Mabaka kwenye Nyayo - Msaada tafadhali

Katibukata

Senior Member
Dec 27, 2007
182
11
Wadau,
Kwa mwezi mmoja uliopita nimekuwa natokwa na dizaini fulani ya mabaka kwenye sehemu ya juu ya unyayo . Yaani ile ya rangi brown ya kukanyagia inatokea kama mabaka juu ya unyayo karibu na ankle. Ukiniangalia visigino na sehemu ya juu unyayo nina mabaka lakini hayaumi.

Wadau hii nini? naweza kutumia dawa gani? Saidia.
 
Katibu Kata....kama mabaka hayo (especially kama ni meusi) yapo kwenye mguu mmoja tu na hayajasambaa mguu mzima, na kama umri wako ni miaka 40 au zaidi...tafadhali timua mbio kwa daktari (surgeon) akucheki na ahakikishe kwamba sio Malignant Melanoma!
 
Ahsante Dr. Riwa,
Umri wangu ni chini ya miaka 35. Mabaka si meusi. Sijui kama nimeeleweka, yaani ile rangi ya unyayo(brown ) inaonekana kwenye ngozi iliyo juu ya kisigino na vidiole vya miguu kwa dizaini ya mabaka-mabaka. Ukiniangalia kwa mbali utadhani nimeota sugu nyingi vidoleni na sehemu ya juu ya visigino karibu na ankles.
 
Back
Top Bottom