mabadiliko ya tabia na shule za kidini

anti-fisadi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
368
31
Imekuwa ni tabia ya wazazi wengi kupima viwango vya shule kwa kuangalia matokeo ya mitihani ya mwisho au wengine kuangalia mtoto mmoja mmoja wanaokutana nao na basi kufikia uamuzi wa kuwahamishia au kuwaanzishia elimu yao kama ni vidudu au msingi huko.

Ni wachache sana wanaofanya utafiti wa kina,kuangalia njia zinazotumiwa kuwafanya watoto wafikie hapo au pia kufuatilia na kujua tabia mbalimbali zinazojitokeza shuleni hapo kutoka kwa wazazi kadhaa. Unakuta wazazi wakijibidiisha kuwatafutia watoto wao shule wanazodhani ni bora bila kujua undani wa hizo shule,kiasi kwamba hata wazazi wengine hudiriki mpaka kulia watoto wao wakikosa!

Nilipata mshtuko pale niliposikia shule kadhaa za kidini zikiripotiwa na matukio ya kudhalilisha watoto na baadhi ya wazazi na walimu wakijua hilo na kuliacha liendelee bila kuchukua hatua sahihi. Moja ya shule hio ipo mbezi beach karibu na st.Gaspers church. Inaripotiwa kuwa watoto kadhaa wameshadhalilishwa kijinsia wakike kwa wakiume lakini bado siri inaendelea na wakati huohuo watoto wakiendelea kuharibika.

Hivi tutakuwa na taifa la kesho la aina gani,kama upuuzi kama huu ukiendelea kukua na kufichwa? Tukiangalia upande mwingine,chanzo cha tatizo sio watoto bali wazazi wanaopuuzia malezi bora ya watoto wao,wengine wakizani malezi ni kazi ya dada wa nyumbani. Mtoto kuchomekwa vijiti,penseli,vidole na vitu kama hivo na wenzake sehemu za siri. Hivi wanatoa wapi fikra kama hizi za kishetani au wazazi wao wanafanya hazarani au wanakuwa wakifanyiwa na madada wa nyumbani??

Matukio haya ni mengi,kuna familia imevunjika kutokana na haya;mzazi mmoja kujua mtoto wao alifanyiwa kiasi cha kuanza kujinyea hovyo na kumficha mwenzake, badae mwenzake alipojua tatizo na kwamba alifichwa ikawa ndio mwisho wa ndoa yao,inasikitisha sana!

Kumbe tatizo ni kubwa zaidi,kiasi cha kuharibu ndoa na sio mtoto pekee! Je polisi,wananchi,mamlaka za ustawi wa jamii, wizara zipo kuchunguza haya mambo mashuleni!? Au mwisho wao ni kwenye kutoa vibali na kupokea malipo!

Nitaendelea kutoa taarifa zaidi punde zikiitajika. Unaweza kunitumia meseji binafsi nitakujibu. Jamani,wazazi tuwe makini hizo ada mnazolipa ni kubwa sana watoto wenu kupuuzwa.

Kama uandishi ni mbovu,tusameheane! Ila nina uhakika nimeeleweka.
 
Back
Top Bottom