Maaskofu

Beria

Member
Nov 4, 2010
5
1
Maaskofu wanapotoa maoni kwanini tusiyachukulie kwamba ni maoni ya watanzania wenzetu? Kwanini tukimbilie udini wakati hoja ya msingi ipo mezani?
 
Karibu sana Beria Jamvini!!
Kweli kabisa maaskofu nao ni Watanzania wana haki kukosoa pale wanapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo kama raia wengine. Mbona walipoambiwa mgombea wao ni chaguo la mungu kipindi kile hawakusema ni udini, leo wanakosolewa wanakimbilia udini..........hawa jamaa vipi!!
 
Moja kati ya shutuma juu ya kanisa katoliki kuhusika na mauaji ya kimbari kule Rwanda ni kukaa kimya na kutokuwa proactive wakati dalili za machafuko zilipokuwa dhahiri kabisa! Halikadhalika "role" iliyochezwa na kanisa hilo wakati wa ukoloni wa kupendelea wa-tutsi then wahutu. Sasa hapa tunataka wakae kimya...

Kwa maoni yangu viongozi wa dini wakiwamo masheikh wanayo haki kabisa kutoa misimamo yao juu ya mwenendo wa nchi, kudhani kwamba wao ni "apolitical" eti hawahusiani na siasa si sahihi kabisa!
 
ndiyo maana wanasema watanzania hatupendi kufikiri. Laiti tungeliangalia wazo lililotolewa (ikifuatiwa na lini, kwapi, kwa nini, nk) alafu tuangalie nani. Hapo angalau matatizo yetu yangekuwa yamepungua hata kwa asilimia fulani
 
Back
Top Bottom