Lu-ma-ga
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 4,780
- 3,227
Walipaswa sana kuacha ushabiki wa kisiasa tangu mwanzo wa regime hii, walipaswa wawe marefa kwa uongozi uloingia madarakani na wananchi kwa kushirikiana na wazee wenzao ndani ya chama kinachotawala(hapa wangelimsaidia mzee mwinyi na kawawa kuirejesha ccm ktk mstari baada ya minyukano ya ndani ya ccm kumpata kikwete, walilisahau hili wote kama maaskofu, wasisi wa chama na kuwaacha mtandao wakiendelea huku walioshindwa na mtandao wakiugulia pasipokujua wapi wakililie au kupata faraja... Haya tuyaonayo ni matokeo ya uzembe wa maaskofu wetu, na wazee aliowaachia kambarage jahazi la ccm kukubali kuegemea na kuacha utamaduni wa kukosoana na kuridhiana ndani ya chama na kuiweka nchi mbele....), maaskofu kama mngeifanya hii kazi vizuri sidhani kama mkuu angelithubutu kuwakoga hadharani....., sasa anapaswa na yeye aseme maana anahisi kuwa aliachiwa mzigo wa kujiponya peke yake ndani ya chama....au anawaona ni chanzo cha matatizo yake..., tafakarini ili muijenge nchi na siyo mtu. Kidumu chama cha mapinduzi
Mimi nimeipenda sana sinema aliyoicheza JK huko Mbinga mbele ya wahasham Maaskofu wakuu, Maaskofu, mapadre, Masista, balaza la walei na waumini kwa ujumla.Haya mambo yamekuwa yakitukera sana sisi waumini, kwani viongozi wetu wameendelea kujishusha na kupunguza hadhi yao mbele ya serikali. Cha kushangaza leo ni kwamba; CCT, na TEC ya leo si ile ya enzi ya utawala wa nyerere na Mwinyi, enzi hizo walikuwa na authority kweli, lakini wamejikuta wakiingizwa mkenge kwa kuwa karibu na watawala kisiasa japo wamekuwa wakifanya kimaficho lakini sisi waumini tunajua na tunaona.Hili ni fundisho kuwa viongozi wa dini wabaki kambini ili siku wanapotoka na hoja mara moja jamii ielewe na kuheshimu.Lakini aliyosema JK jamii inaweza leo kushawishika kukubali hata kama itakuwa uongo kwani wamejenga mazoea ya kuchanganya mambo.