Maandishi ya Lugha ya Kiingereza Kwene Fulana zetu

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,489
86,005
Hua nina tabia ya kupenda kusoma soma sana hasa maandishi ya kwene fulana; nilishawahi kukutana na maandishi ambayo mengi ni matusi au hayana maana kwa mvaaji; Mfano ninayoweza kuyakumbuka fasta fasta hapa ni pamoja na haya hapa;

* I bleed Green (imevaliwa na kijana wa Kiume)
* Do Me Please halafu nyuma ikaandikwa Do me Again Please ( Imevaliwa na kijana wa Kiume)
* Leave me a message, I am out of my mind
* Give a man a fish, he will lie for a day, teach him to fish and he will lie for a life time
Na nyingine nyingi tu, sasa point yangu ni kuwa, je hakuna namna ambayo tungeweza kuwasaidia ndugu zetu wasivae vitu ambavyo kwa mazingira yetu vinaleta maana inayokanganya? Waweza kuweka maandishi mengine unayokumbuka pia
 
Mimi ninayo T-shirt safii sana rangi nyekundu halafu ina maandishi kwa rangi mbali mbali "I LOVE SCHOOL BOYS", nikivaaga familia nzima kelele, "haifai vua vua", njiani kila mtu anasoma kifua changu halafu ananipiga jicho la kulikoni? I like it!
 
Ndio mambo ya kutojua lugha. Muone huyu Mchina.

fck-it-12.jpg
 
Back
Top Bottom