Maazimio ya kamati ya jumuiya ya madaktari kuhusu tamko la serikali juu ya mgomo wa madaktari

chitage

Member
Mar 3, 2008
41
41
TAARIFA YA KAMATI YA MUDA YA KUSHUGHULIKIA MADAI YA MADAKTARI KUFUATIA TAMKO LA BUNGE (ILIYOTOLEWA LEO KWENYE VYOMBO VYA HABARI);

Baada ya taarifa ya bunge kuwasilishwa leo ijumaa, kamati ya madaktari inaazimia haya yafuatayo;

• Kamati inalishukuru bunge la jamhuri ya muungano kupitia mwongozo wa spika kwa kuiagiza kamati ya kudumu ya huduma za jamii kuanza kazi mara moja ya kukutana na jumuiya madaktari.

• Kamati pamoja na jumuiya ya madaktari ipo tayari kukutana na kamati ya huduma za jamii.

• Kwa kuwa suala hili ni la umuhimu na dharura kubwa, Mkutano wa jumuiya ya madaktari unatarajiwa kufanyika jumamosi tarehe 04/02/2012 kuanzia saa 4 asubuhi.

• Kamati inasikitika kuwa kauli ya waziri wa afya iliyotolewa bungeni ilijaa upotoshaji mkubwa kwa jamii na wabunge na kwa kuwa busara za naibu spika zilitoa ufafanuzi kuwa kauli hiyo ni ya upande mmoja na wangependa kusikia kutoka kwa madaktari lakini kanuni haziruhusu, kamati imeona kuwa ni muhimu kufafanua baadhi ya masuala yaliyopotoshwa na ambayo hayajatolewa ufafanuzi wowote;

1. Si kweli kuwa huduma zinaendelea kama kawaida katika hospitali tajwa,kwa mfano KCMC taarifa za jana zinaonyesha kuwa hali ilikuwa mbaya sana kiasi cha kusitisha huduma zote kasoro huduma ya magonjwa ya ngozi ,hali hiyo ililazimu Askofu mkuu wa KKKT kufika hospitalini hapo kuwasihi madaktari,jambo ambalo lilishindwa kutatua tatizo. Propaganda za waziri ni msiba mkubwa kwa taifa.

2. Si kweli kuwa madaktari bingwa walikataa kwenda mikoani,taarifa ya kweli ni kuwa taratibu hazikufuatwa kabisa,badala yake kejeli na ubabe ulitumika huku madaktari bingwa wengi kati yao wakihamishwa kupitia magazetini. Mfano upo wa madaktari ambao walienda kuripoti mikoani wakasumbuliwa na kuzungushwa kupewa masurufu ya safari,hospitali ya mkoa ikimuelekeza kuwa jukumu hilo ni la wizara na wakati huo huo wakienda wizarani wanaambiwa jukumu hilo ni la mikoa.

3. Mojawapo ya madai ya madaktari ni suala la uboreshaji wa huduma kwa wagonjwa na mazingira ya kazi, waziri amelikwepa na kupoteza muda wa wananchi kuzungumzia propaganda zisizo na tija.

4. Suala la bima ya afya kwa watumishi wa afya hajatolea tamko lolote.

5. Suala la uwajibishwaji wa watendaji wa wizara ya afya akiwemo yeye, amelikwepa kabisa.

6. Serikali inazungumzia na kutoa ahadi siku zote bungeni kuwa inapeleka watumishi wa afya wilayani na vijijini lakini Mh Waziri akifahamu kuwa dai mojawapo la madaktari ni kuomba serikali iingize posho ya mazingira magumu kwa watumishi wa afya wanaopelekwa maeneo ya mazingira magumu mojawapo ikiwa mikoa ya pembezoni mfano ni Rukwa anapotokea waziri mkuu, hili hajalitolea tamko wala kulizungumzia kabisa.

7. Bw Waziri ametumia muda mrefu kupiga propaganda za mshahara badala ya kusema wao wanatoa ofa gani ili tuelekee kwenye meza ya mazungumzo.

• Mwisho kabisa , jumuiya ya madaktari inaona kuwa serikali haina nia ya dhati kupata ufumbuzi wa mgogoro huu.
 
Ni kweli kabisa, hawa jamaa pale wizara ya afya wanahitaji kuwajibishwa kwa huu mgomo.
 
Ni aibu sana kwa professional kama yeye kubadilika ghafla baada ya kuukwaa uwaziri!...Hivi alipokuwa IHI kweli alikuwa ameridhika hivi?
Na hiyo kamati ya kudumu ya huduma za jamii ina guts au meno kiasi gani?..Inaweza kum'summon Waziri na kumhoji kwa huo uwongo wa mchana kweupe aliolidanganya taifa kupitia Bunge letu??
Napenda kujua hayo kwanza!
 
Ni aibu sana kwa professional kama yeye kubadilika ghafla baada ya kuukwaa uwaziri!...Hivi alipokuwa IHI kweli alikuwa ameridhika hivi?
Na hiyo kamati ya kudumu ya huduma za jamii ina guts au meno kiasi gani?..Inaweza kum'summon Waziri na kumhoji kwa huo uwongo wa mchana kweupe aliolidanganya taifa??
Napenda kujua hayo kwanza!

Inaweza
 
Kuhusu Dr. Ulimboka hivi ni kweli si mtumishi wa umma na si daktari? Na kama si mhusika ameingiaje kuwa kinara wa ma dr? Naomba ufafanuzi mwenye ufahamu wa hili.
 
"sie twatibiwa India Gomeni Tu hilo mtalaumiwa na ndugu zenu na majirani zenu posho hatuwaongezei ng'o pesa tunayowapa ni nyingi sana" by serekali ya Tanzania
 
Kuhusu Dr. Ulimboka hivi ni kweli si mtumishi wa umma na si daktari? Na kama si mhusika ameingiaje kuwa kinara wa ma dr? Naomba ufafanuzi mwenye ufahamu wa hili.

achana na Pinda kachanganyikiwa huyo..hivi wewe unamfuatisha pinda na maneno yake ya kilabuni..
 
Kamati ya Bunge sikilizeni kilio hiki. kinwahusu wazazi wenu na ndugu zenu tuliopo huku vijijini jamani.
 
Nchi yetu haitawaliki tena kutokana na Uongozi mbovu. Ukisoma kwa makini madai ya madaktari utajua makosa yako ktk muundo mzima wa AFYA nchini lakini nina hakika wananchi hawako tayari kukubali ukweli kama wanavyomshabikia Lowassa arudi madarakani. Bunge linaloshindwa kuwaita viongozi wahusika wa mgomo huu bungeni kujibu ama kutafuta suluhu kwa sababu ya kanuni ambazo hazikutegemea dharura kama hii ni mfano mzuri sana kuonyesha kwamba Katiba nzima ya Tanzania inatakiwa kutazamwa Upya...

Pengine nikubali kwamba huu mgomo wa madaktari unaweza kuwa mwanzo wa anguko la CCM lakini kama kweli wamekubali kukutana na kamati ya Bunge ili wapate kuongezewa posho, bima na kadhalika wakati wananchi na watumishi wengi nchini hawana posho wala bima hizi ni mwanzo wa kuivuruga nchi kwenda bila dira, sera na ilani...

Nitarudia kusema kama daktari haridhiki na kazi au mazingira ya kazi alo ajiriwa anatakiwa kuandika barua ya kuacha kazi na atafute sehemu nyingine..Lakini hili haliwezekani kutokana na kwamba vitengo vyote vya Afya nchini vinalindwa na mfumo mmoja ambao ndio tatizo kubwa. Isipokuwa kama lilivyo swala la waziri mkuu mstaafu Lowassa, wananchi wameamua kulifumbia macho na kama kawaida yetu kutafuta mchawi mwingine hali mchawi tunaye na tunakula naye meza moja.
 
Na nyie msituchoshe! Kama vipi jifukuzisheni kazi kabisa ili tujue hatuna madaktari. Sitaki nataka kibaooooooooo!
Wewe jisemee nafsi yako acha kutujumuisha. Mimi nawaunga mkono madaktari na nawapongeza kwa kutoa taarifa na ufafanuzi muafaka wa upotoshaji wa mshenzi mwenzio Mponda.
 
Maamuzi mazuri,kazeni buti kitaeleweka tu, jaribu kuacha space between paragraphs ili kurahisisha usomaji Bw Chitage.
 
Ni aibu sana kwa professional kama yeye kubadilika ghafla baada ya kuukwaa uwaziri!...Hivi alipokuwa IHI kweli alikuwa ameridhika hivi?
Na hiyo kamati ya kudumu ya huduma za jamii ina guts au meno kiasi gani?..Inaweza kum'summon Waziri na kumhoji kwa huo uwongo wa mchana kweupe aliolidanganya taifa kupitia Bunge letu??
Napenda kujua hayo kwanza!

Kwa taarifa yako, IHI imekua kutokana na yeye kuwa hewala baba, na kupisha wenye pesa wafanye wanachotaka, he has never been efficient, important, present whatsoever, he was a rubber stamp
 
Ni aibu sana kwa professional kama yeye kubadilika ghafla baada ya kuukwaa uwaziri!...Hivi alipokuwa IHI kweli alikuwa ameridhika hivi?
Na hiyo kamati ya kudumu ya huduma za jamii ina guts au meno kiasi gani?..Inaweza kum'summon Waziri na kumhoji kwa huo uwongo wa mchana kweupe aliolidanganya taifa kupitia Bunge letu??
Napenda kujua hayo kwanza!

Waziri siyo Medical doctor bali ni PhD holder....I am sure he ameanza kuifahamu profession baada ya kuwa waziri

Kamati za kudumu za Bunge zina mamlaka ya kumwita Waziri na watendaji wake wote na kuwahiji. Kama hawaridhiki na majibu yao, wanaweza kupeleka taarifa na mapendekezo yao bungeni!!
 
Acha kuhadaa umma wewe. Mponda ni doctor by profession. Amefanya kazi IHRI na utendaji wake hauna mfano. Fuatilia tafiti zake uone naongelea nini.
 
jitahidi usichoke na wewe..... ila ikiuma sema

Achana na hawa watu,

Tuliwaeleza toka mwanzo kwamba kwenye hili gogoro serikali inatafuta aibu wakatubishia,

Sasa wanatafuta pa kuficha nyuso zao!!
 
naipenda hii kamati ya madaktari kwa sababu haina papara wala kigeugeu.kamati imesimama.change is coming.
 
Na nyie msituchoshe! Kama vipi jifukuzisheni kazi kabisa ili tujue hatuna madaktari. Sitaki nataka kibaooooooooo!

Mkuu haujalazimishwa kuchngia kwenye thead hii kama uliona hauna hoja ya kuchangia
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom