Maazimio ya kamati ya jumuiya ya madaktari kuhusu tamko la serikali juu ya mgomo wa madaktari

kwa hiyo mgomo unaendelea?
TAARIFA YA KAMATI YA MUDA YA KUSHUGHULIKIA MADAI YA MADAKTARI KUFUATIA TAMKO LA BUNGE (ILIYOTOLEWA LEO KWENYE VYOMBO VYA HABARI);
Baada ya taarifa ya bunge kuwasilishwa leo ijumaa, kamati ya madaktari inaazimia haya yafuatayo;
• Kamati inalishukuru bunge la jamhuri ya muungano kupitia mwongozo wa spika kwa kuiagiza kamati ya kudumu ya huduma za jamii kuanza kazi mara moja ya kukutana na jumuiya madaktari.
• Kamati pamoja na jumuiya ya madaktari ipo tayari kukutana na kamati ya huduma za jamii.
• Kwa kuwa suala hili ni la umuhimu na dharura kubwa, Mkutano wa jumuiya ya madaktari unatarajiwa kufanyika jumamosi tarehe 04/02/2012 kuanzia saa 4 asubuhi.
• Kamati inasikitika kuwa kauli ya waziri wa afya iliyotolewa bungeni ilijaa upotoshaji mkubwa kwa jamii na wabunge na kwa kuwa busara za naibu spika zilitoa ufafanuzi kuwa kauli hiyo ni ya upande mmoja na wangependa kusikia kutoka kwa madaktari lakini kanuni haziruhusu,kamati imeona kuwa ni muhimu kufafanua baadhi ya masuala yaliyopotoshwa na ambayo hayajatolewa ufafanuzi wowote;
1. Si kweli kuwa huduma zinaendelea kama kawaida katika hospitali tajwa,kwa mfano KCMC taarifa za jana zinaonyesha kuwa hali ilikuwa mbaya sana kiasi cha kusitisha huduma zote kasoro huduma ya magonjwa ya ngozi ,hali hiyo ililazimu Askofu mkuu wa KKKT kufika hospitalini hapo kuwasihi madaktari,jambo ambalo lilishindwa kutatua tatizo. Propaganda za waziri ni msiba mkubwa kwa taifa.
2. Si kweli kuwa madaktari bingwa walikataa kwenda mikoani,taarifa ya kweli ni kuwa taratibu hazikufuatwa kabisa,badala yake kejeli na ubabe ulitumika huku madaktari bingwa wengi kati yao wakihamishwa kupitia magazetini. Mfano upo wa madaktari ambao walienda kuripoti mikoani wakasumbuliwa na kuzungushwa kupewa masurufu ya safari,hospitali ya mkoa ikimuelekeza kuwa jukumu hilo ni la wizara na wakati huo huo wakienda wizarani wanaambiwa jukumu hilo ni la mikoa.
3. Mojawapo ya madai ya madaktari ni suala la uboreshaji wa huduma kwa wagonjwa na mazingira ya kazi, waziri amelikwepa na kupoteza muda wa wananchi kuzungumzia propaganda zisizo na tija.
4. Suala la bima ya afya kwa watumishi wa afya hajatolea tamko lolote.
5. Suala la uwajibishwaji wa watendaji wa wizara ya afya akiwemo yeye, amelikwepa kabisa.
6. Serikali inazungumzia na kutoa ahadi siku zote bungeni kuwa inapeleka watumishi wa afya wilayani na vijijini lakini Mh Waziri akifahamu kuwa dai mojawapo la madaktari ni kuomba serikali iingize posho ya mazingira magumu kwa watumishi wa afya wanaopelekwa maeneo ya mazingira magumu mojawapo ikiwa mikoa ya pembezoni mfano ni Rukwa anapotokea waziri mkuu, hili hajalitolea tamko wala kulizungumzia kabisa.
7. Bw Waziri ametumia muda mrefu kupiga propaganda za mshahara badala ya kusema wao wanatoa ofa gani ili tuelekee kwenye meza ya mazungumzo.

• Mwisho kabisa , jumuiya ya madaktari inaona kuwa serikali haina nia ya dhati kupata ufumbuzi wa mgogoro huu.
 
Acha kuhadaa umma wewe. Mponda ni doctor by profession. Amefanya kazi IHRI na utendaji wake hauna mfano. Fuatilia tafiti zake uone naongelea nini.

Wewe kama huna hakika basi uliza....I know Mponda kwa karibu sana and he has never been in such a class. IHI alikuwa kwenye mradi wa social marketing of vyandarua maarufu kama KINET project....

Unataka data zaidi??

Hapo kwenye blue...kuwa mwanalifu sana ndugu vinginevyo unaweza kuzua matatizo makubwa. Kama hujui kazi zake naomba nikuwekee hapa...

Mponda H - PubMed - NCBI
 
Achana na hawa watu,

Tuliwaeleza toka mwanzo kwamba kwenye hili gogoro serikali inatafuta aibu wakatubishia,

Sasa wanatafuta pa kuficha nyuso zao!!
Mponda amenisikitisha sana.... anadhani wizara ni sawa na IHI alipokua anaajiri wale mabinti na kuwaweka kinyumba na kiofisi!! we mwache tu, time ikifika atawekwa bayana
 
hahahaaaa wameuta 'BWANA Waziri' nadhani ni kujibu madharau ya waziri kumuita Dr Ulimboka 'Bwana' Ulimboka' Good on you doctors!!!. lol!
 
Mwita 25 hujui medical dr ni nani. Amka usingizini phd ya material mngment ndio MD

Huyu mwita hana tofauti na watanzania wengi...mtu hajui kitu halafu anajifanya kujua sana!!

Ndo maana wengine tunaamua kukaa kimya!!
 
Wewe kama huna hakika basi uliza....I know Mponda kwa karibu sana and he has never been in such a class. IHI alikuwa kwenye mradi wa social marketing of vyandarua maarufu kama KINET project....

Unataka data zaidi??

Hapo kwenye blue...kuwa mwanalifu sana ndugu vinginevyo unaweza kuzua matatizo makubwa. Kama hujui kazi zake naomba nikuwekee hapa...

Mponda H - PubMed - NCBI

Teh teh teh.....kuna watu wanapenda kuropoka bila kuwa na ushaidi wa kutosha mkuu,mradi tu nao waonekane wametoa comment hata kama ni pumba,hiv mponda alikua IHRI au ifkara health institute?naona umekamata uongo Mwita 25
 
"sie twatibiwa India Gomeni Tu hilo mtalaumiwa na ndugu zenu na majirani zenu posho hatuwaongezei ng'o pesa tunayowapa ni nyingi sana" by serekali ya Tanzania

Naona umejivika ufilauni wa serikali yenu. Kwamba umekaa tu hata hujui maoni na msimamo wa wananchi ukoji. Hii ndo hasara ya kukaa watu wa kijani tu kila wakati, mnafarîjiana kwamba mambo shwari. Mtakufa kifo kibaya tu.
 
hakuna njia yoyote ya kusuluhisha mgogoro bila mazungumzo.hata rwanda walichinjana na mwisho wake walizungumza ,kenya vilevile.sasa sioni kwa nini serikali inakataa kukaa na madaktari,nadhani kuna jambo kubwa linakuja!
 
Teh teh teh.....kuna watu wanapenda kuropoka bila kuwa na ushaidi wa kutosha mkuu,mradi tu nao waonekane wametoa comment hata kama ni pumba,hiv mponda alikua IHRI au ifkara health institute?naona umekamata uongo Mwita 25

Hiyo sijawahi kuisikia kwa kweli,

Ila watanzania wengi tuna matatizo sana...tunapenda sana mambo ya kurushana kama kwenye taarabu...Ndo maana wengine wanafikia hatua ya kubandika matokeo yao ya kuchechemea kwenye public forum!!

Sie ngoja tunyamaze tu...Hata hivyo akina mwita waache uchokozi!!

Babu DC (1947)!!
 
hahahaaaa wameuta 'BWANA Waziri' nadhani ni kujibu madharau ya waziri kumuita Dr Ulimboka 'Bwana' Ulimboka' Good on you doctors!!!. lol!

bwana waziri ameamua kumcheki bwana ulimboka
 
  • Thanks
Reactions: FJM
hakuna njia yoyote ya kusuluhisha mgogoro bila mazungumzo.hata rwanda walichinjana na mwisho wake walizungumza ,kenya vilevile.sasa sioni kwa nini serikali inakataa kukaa na madaktari,nadhani kuna jambo kubwa linakuja!

Kama kuna jambo kubwa linaloweza kujitokeza ni huu mgomo kusambaa hadi kwenye sectors nyingine...Tatizo ni hawa watu kama Mgaya wa TUCTA ambao wanakomba michango ya wanachama wao wakiwemo madkaria halafu eti wanajidai kuwakana hadharani.

These have to be dealt with after this step!
 
Hiyo sijawahi kuisikia kwa kweli,

Ila watanzania wengi tuna matatizo sana...tunapenda sana mambo ya kurushana kama kwenye taarabu...Ndo maana wengine wanafikia hatua ya kubandika matokeo yao ya kuchechemea kwenye public forum!!

Sie ngoja tunyamaze tu...Hata hivyo akina mwita waache uchokozi!!

Babu DC (1947)!!

Ni kweli mkuu,watanzania wengi tunapenda sana kuropoka na kutaka kuonekana twjua hata kwa yale tusiyoyajua,badala ya kutaka kujifunza toka kwa wenzetu yale tusiyotajua,sisi ni kimbelmbel na kujifanya twajua,ndio maana baadhi wataendelea kubaki na ukilaza wao kwa kutotaka kujifunza....hata hiyo IHRI ndio naisikia kwa mkuu Mwita 25
 
Back
Top Bottom