Sirdirashy
JF-Expert Member
- Jan 26, 2014
- 3,223
- 2,950
Lkn km kweli kuhusu miaka mitano aku
Kweli posho tamu...Mrema hayupo peke yake!
View attachment 184681
Chapa usingiziii...ukiamka toa ushauri na kuunga mkono hoja, bingo?
Kila mtu ni shahidi jinsi gani nchi yetu ya Jamhuhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyopiga hatua kubwa ya maendeleo hasa katika uongozi wa mh.Rais JK.Kwa muda mfupi nchi yetu imefanya vizuri katika nyanja zote,uchumi wetu umeimarika kwa kasi ya ajabu.Sekta za elimu,afya,kilimo,utawala bora,demokrasia na uhusiano wa kimataifa ni mafanikio ya hali ya juu ktk uongozi wa mh.Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,ndg.Jakaya M.Kikwete.Hivyo basi katiba ijayo inapaswa iwe na kipengele cha kumuongezea muda rais aliyefanya vizuri km mh.JK ili aweze kukamilisha kazi ya kuwatumikia Watanzania.Miaka mingine 5 inatosha ili amalizie kutuletea maendeleo.Wapinzani hasa Chadema hamna chenu,chama chenyewe kinakwenda mramba.Mmeshindwa hata kutuma mwakilishi Sauz kwenye msiba wa mzee Mandela.Napenda kuwasilisha.
Iwapo katiba ingeruhusu rais Kikwete kugombea tena awamu hii, je kwa utendaji wake na utekelezaji wa ilani na ahadi zake tangu alipoingia madarakani angeweza kuibuka tena kwa ushindi urais 2015?
Unatumia nguvu nyingi kupingna na hoja ndogo sana. Dig deep kwenye issues. Nasema hivi, JK amefanya mema mengi kwa Tanzania pamoja na Changamoto za kiutawala anazokutana nazo. Kubali hoja kwa hoja, pinga hoja kwa hoja. Hayo mengine unayoyasema ukayaseme kwa wenzako mnapokuwa mnasukana nywele au mkiteka maji...
craaaaaaa.........!!!!
AiseeHivi JK ameshaelewa sasa kinachoifanya Tanzania kuwa maskini? Mimi naona kuwa JK apunguziwe muda wa kukaa Ikulu, miaka 5 mingi sana! Wakati wa Serikali zilizopita JK alikuwa Waziri wa Nishati na Madini na alisaini mikataba mibovu ya madini! Pia baada ya kujua uovu uliofanywa na Serikali ya Mkapa, aliamua kuyafumbia macho na kuamua kudai kwamba "mzee (Mkapa) aachwe apumzike" kwa ufisadi aliofanya!
Tusidanganyane JK akiendelea kuwa Ikulu Tanzania itakuwa kama Somalia!
Hakuna shaka kuwa wapuuzi ni wale wanaoupinga ukweli. Hata kama una chuki binafsi na JK lakini kusema ukweli mema tunayaona.
Mradi wa mabasi yaendayo kasi umeshaanza, upo hatua ya mwanzoni
Flyovers nazo zipo mbioni...
Mnataka mfanyiwe nini watanzania??
tumfanye rais wa maisha ..............
Au tumfanye mfalme..........
KamweneQuadratic
Ulichosema ni kweli tupu,Rais JK asiongezewe tu miaka 5 bali Katiba mpya imtangaze kabisa kuwa ni Rais wa milele wa TZ kwani kaifanyia mengi sana nchi yake Tanzania
Mosi;katupa umeme wa uhakika kabisa TZ;chini ya utawala wa maulana JK kwa kweli wa TZ wanafaidi umeme wa bei rahisi tofauti na viongozi wengi waliotangulia.
Pili;hali za huduma za afya TZ ni za juu sana chini ya utawala wa JK hata ikafikia ile kadhia ya kulala chini akina mama wajawazito pale Mwananyamale,Muhimbili na karibia hospital zote za TZ sasa haipo tena
Tatu;Rais wetu JK kadhibiti sana mfumuko wa bei na hivi sasa chini ya utawala wake shupavu shilingi yetu imepanda sana bei kulinganisha na bei ya dola ya kimarekani
Nne;wakulima hivi sasa wana uhakika wa kupata bei nzuri ya mazao yao kwani JK kaimarisha sana soko la ndani na la nje kwa products zitokazo mashambani mwetu hasa alipowapa pembejeo za kisasa wakulima wa TZ
JK kaifanyia mambo mengi sana TZ na mengine nitaendelea kuyataja siku zinazokuja lkn sidhani kama itakuwa vibaya kutoa wazo langu kwenye katiba mpya imtangaze JK kama Rais wa milele wa TZ ili kuenzi mazuri aliyoyafanya kwa miaka 5 tu ya uongozi wake!