"Mabala wa mabalaa" Ni Nani?

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,701
Katika gazeti la Raia Mwema kuna sehemu hii ya makala za "Aya za Ayah Binti Hidaya". Mwandishi wa makala hizi licha ya kuwa na ujumbe mzito lakini huwa zinakuwa zimeandikwa kwa namna ambayo inavutia sana kusoma. Mtu unasoma ukiwa unatabasamu hata kama ujumbe unakera.
Naomba kumjua mwandishi wa makala zile ambae anajitambulisha kama MABALA WA MABALAA...
 
ninacho fahamu ni mzungu mwenywe uwezo mkubwa wa kuzungumza na kuandika kiswahili kwa ufasaha.mengine zaidi kuhusu yeye wadau wengine watachangia,
 
Richard Mabala, aliyeandika kitabu cha Mabala the farmer, ailkuwa ni mwalimu wa secondary Mzumbe kama sikosei na baadaye akaacha, na kuwahi kuajiriwa UDSM, sikumbuki vema alikuwa idara gani na sasa nafikiri anafanya kazi na mashirika mbalimbali ya kiuana harakati. Ni mzungu aliyezaliwa na kukulia bongo (Tabora kama sikosei - mnyamwezi wa kizungu), ana uraia wa bongo na anayeipenda Tanzania kuliko nchi ya babake.
 
Yeah..Anaitwa Richard Mabala...ni Muingereza nafikiri,alioa Mtanzania na hivyo akaamua kubadilisha jina lake la Ukoo na kuchukua hilo la Mabala...Ni Mtaalamu wa Literature,ameandika articles nyingi lakini ni maarufu sana kwa vitabu vyake ambavyo vimetumika sana kipindi fulani cha 90's kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza katika somo la kiingereza,vinaitwa Mabala the farmer na Hawa the Bus driver....
 
Precisely!
 
huyu ndo yule richard mabala aliyekuwa na katuni ya mzungu mtaani. Ni wahapahapa kitu kama mabala watu wa wapi?
 
Ni raia wa kitanzania anaitwa richard mabala ni mmoja kati ya wazalendo wachache waliopo tz anaishi Africa sana siza Dar es salaam. Nasikia ana wake wawili mmoja ni mzungu na mwingine ni mwafrika

Jina lake halisi ni Richard Satewite, Lakini alinogewa NA nswalu NA matobolwa ya Tabora akaamua kuachana NA Satewite, NA kuchukua Mabala. Alifundisha Chang'ombe Chuo cha Ualimu, ameifanya UNICEF etc
 
Kumbe ndiye aliyeandika Mabala the farmer!!
Pia ni mwandishi wa makala katika gazeti la Mwananchi Jumapili...??
 
Jina lake halisi ni Richard Satewite, Lakini alinogewa NA nswalu NA matobolwa ya Tabora akaamua kuachana NA Satewite, NA kuchukua Mabala. Alifundisha Chang'ombe Chuo cha Ualimu, ameifanya UNICEF etc
Mkuu angalia maandishi yako! usijeleta kizaazaa
 
Dah kwa kusoma makala zake huwezi pata picha wala ingia akilini kama mwandishi ni mzungu kwa jinsi anavyotumia kiswahil fasaha, na kwa kutumia lugha ya kuchombeza haswaa kama amezaliwa na kukulia pwani....

Nashukuru kwa mtoa post na wachangiaji na mimi leo nimemfahamu mababala wa mabalaa ni nani...
 
Jamaa huwa nasoma sana makala zake ndani ya raia mwema na mwananchi-leo ndo nafaham kua ni mzungu,thanx jf,anaboresha kiswahili fasaha
 
Aiseee.....leo usiku huu nimemuona akihojiwa bbc nikashangaa sana, siku zote nilijua ni mswahili mwenzetu kumbe ni mzungu?? Ni mwanafasihi mzuri wa kiswahili...
 
Back
Top Bottom