Maandazi yanawamaliza Tembo Tanzania!

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
7,312
6,770
Jamani sjui niseme ni ubunifu au uharibifu!?

Imeibuka mbinu mpya inayotumiwa na majangili kuwaua tembo, na hii mbinu inatumika sana katika pori la hifadhi ya selous...

Yanachukuliwa maandazi ya kutosha, kisha yanachomwa sindano ya sumu(kwa usalama naomba nisiitaje aina hiyo ya sumu)

Basi, jangili huenda na maandazi hayo hadi porini na kutegesha njia ambayo anajua kabisa tembo watakuja...

Kwa ugunduzi wao wa kijangili,..tembo wanapenda sana maandazi! Basi tembo wanapofika eneo hilo lenye maandazi hufakamia....na baada ya muda mfupi hufa! Jamaa wanakuja na kung,oa meno na kuondoka zao.

Mbinu hii inawasumbua sana askari wetu wa maliasili kwani walizoea kusikiliza milio ya risasi ili kujua mahahali fulani kuna majangili.

Hii mbinu ni mbaya sana kwani huua hata tembo wadogo wasio na meno.

Tutunze maliasili zetu jamani, ubunifu wa uharibifu si jambo jema.

Wenzetu wa kenya huwatupia tembo nusu kaputi, tembo akilala wanakata pembe kwa msumeno baabae tembo anaamka na kuendelea na maisha- elephant with no ivory. Hii ya selou ni chiboko.

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom