Mabadiliko gani yanatakiwa ndani ya CHADEMA?

Kintiku

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
617
319
Sio siri CDM ndo chama kikubwa cha upinzani, CDM ina self made wafuasi/mashabiki kuliko wanachama, CDM inapendwa na watu hasa vijana bila kushawishiwa kwa mikutano au vipeperushi. Pamoja na kudaiwa kuibiwa uchaguzi wa 2010, ukweli unabaki CDM ilishindwa uchaguzi pamoja na kuwa na ufuasi mwingine.

Leo naomba tuangallie upande wa pili ni makosa gani yalikifanya kishindwe uchaguzi (udhaifu wa ndani) na kinafanya nini hivi sasa kurekebisha hizo kasoro kwa siku za baadaye. Naona kama CDM kinakosa kitu fulani mahali fulani kukifanya kiwe chama chama cha kuwasemea wananchi-kuna mahali pana mushkeli hapajakaa sawa. Nina imani pakirekebishwa hapo, hata viongozi wakisema kuwa watu waingie bararabani watu watafanya hivyo bila kusita. Mfano idara yao ya habari na uenezi haiko active sana, ubunifu hakuna kabisa.

Natamani kuona CDM isiwe ''reactive chama'' yaani wao wanaonekana na kusikika kufuata matukio. Pia wawe wai kueleza misimamo yao kuhusu masula yanayokuwa kwenye public sana. Mfano, walifanya vema khs mafuriko, je kuhusu ushoga, je wao kutumika na EL au RA mbona hakuna tamko. Naona kama CDM kinahitaji kuwa na washauri ambao wako nje ya boski la uongozi, wachambuzi ambao hata sio wanachama lakini wanapenda mabadiliko.

Hebu tuwape ushauri CDM, wafanye nini ili wapige hatua nyingine kubwa kutoka hapo walipo leo ambapo naona kama kuna ka stalemate fulani hivi. Kama unaonyesha udhaifu basi jaribu na kupendekeza ufumbuzi wake
 
Check hapo kwenye Red utaona huu jamaa alikvyo chini katika kuwanza,unaweza kudhibtisha kama CDM kilishindwa mwaka 2010,Je wewe huoni busara zinazotumika kuepusha mambo maana wangekuwa CCM wakinyimwa hata kufanya mkutano tu wa kuhamasisha michango na kugawa Tshirt mweeeee ,mshekeli gani unaona huo ndo uchochezi,sio ule wa Kibanda ule unaelemisha watu,CCM mnataka watu wawe mbumbumbu ili mpate loophole,subiri watu waende shule ndo mtajua kuwa sasa ndo kwenda kisayansi zaidi.Hakuna kitu ambacho watu wanatumia akiri kama CDM ili kudeal na hao magamba.
Kwa hiyo wewe unataka VITAkama Magamba utaona vyombo vyetu vya usalama viko imara----Imara vyombo vyenu sio vyombo vya taifa vya usalama.wewe unajua kabisa watu wameiba kura halafu unachekacheka tu.
CDM kina kila kitu ,ushauri watu wako kibao ,hata wewe pia unashauri japo hujuwi kama unashauri.Ukisema vibaya CDM ujuwe wewe unaitangaza tu ,sifa ya kuisema vibaya watu ndo unazidi kuipenda.
Nenda kwenye Basi,vinjiweni,baaa ,shuleni, misibani ukasema hayo maneno yako uone,au usiende mbali muulize Nepi alivyozunguka nchi nzima ,atakupa jibu ,wewe muulize tu.
 
Ni swali zuri sana lakini hebu kaanze nalo CCM ndio uje ukapitie na jibu huku baadaye. Kuna hoja nyingine bado?
 
kawashauri magamba kwanza njia nzuri ya kumuondoa el kwenye chama,halafu mbona swala la jk kuileta richmond kwenye hiyo post yako hujaongelea kabisa, wape cdm ushauri pia juu ya hilo wafanyeje
 
Unaweza kuwa na point lakini umejichanganya mwenyewe hadi hueleweki.
Hili la kuchakachuliwa huwezi kulipinga kirahisi kwakuwa tu NEC ilimtangaza JK kuwa mshindi. Hadi leo hii NEC hawajathubutu kutoa matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Nenda tume ama angalia kwenye tovuti yao, hakuna kitu kama hicho.

Kitu kingine usichoeleweka ni kuwapa watu kazi ambayo wewe mwenyewe umeshindwa kuonyesha mwelekeo.

Unataka watu waonyeshe madhaifu na kutaja namna ya kuondokana na udhaifu huo. Tuanze na wewe mwenyewe kuna lolote umeliona na nini ushauri wako?
 
Yale ya kuking'o haraka zaidi madarakani ile kampuni ya mafisadi CCM kusudi taifa lipate ahueni.
 
Nadhani nimewasilisha vibaya: Ngoja niseme hivi.

  1. Je Chadema kifanye mambo/ marekebisho gani ili uchaguzi ujao kichukue dola. Maana kama kuibiwa na NEC ni toka vyama vingi vilipoanza. Ina maana CDM itaendelea kuwa hivo hivo so long as wanaibiwa na NEC?
  2. Mabadiliko gani ya kiutendaji yanahitajika ili kupiga hatua toka hapa CDM ilipo leo?
 
We kwani umeona utendaji una kasoro au una mafanikio?
Jiulize uchaguzi wa 2010 chadema kimepata mafanikio zaidi kuliko chama chochote cha siasa nchini Tanzania, we unaongelea uchaguzi mdogo wa Igunga ccm waliochakachua kura?
 
CDM wanatakiwa kupata viongozi ngazi ya serikali ya vitongoji, vijiji na kata ili kujihakikishia ushindi katiaka chaguzi zote zinazo kuja, kwani huko ndiko magamba utumia kuiba kura.
 
Leo naomba tuangallie upande wa pili ni makosa gani yalikifanya kishindwe uchaguzi (udhaifu wa ndani) na kinafanya nini hivi sasa kurekebisha hizo kasoro kwa siku za baadaye. Naona kama CDM kinakosa kitu fulani mahali fulani kukifanya kiwe chama chama cha kuwasemea wananchi-kuna mahali pana mushkeli hapajakaa sawa. Nina imani pakirekebishwa hapo, hata viongozi wakisema kuwa watu waingie bararabani watu watafanya hivyo bila kusita. Mfano idara yao ya habari na uenezi haiko active sana, ubunifu hakuna kabisa.

Kumbe Viongozi wa CDM ni wasikivu tofauti na wanachama wote- Hongera Mnyika kuja kuimarisha Kurugenzi ya Uenezi
 
mleta hoja ana mantiki ingawa watu mnampinga kishabiki. it is real critical to do SWOT analysis. on top of that nawashauri watumie Porter's 5 force model to analyze their "market" as illustrated below:

  1. Supplier Power: hapa tuchukulie kuwa ni vyama vya siasa vinavyojaribu kuuza sera na mipango kwa wananchi
  2. Buyer Power: hapa tunachukulia buyers kuwa ni wananchi watakaonunua sera za chadema
  3. Competitive Rivalry: What is important here is the number and capability of your competitors.
  4. Threat of Substitution: je wananchi wanaweza kuona mbadala wa Chadema kama chama kikuu cha upinzani? Je wanaweza kuamua kuto-support chadema na maisha yakaendelea?
  5. Threat of New Entry: hapa chadema wajiulize kama kuna potential entries like chama cha Hamad Rashid etc
 
Hongera sana mkuu Kintiku kwa kusimama kwenye hoja hatakama responses zilikuwa negative. Naungana na ww kwenye kutoa ushauri lakini kuna website ya CDM kunasehemu ya kutoa maoni moja kwa moja. Mi naamini katika kujadiliana ili kufikia perfection. Umeshauri kulikuwa na mapungufu kwenye idara ya uenezi naona utakuwa umeridhika sasa lakini bado tunapenda kuona hotuba ya rais inajibiwa ili kubalance taarifa kama alivyofanya Dr. Slaa wakati anatoa tathmini ya mwaka2011. Wewe(kintiku) ni mfano wa kuigwa ili kunurture tabia ya kujibu hoja kwa hoja.
 
kintiku nafikiri maswali yako chadema wameanza kuyafanyia kazi mojawapo ni swala la kuteuliwa mhe.mnyika kuimalisha kitengo cha uenezi wa chama. swala lako la matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana ni la kikatiba zaidi kuliko chama cha siasa. kwahiyo kama ungependa watanzania wenyewe kupitia kura zao ndio wachague Rais na siyo NEC kuwachagulia Rais basi inabidi ujiunge kwenye harakati za kudai mabadiliko ya katiba ya kweli yalioanzishwa na CDM.
 
Chadema itoke kuwa Chama kinachoendeshwa kifamilia zaidi na Ukoo wa Kichaga na kiwe Kitaasisi zaidi!
 
Back
Top Bottom