Mabadaliko kwa Mitihani kidato cha NNE na SITA.

Brightman Jr

JF-Expert Member
Mar 22, 2009
1,225
232
Wadau na wapenda masuala ya kielimu, kuanzia mwaka ujao kutakuwa na mabadiliko ya ufanyaji mitihani kwa wanafunzi wa vidato tajwa. Kidato cha Nne watakuwa wakifanya mitihani ya taifa kila ifikapo mwezi NOVEMBA badala ya Oktoba kama ilivyo sasa na kidato cha Sita mitihani ya taifa itakuwa ikifanyika kila ifikapo mwezi MEI badala ya Februari. Source TBC.
 
kuna mantiki gani hapo?kwani mda huu unamadhara gani na maandalizi ya watahiniwa au inaathiri vipi maendeleo ya elimu hapa nchini? Msaada tafadhali mtoa maada.
 
Bado wanaendelea na mkakati wa kuyumbisha sera za elimu... kweli hawa hawalitakii mema taifa letu
 
Hii wizara kila anayeingia anakuja na utaratibu wake. Waliotoka walitaka elimu ya msingi iishie std 6 na wengine walitaka stv 8. Tutakuwa na msimamo mmoja lini?
 
kuna mantiki gani hapo?kwani mda huu unamadhara gani na maandalizi ya watahiniwa au inaathiri vipi maendeleo ya elimu hapa nchini? Msaada tafadhali mtoa maada.

Sababu kuu ni kufanya usahihishaji (marking) kipindi cha likizo cha miezi ya Juni na Desemba shule zikiwa zimefungwa.
 
Jamani mbona hii wizara ya elimu mbona inataka kuwachanganya watu mara mtihani wa form six ni may leo tena wanasema mtihani utafanyika february.hii inaonyesha ni jinsi gani wizara hii ilivyokosa msimamo kwani inawachanganya tu wanafunzi
 
Mulugo: MTIHANI wa kidato cha sita 2013 NI MWEZI WA PILI siyo wa tano tena!. Pamoja na kwamba BARAZA la mitihani la taifa limelazimika kutoa ratiba 2 tofauti za mitihani ya kidato cha sita ndani ya wiki 2, RATIBA ya kwanza kabla ya mkanganyiko ndiyo itakayofuatwa!. Sasa mitihani itafanyika mwezi wa pili kama ilivyopangwa awali!..
 
Sababu za mabadiliko haya yaliyotangazwa na Naibu waziri wa Elimu Bw. Mulugo! ni hizi zifuatazo: 1. Utata wa wanafunzi kukalishwa shule baada ya kumaliza mitaala ya masomo miezi mitatu kabla ya mtihani;2. Utata wa Ongezeko la gharama za uendeshaji shule kwa kuhudumia wanafunzi miezi mitatu bila kuwa na jambo jipya la kujifunza. Huu ni mzigo kwa Wenye shule, wazazi na serikali.
 
Sasa vijana someni saana, muda ni mfupi. Pamoja na kwamba taarifa za mabadiliko haya bado hazijafika kiofisi mashuleni, mjue huu ni ukweli usiopingika. Huko mashuleni, wengine mnaweza kuzikuta ratiba mpya za mitihani mwezi wa tano, lakini ratiba inayokubalika ni ile ya awali ambayo pia iko shuleni.
 
Naibu waziri wa elimu bwana MULUGO, amesema MITIHANI YA KIDATO CHA SITA mwaka 2013 itafanyika mwezi wa pili kama ilivyopangwa awali. Hivyo ratiba ya mitihani kuanyika mwezi wa tano kwa wanafunzi waliokidato cha sita sasa imefutika. Waraka wa wizara utawahusu wanafunzi watakaofuata. SASA MLIOKATA TAMAA RUDINI DARASANI MSOME KWA NGUVU, PEPA MWEZI WA PILI 2013. JIANDAENI MUDA BADO UPO!.
 
ACHANA na wanasiasa wababaishaji. Matatizo ni makubwa kuliko unavyojua wewe!. KURUDISHA MTIHANI FEBRUARI NI MUHIMU SAAANA!. SABABU: Shule nyingi makini zinamalizia syllabus mwezi huu au mapema mwezi ujao, je, wangefundisha nini miezi mitatu iliyoongezwa? Nani angelipa gharama ya wanafunzi kuongezewa muda wa kukaa shule? SASA SOMENI KWA BIDII MSUBIRI MTIHANI FEB 2013.
 
KILICHOBAKI TULIENI MSOME KWA BIDII, Fanyeni mitihani, kisha INGIENI KWENYE SIASA MJE mlikomboe taifa toka kwenye ujinga huu!
 
Sababu za mabadiliko haya yaliyotangazwa na Naibu waziri wa Elimu Bw. Mulugo! ni hizi zifuatazo: 1. Utata wa wanafunzi kukalishwa shule baada ya kumaliza mitaala ya masomo miezi mitatu kabla ya mtihani;2. Utata wa Ongezeko la gharama za uendeshaji shule kwa kuhudumia wanafunzi miezi mitatu bila kuwa na jambo jipya la kujifunza. Huu ni mzigo kwa Wenye shule, wazazi na serikali.

Hatma ya wahitimu wa kidato cha sita itakuwa nini kuanzia 2014 katika kujiunga na elimu ya juu hapa nchini? Ilivyo sasa, Majibu yanatoka Mwisho wa April na mwanzoni mwa May. Udahili wa vyuo kupitia TCU unaanza April mpaka June. Applications TCU deadlines ni Early July. Notification of admission ni anytime August. Registration at Universities late Sept to early October. Swali linakuja kwamba ukibadilisha mihula ya Sekondari hawa wa kidato cha sita watajiunga lini na vyuo vikuu?

Hawa wenzetu wanapobadilisha mihula wanajua kuwa wanaathiri ratiba za vyuo vikuu? je, wakuu wa vyuo nao walihusishwa? TCU, HESLB???

Tusubiri Kasheshe 2014.
 
Kimsingi tatizo bado lipo na lina endelea kuitafuna wizara ya Elimu kujikuta kila mara inapata Mawaziri ambao niwajuaji. Mh. Mungai alibadili mfumo mzima wa Elimu bila kushilikisha wadau wowote.Hivyo binafsi pamoja na wadau wengine wa JF mnakubaliana na mimi kuhusu hilo,na pamoja na hayo Wanasiasa wote walikaa kimya.HIVYO NAWASIHI WANAFUNZI WOTE KUWA KATIKA MAANDALIZI WAKATI WOTE.HIVI NDIVYO ELIMU YETU ILIVYO."UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI".
 
Hv mbona huyu MULUGO ana maamuzi mazito sana kwenye hii wizara?
Sijawahi kumsikia waziri mwenye dhamana akitoa maamuzi yake?
 
Sababu za mabadiliko haya yaliyotangazwa na Naibu waziri wa Elimu Bw. Mulugo! ni hizi zifuatazo: 1. Utata wa wanafunzi kukalishwa shule baada ya kumaliza mitaala ya masomo miezi mitatu kabla ya mtihani;2. Utata wa Ongezeko la gharama za uendeshaji shule kwa kuhudumia wanafunzi miezi mitatu bila kuwa na jambo jipya la kujifunza. Huu ni mzigo kwa Wenye shule, wazazi na serikali.

Malalamiko kutoka kwa wazazi yalitolewa lini na nani waliyatoa kujustify hoja dhaifu kabisa hii!

Ieleweke kuwa shule nyingi sana za private ni za viongozi waandamizi ama waandamizi wastaafu, sasa hawa ndiyo wanatuharibia mfumo wa elimu nchini, hivi kweli kwenye shule zetu za kata kuna uwezekano wa kumaliza 'silabasi' kiasi cha kukaa hata wiki moja achilia mbali miezi mitatu?
Chunguzeni kwa makini.
 
kj.jpg kj.jpg Sasa kwa nchi yenye sheria mbovu, sera mbovu na rais dhaifu unategemea nini tena hapo?
 
Back
Top Bottom