Mabadiliko haya kwa gharama gani?

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
718
703
Taarifa zinasema kuwa mamlaka ya mawasiliano nchini TRCA kesho Ijumaa Desemba 2.2011 itaendesha mkutano wa watangazaji nchini huku mada kuu ikiwa ni mabadiliko kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Digitali.

Mkutano huo unaofanyika kunduchi Beach utawakutanisha wadau wa masuala ya utangazaji kuangalia jinsi tanzania inavyoelekea kubadilisha mfumo wake wa utangazaji ikiwa ni makubaliano ya kidunia kwamba ifikapo mwaka 2015 watangazaji wote watakuwa katika mfumo wa digitali.

Aidha inaelezwa kuwa Tanzania itaanza utekelezaji wake kwa sekta ya Television ambapo ifikapo desemba 31 mwaka 2012 itahama kutoka analogia kwenda digitali.

Binafsi nina changamoto ambazozimekuwa zikisumbua fikra zangu na ambazo pengine wajumbe wanaohudhuria mkutano huo wataweza kuziangalia na kuzipatia ufumbuzi.

Changamoto ya kwanza ninayoiona kwangu ni TCRA: mamlaka hii inanipa shida katika utekelezaji wa majukumu yake. Wakati ikitangaza kuwa watumiaji wa television wanapaswa kubadilika ifikapo Desemba 31 mwaka kesho, imeshindwa kutoa elimu ya kutosha kwa umma, hasa wanaoshi vijijini.

Jitihada nyingi imekuwa ikizielekeza kutoa semina: zinazofanyika mijini, kutoa matangazo kwneye magezti yanayosomwa miji, na vipindi vichache vya radio na Television.

Watu walioko pembezoni mwa nchi wameachwa bila kufikishwa ujumbe inavyostahili, jambo ambalo linaweza kupelekea kukosa haki yao ya msingi ya kupata taarifa baada ya kuanza kwa mfumo mpya.

Nimefika Ngara hivi karibubni na katika mazungumzo yangu na wwadau mbalimbali imebainika kuwa hakuna elimu au utaratibu unaoandaliwa kwa ajil ya kuwawezesha kubadilika kutoa televison za sasa kwenda Digitali.

Wakazi wengi wa wilaya hiyo hupata matangazoya television kwa njia ya sateliti : TRCA, nimeona wengi wanatumia receiver ambazo zimeandikwa kuwa ni Digial receiver, lakini hawa nao wanatakiwa kununua vingamuzi !. Je haiwezekani vingamuzi hivi vikatumika katika mfumo mpya? Tofauti yake na vingine ni nini?, majina?

Suala hli la kutoka analojia kwenda digitali ni suala mtambuka, linagusa kila sekta. kiuchumi, kijamii, kisiasa, utamaduni n.k

Naomba tuangalie suala hili katika mtazamo wa kiuchumi. Tunaweza kutaelezwa ni gharama kiasi gani zitatumika kubadili seti za television katika nyumba zote Tanzania kutoka analojia kwenda digitali?

Nafahamyu familia ambazo zina seti tatu hadi nne. Hizi zitaingia gharama kiasi gani na mwisho wa siku taiifa litaigia gharama kiasi kagi katika hili.
Na hizi seti za television ambazo hazitatumika tena, zitakwenda wapi? Tumeangalia mazingira yataathirika kiasi gani?

Naelewa pia kuwa ifikapo desemba 31, 2012 mfumo huu utabadilika, kama ilivyopangwa kwani inavyoonekana TRCA huwa inaweza kuwabana watumiaji wa kawaida ambao wametelekezwa na mfumo mbovu wa kuendesha biashara hapa Tanzania.

Tuliona wakati wa kusajili line za simu za mkononi namna makampuni ya simu yalivyoweza kusimama na kufanikiwa kusongeza muda wa usajili mara kadhaa, lakini hadi sasa tunaona kuw ainawezekana kununua line ya simu na kuitumia bila kuisajili!, makampuni ya simu yameachwa bila kuchukuliwa hatua.

Katika suala hili ambalo litawawezesha wafanyabiashara wajanja wenye vituo vya television kujinufaisha kwa kupata malipo ya kila mwezi kutoka kwa watazamaji wake, TRCA haiwezi kuchukua hatua.

AGAPE TV wamelifanya hili kwa muda mwingi (huku wakitangaza kuwa malipo ya mwezi hayana budi kulipwa ) lakini TCRA haikuweza/ haijaweza kuchukua hatua , wakati tunafahamu kwamba sio channel zote zinapaswa kuwa za kulipia
Suala la mabadiliko halina budi kuwa la msingi katika maisha ya binadamu, lakini hatuna budi kuangalia kama mabadiliko tunayoyakusuda yanaweza kutekelezwa katika mazingira yetu.

Utunaambiwa kuwa ifikapo mwaka 2015 , duna yote mfumo wa utangazaji hauna budi kuwa Digitali, Sawa, lakini je dunia yote itakuwa sawa kijiografia na kiuchumi katika kufikia suala hili.

Ifikapo 2015 au hata 2012 Mkazi wa Kashozi kule karagwe atakuwa katika mazingira sawa na mkazi wa Osnabruck Ujerumani kuweza kutumia mfumo huu?
Tumeyaandaa mazingira yetu kiasi gani?, kwanini tunasahau maneno ya nyerere aliyepata kusema kuwa IMF haijapata kugeuka kuwa international Ministry of Finance . Hawa ITU wanaotaka dunia yote kuwa sawa ifikapo mwaka 2015 ni akina nani?, nani atafaidika na mabadiliko hayo?

Sitaki kuingia sana katika mabadiliko kwenye mfumo wa radio kwani nafikiri huko kutakuwa na mambo mengi zaidi.

Tunaambiwa kuwa kutakuwa na kampuni tatu ambazo zitayumika kurusha matangazo huku vituo vyote vya radio vikitakiwa kupitisha matangazoyake kwenye kampuni hizo.

Ukiwa Ngara, huwezi kupata matangazo ya TBC, au AGAPE ambayo ndio imepewa leseni ya kurusha matangazo ya vituo vya radio ya kijamii , sasa hawa wakazi wa maeneo hayo wataweza vipi kupata haki yao ya kupata habari
Suala hili pia linajitokeza pia katika television wapo wanaonunua ving.amjuzi lakini hawapati matangazo na hakuna hatua zinazochukuliwa.

Leo wapanda pikipiki wanaofanya biashara yakubeba abiria wengi wao wana aina ya radio ambazo zikifunguliwa zinaina ya Trasmitter ambazo huingilia matangazo ya radio zilizoko katika umbali fulani kutoka chombo kilipo. TRCA zijui kama wanalijua hilo na wananchukua hatua gani dhidi ya teknolojia hiyo
Lakini pia hawa watu waliowekeza katika miundo mbinu ya kurusha matangazo kwa njia ya radio (minara) watatakuwaje wakati huo ukifika.

Binafsi naona kama tunalenga kutaka kuwanufaisha watu chache( kampuni za kurusha matangazo) kwnai wakati tunafikiria kutoka analojia kwenda digitali, suala hili lilipaswa kuachwa kwa wamiliki wa radio na televison kuamua wenyewe kwenda na mabadiliko.

Naamini kwamba kama wakiachwa wenywee bila msukumo wa mambo yaliyo nyuma ya pazia, wamilki hawa wataona umuhimu wa kubadili mfumo wao wa utangazaji na hivyo kuepelekea mabadiliko hayo kwa wasikilizaji au watazamaji wao.

Tukiyafikiria hayo kuna sua la la matumizi ya Computer kupata matangazoya radio na television huko TCRA imejipanga vipi?

Leo radio nyingi zinarusha matangazo yake kwenye internet kwa njia mbalimbali haya makapuni yatashughulikia pia aina hii ya matangazo?
Lakini kubwa ninalotazama ni kuwa watunga sera wetu pamoja na watendaji wao wana mtazamo hasi juu ya Tanzania.

Wanaitazamana Tanznaia kwa jicho ya Dar es salaam, ndio maana utasikia mipango kama ya kujenga barabara za kupitia juu katika taifa ambalo bado kuna shule ambako wnaafunzi wake wanasoma wakiwa chini ya miti( shuleya msingi kagali, wilayani Ngara).

Wakati pato la wastani la mkazi w awilaya ya Ngara ni shilingi 670 kwa siku kuna watu wanafikiria kuhamisha matangazo kutoka analojia kwenda digitali ili kuboresha usikivu

Labda kwa sababu televisoon ni suala la anasa na sasa na raddio zinaelekea huko, lakini kuna radio (sio zote) za kijamii ambazo zina manufaa makubwa kwa wananchi kuliko tunavyotazama.

Ingekuwa abora TCRA na mabwa na wakubwa wanaofikiria dunia kuwa sawa ifikapo mwak a2015 watafute mbinu za kumsaidia mkazi wa ngara kuongeza pato lake kutoka shilingi 670 kwa siku kuliko kujaribu kumkandamiza.

Nawatakia mkutano mwema na pengine mtatusaidia kupata majibu ya dukuduku zangu, kwani imekuwa vigumu sana kwa TRCA kujibu hoja mbalimbali zinazowekwa kwenye mtandao wake hususan ukurasa wa malalamiko ya wateja ambayo kw ahakika yapo mengi. Makampuni yetu ya simu sina la kuongeza
Mabadiliko sawa lakini kwa gharama gani?
 
pia nashauri kuwa kuwe na vingamuzi vilivyoungana badala ya kumpa mzigo mwananchi kununua receiver mbili au tatu
 
Back
Top Bottom