Maaskofu wamshambulia Kikwete

nimechokaaaa na matamkoo, hadi miaka 100 ya uhuru itafka still tupo kwenye matamko more action are needed pliz Tanzanians.
 
si walisemaga hapo awali kwamba ameteuliwa na Mungu ?Imekuwaje tena?

Kateuliwa na mafisadi ndani ya Magamba, angekuwa kateuliwa na Mungu angeshavisikia vilio vya Watanzania miaka mingi iliyopita.
 
mie nangojea tamko la bakwata nione litakuwa na mlengo wa kidini au kutetea maslahi ya taifa, tusubiri

Mkuu BAKWATA ni kitengo cha propaganda cha CCM, hivyo na wao wana sehemu yao katika hayo malipo ya Dowans.
 
mie nangojea tamko la bakwata nione litakuwa na mlengo wa kidini au kutetea maslahi ya taifa, tusubiri

tatizo la bakwata ni kotokuwa wabunifu wa hoja utaona kila siku wanajibu tu hoja za watu, kazi kutoa matamko ni lini wao wataanzisha hoja na watu wakafata, unakumbuka kabla ya uchaguzi kuhusu walaka wa rc nao wakatengeneza wao kwa hiyo kanisa ni perce seter wenyewe wanafata, kitu kingine ni watu ambao wamekuwa wakitumiwa nyerere aliwatumia,
 
Wale hata siku moja hawatatoa kauli yoyote ya kumpinga Kikwete ukiondoa ile issue ya mahakama ya Kadhi. Yaani utadhani kama nchi kwenda mrama hakuwagusi kabisa wao. Nimejaribu kutafuta kama Bakwata wameshatoa tamko lolote lile la kupinga malipo ya Dowans lakini sikuambua kitu, labda siku za usoni nao watafanya hivyo.

Kwani kwenye kupinga Dowans kutakuwa na pilau?kama hamna msitegemee kusikia lolote kutoka kwa hawa jamaa.
 
Na hilo ndilo tamko la BAKWATA.
Dugu ficha upumbavu wako.
Hapa Bakwata inaingia vp?
Yeyote anayepinga malipo hayo kwa kupaza tu sauti ni mtafuta cheap popularity. Hukumu ya kisheria huwa challenged kwene court of law na si kwenginewe au kwene majukwaa yasohusika.

Commonsense 101
 
Kwani kwenye kupinga Dowans kutakuwa na pilau?kama hamna msitegemee kusikia lolote kutoka kwa hawa jamaa.

Mhhhh!...labda liandaliwe pilau la nguvu ili nao waweze kuunga mkono haya mapambano ya kupinga malipo fisadi dhidi ya Dowans. Inasikitisha sana kwamba malipo haya ambayo yalikuwa yafanyike tangu mapema mwaka huu (kama sikosei January 2011) na taasisi mbali mbali nchini wakiwemo Watanzania wa ndani na nje ya nchi kusimama kidete kupinga malipo hayo fisadi, Bakwata bado haijaona umuhimu wa kufanya hivyo.
 
hata wakipinga watataka alipe mwakyemb,6 n.k kwasbb wao ndio waliotoa ushauri mbaya wa chuki.
 
• wamuonya asiilipe dowans kwa vile alishaikana

na danson kaijage, dodoma
tanzania daima


maaskofu wa kanisa la
christian mission fellowship (cmf), wamesema kitendo cha rais jakaya kikwete, kuendelea kuwakumbatia watuhumiwa wa ufisadi ndani ya serikali yake kinazidi kuwaangamiza watanzania kwa umaskini.

Mbali na lawama hizo, pia wamesema kuwa kanisa hilo litaungana na wanaharakati wa kweli na wapenda maendeleo nchini ili kuhakikisha wanaipinga serikali kulipa deni la dowans la sh bilioni 94.

Maaskofu hao, walitoa kauli hizo jana mjini hapa wakati wa ibada maalumu ya kumsimika makamu askofu mkuu wa kanisa hilo nchini, askofu dorlinad mhango, iliyoongozwa na askofu mkuu wa cmf, dk. Mungulu kilimba.

Kauli hiyo inakuja siku chache tangu mahakama kuu kanda ya dar es salaam, isajili tuzo ya dowans iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara (icc), ikilitaka shirika la ugavi wa umeme nchini (tanesco), kulipa fidia hiyo kutokana na kosa la kuvunja mkataba baina yake ya kampuni ya dowans tanzania.

Askofu kilimba alisema kuwa inashangaza kuona serikali inaridhia kulipa deni hilo haraka wakati haina fedha za kuendeshea shughuli mhimu za kimaendeleo za kumkomboa mtanzania anayeishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku.

Alibainisha kuwa kanisa hilo, kamwe halitanyamazia kitendo hicho na hivyo lazima waungane na wanaharakati nchini kuhakikisha wanapinga ulipwaji wa fedha hizo licha ya icc kutoa hukumu ya kuitaka tanesco kulipa fidia hiyo.

"kamwe viongozi wa dini hatuwezi kunyamaza juu ya hili, kwani tunajiuliza kuna nini hadi serikali iridhie haraka kulipwa kwa fedha hizo wakati kuna matatizo mengi ambayo yanatakiwa kutatuliwa," alihoji askofu huyo na kuongeza:

"watanzania wangapi wanaishi chini ya dola moja kwa siku na hawajui hatma ya maisha yao, hawana umeme, huduma za afya ni mbovu halafu inakuwaje serikali iwe tayari kulipa deni la dowans upesi na kuacha kushughulikia matatizo mengine muhimu? Sisi kama kanisa hapa hatuwezi kunyamaza."

aliitaka serikali kuueleza umma wazi wazi ni wapi fedha hizo za kuilipa dowans zinatoka na zinalipwa kwa nani ikiwa viongozi wote wa juu akiwemo rais jakaya kikwete, walikiri kuwa hawawajui wamiliki wa kampuni hiyo.

"jamani ndugu zangu lazima tujiulize kuna nini kati ya serikali na dowans? Wazee wa jumuiya ya afrika mashariki hadi leo wanaandamana hadi kulala barabarani hawajalipwa madeni yao, lakini leo hii serikali inaharakisha kulipa deni la dowans, hii haiwezi kukubalika kirahisi na ni haki yetu kuhoji na kuungana na wanaharakati wa kweli wapenda maendeleo kupinga malipo hayo," alisisitiza askofu huyo.

katika hatua nyingine, askofu kilimba aliwataka watumishi wa kanisa hilo kuhakikisha wanasema ukweli juu ya mambo yanayokwenda kinyume na matarajio ya nchi hasa suala la rushwa, ufisadi na viongozi wa serikali kujilimbikizia mali wakati watanzania wengi wanakufa kwa umaskini.

"viongozi wa dini ni lazima kuikosoa serikali bila woga kwani sisi ndiyo kazi kubwa tunayotakiwa kuifanya, sasa angalia viongozi wa serikali wanavyojichukulia mali pamoja na kuingia mikataba mibovu na kulisababishia taifa janga kubwa la umaskini na madeni. Lazima tupige kelele kwa ajili ya kufanya mabadiliko," alisisitiza askofu kilimba.

Kwa upande wake, makamu mpya wa askofu mkuu, mhango, alisema kuwa kinachosababisha umaskini nchini ni rais kikwete kutokuwa na maamuzi kwa viongozi aliowachagua.

Askofu mhango alisema rais kikwete ameshindwa kuwa na maamuzi magumu ya kuwawajibisha watendaji wazembe na wale ambao si waaminifu na badala yake amekuwa kinara wa kuwakumbatia.

"wapo watumishi wengi ambao amewateua kushika nyadhifa mbalimbali ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi lakini rais amewakumbatia anashindwa kutoa maamuzi magumu kwa lengo la kunusuru nchi katika janga la umaskini uliopindukia.

"kuna jamaa zake wengi ambao wanatuhumiwa kwa rushwa lakini amewakumbatia. Pamoja na kutoa misemo ya kujivua gamba lakini hizo ni porojo tu wakati watanzania wakizidi kuangamia," alisema mhango.

Askofu mhango alisema kwa nafasi yake, atahakikisha anazungumza na serikali kwa kuitaka ijenge viwanda vikubwa na vidogo ambavyo ni vya ndani ili kuepukana na taifa kugeuzwa dampo la kutupa takataka kutoka nje ya nchi.


kanisa hili linapatikana wapi?
 
Walipe kodi tulipe dowans hawana lolote matamko gani unafk wangetoa matamko na ufsad wa mkapa,lowasa kwanza ndo tuwaunge mkono
 
ni vizuri kama viongozi wa dini pia kutoa maoni yao kwa mambo yanayohusu maslahi ya umma kuliko kukaa kimya tu,ila nna wasiwasi na hii bakwata..
 
Back
Top Bottom