Mabalozi wa CCM Igunga wataka kujivua gamba; Wadai rushwa ilitumika

waende cuf maana wana elements za kushawishiwa na elfu kumi kumi hizo
Mabalozi 18 wameamua kukihama CCM kwa kile walichodai ni ubadhirifu wa resources isivyohalali wakati wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na rushwa. Hawajaamua wanahamia chama gani bado but CDM yawezakuwa kimbilio. Walitoa mfano wa rushwa kuwa ni katika mtaa wa KOKOTO ambapo laki tano zilitolewa kwa watu 48 na iliposhindikana kugawiana kwa haki ndio siri zikaanza kuvuja, wanadai pesa zilizomwaga zilikua kufuru lakini pia walilazimishwa kuvunja sheria ili kulinda maslahi. Sijui kama CCM watafika
Source: WAPO RADIO
 
mabalozi 18 wa ccm wa igunga wamejivua gamba.wamesema ccm imeshinda kwa sababu walikuwa wanatoa rushwa na ushahidi upo na wanaeleza pia jinsi m/kiti wao alivyokua anasambaza 45mil.wasema ijumaa ijayo watatangaza wanaenda chama gani.
wakati huo huo aliyekua mgombea wa ubunge kupitia cuf kasema hatagombea tena kwa sababu hana hela.anasema angekua na hela angeshinda.anasema kura zake 9000 zimenunuliwa na ccm.
source;ABDALLAH RAMADHAN WA WAPO RADIO
MY TAKE;
hela za rushwa zinaisambalatisha ccm.mia

Nyie chadema si ndio mlisema wakipewa rushwa wapokee ila kura wawape nyie, sasa imekuwaje tena baada yakushindwa ndio mnaleta haya ?
 
Unaweza kuona jinsi gani inchi yetu ilivyokosa uzalendo kuanzia magogoni hadi kwa mjumbe wa nyumba kumi kumi. Unadhani tutaweza kuurudisha uzalendo kwa kuendelea kujipendekeza kwa hawa wazee wetu wa CCM! Tusahau.

Ni kuamua liwalo na liwe, 2015 ni mbali sana ila kwa vile wengi wetu bado tunaona shida tulizo nazo hazijasababishwa na serikali yetu, basi ngoja tuendelee kuelemishana kwanza.

utamwelimisha nani huko kijijini ilihali vyama vya upinzani havina hata matawi? Ila kuna swali huwa najiuliza mjumbe wa nyumba kumi ni kwaajili ya kusaidia matatizo ya wanachi wanomzunguka au ni kwa ajili ya chama? Hivi ni laziama mjumbe wa nyumba kumi awe mwana ccm? Hivi wanateuliwa au wanchaguliwa na nani? Je atakuwa yupo kwa matakwa ya kuwasaidia wanachi au chama? Je anatumikia chama au ni watu? Hii nchi mi naona bora iuzwe tu hadharani kila mtu agawane chake akafie mbali kuliko wachache wanavyoiuza kimya kimya Utafikiri hatuoni. Wajinga ndio waliwao.
 
Kuna siku niliandika humu jamvini kuwa uchaguzi ukiisha wanaigunga wataachwa na njaa zao wakati wenyewe wanakula bata dom,hao mabalozi hawana lolote ni kwamba walipewa ahadi hewa,wametumika kugawa mahindi na maji,watu wamechukua jimbo wao wamebaki wanaota jua.nitawashangaa sana kama watahama chama,wasubiri miaka 4 ya kazi waliyoifanya ipite.
Hii inaitwa Die slowly!
 
haya hao ni wanaCCM wenzao, sie tusemeje tena? labda kuwalaumu TakoKuru kwa kukaa kimya
 
mabalozi 18 wa ccm wa igunga wamejivua gamba.wamesema ccm imeshinda kwa sababu walikuwa wanatoa rushwa na ushahidi upo na wanaeleza pia jinsi m/kiti wao alivyokua anasambaza 45mil.wasema ijumaa ijayo watatangaza wanaenda chama gani.
wakati huo huo aliyekua mgombea wa ubunge kupitia cuf kasema hatagombea tena kwa sababu hana hela.anasema angekua na hela angeshinda.anasema kura zake 9000 zimenunuliwa na ccm.
source;ABDALLAH RAMADHAN WA WAPO RADIO
MY TAKE;
hela za rushwa zinaisambalatisha ccm.mia

Nahisi mabarozi hao wametoswa mgao.waliowatumia wamepata wanachoitaji wamewakimbia.?
Je wanaweza kuyasema hayo mahakamani au.?????
 
Hawa mabalozi wamepima hali ya siasa za igunga na wameona 2015 kutakuwa na kazi ngumu sana ccm kushinda sasa wameanza kucheza na akili za wanaigunga ili waonekane wapo safi.
 
mgombea pekee kupitia chama cha kafu amesema hagombei tena ubunge eti yeye ni masikini hawez kuhonga kama ccm ,
hata mtaji wake 11elfu umenunuliwa na ccm.
Chanzo cha habari wapo fm.
Je mnamsikitia au amestahili?

si kweli huyu jamaa ni baada ya kushindwa sasa inabidi atafute pa kutokea
 
Naona chakula cha mgao kimeisha na hamna mgao tena. Ngoja njaa iwatengeneze watanyosha tu maneno!
 
Kuna siku niliandika humu jamvini kuwa uchaguzi ukiisha wanaigunga wataachwa na njaa zao wakati wenyewe wanakula bata dom,hao mabalozi hawana lolote ni kwamba walipewa ahadi hewa,wametumika kugawa mahindi na maji,watu wamechukua jimbo wao wamebaki wanaota jua.nitawashangaa sana kama watahama chama,wasubiri miaka 4 ya kazi waliyoifanya ipite.
Hii inaitwa Die slowly!
Mkuu hiyo inaitwa killing softly rather than die slowly.
 
Hii dhambi itatafuna tu
Hata Kafumu itamtafuna tu
CCM wote itawatafuna tu
Labda kama Mungu hayupo.
 
madebe ya unga yameisha ndani na njaa imeanza kuwakong'ori

mabalozi 18 wa ccm wa igunga wamejivua gamba.wamesema ccm imeshinda kwa sababu walikuwa wanatoa rushwa na ushahidi upo na wanaeleza pia jinsi m/kiti wao alivyokua anasambaza 45mil.wasema ijumaa ijayo watatangaza wanaenda chama gani.
wakati huo huo aliyekua mgombea wa ubunge kupitia cuf kasema hatagombea tena kwa sababu hana hela.anasema angekua na hela angeshinda.anasema kura zake 9000 zimenunuliwa na ccm.
source;ABDALLAH RAMADHAN WA WAPO RADIO
MY TAKE;
hela za rushwa zinaisambalatisha ccm.mia
 
Watoe ratiba ya Bariadi kwa Chenge na Monduli mechi zihamie na huko pia baada ya rasharasha ya Igunga.
Baada ya ccm kuonja joto la jiwe Igunga, hakuna atakayevuliwa gamba tena. EL na AC wataendelea kupeta kama kawa.
 
Kumbe Abdallah Ramadhani anafanya kazi pale kwenye radio ya wapendwa!
ww umejua leo!!!mbona wako wengi tu wanaofanya kazi kwa wapendwa sio huyo tu, Huko hakuna ubaguzi kama kule unako kujua ww. samahani wandugu hivi mbona sijaskia tamko la kuwapongeza wanaIGUNGA kwa kuitikia wito wa wale jamaa waliosema w/nchi wasiipigie kura CDM. Au maadamu wamemchagua waliesema achaguliwe basi w/chi hawasitahili kupongezwa? Jamani tafadhali kwa kutumia majukwaa yaleyale toeni tamko la kuwashukuru wanaIGUNGA kwa kukubali ombi lenu
 
mabalozi 18 wa ccm wa igunga wamejivua gamba.wamesema ccm imeshinda kwa sababu walikuwa wanatoa rushwa na ushahidi upo na wanaeleza pia jinsi m/kiti wao alivyokua anasambaza 45mil.wasema ijumaa ijayo watatangaza wanaenda chama gani.
wakati huo huo aliyekua mgombea wa ubunge kupitia cuf kasema hatagombea tena kwa sababu hana hela.anasema angekua na hela angeshinda.anasema kura zake 9000 zimenunuliwa na ccm.
source;ABDALLAH RAMADHAN WA WAPO RADIO
MY TAKE;
hela za rushwa zinaisambalatisha ccm.mia

WAPO radio ni radio yenye mrengo wa Chadema. Ni mali ya kanisa pasi na shaka.
 
Back
Top Bottom