali, mishahara na malupulupu yao hawayagusi, je hii ni haki? Mshahara na malupulupu wayapatayo ni kwa ajili ya kujikimu katika maisha au kama watumishi wengine wa umma au ni kwa ajili ya nini?

Suala hili linatakiwa kuangaliwa upya, maana niliona siku moja jengo la ubolozi wa Tanzania umoja wa Mataifa kule Westchester County, NY ambalo ni mali ya Tanzania, hata ukarabati umeshindikana, kufyeka nyasi hakuna, matofali toka ukingo yanaporomoka, hadi kufikia serikali kununua majengo mengine wakati like kingetunzwa lilikuwa zuri na kubwa na lililo sehemu iliyotulia kama bongo upo Oysterbay vile.

Wakuu wengi wa Marekani na Ulaya utawaona siku za mapumziko wamevaa kaputula na kushika mowing mashine kusafisha mazingira ya nyumba zao na ni sehemu ya mazoezi kiafya, bongo ni kutulia kwenye viyoyozi wakinywa konyagi na wiski na serikali itume watu kusafisha hadi chumba cha kulala, huu ni umwinyi na utemi ambao ulimwengu wa leo hauko.

Je, hawa utawaambia wamsaidie mke wake kubadilisha dipper ya mtoto? Subutu.
 
Yote tisa lakini vyoo vya balozi zetu ni vibovu na vichafu kupita kiasi, sijui maafisa wa ubalozi huwa wanajisitiri vipi.

Mimi nashauri bora hizo balozi wazifute tu,maana hazina msaada wowote, tubaki na mabalozi wa heshima tu.
 
Mabalozi wenyewe hawana tija kwa nchi, acha wateseke tu! Badala ya wao kutembelea mashamba ya mananasi wanasubiri mkulu akakague hadi mashamba ya nyanya. Wanafanya nini huko hawa? Kama vipi warudi.
 
Back
Top Bottom