Maandamano ya UKUTA yasipofanyika...

Kuna Mji umekuwa ukituhumiwa mara nyingi kwamba wao hawaruhusu maandamano kabisa, sijui kwanini. Mji huo unaotuhumiwa ni Moshi ulioko kule Mkoani Kilimanjaro. Nimetumia neno kutuhumiwa kwakuwa haijathibitishwa.
 
Kama UKUTA wakinywea na mwishowe kutokufanya hayo maandamano yao ambayo wamepanga kuyafanya hiyo tarehe 1 mwezi ujao, basi mheshimiwa MWENYE ENZI, MTUKUFU rais Magufuli atakuwa amepata ushindi mkubwa sana.

Hayo maandamano yasipotokea atakuwa kafanikiwa kuwatisha wananchi katika kutofanya yale ambayo hayampendezi yeye.

Na huu ndo utakuwa mwanzo tu. Huko mbeleni ikitokea kuna jambo ambalo halimpendezi yeye binafsi basi hatosita kutumia vyombo vya dola kuwatisha watu ili waache kufanya walichokuwa wamepanga kufanya.

Hiyo ndo Tanzania mpya. Tanzania ya MWENYE ENZI, Mtukufu rais John Pombe Joseph Magufuli [nahisi pia tutalazimishwa kuyatumia majina yake yote manne la sivyo wataokiuka watatafutwa na kuadhibiwa, hata kama wapo mitandaoni].

Na nyie wachora vikatuni nahisi dawa yenu inakorogwa huko maabara. Kama mkiendelea kumchora vibaya MWENYE ENZI, MTUKUFU rais John Pombe Joseph Magufuli basi siku zenu zinahesabika.

Yakiwatokea ya kutokea msije lalama eti sikuwaambia! Shauri yenu.
Miafrika Ndivyo Tulivyo.
 
CHADEMA CHAMA KIMOJA ILA NGUVU YAKE SIO MCHEZO MAANA CCM wameaanza kutumia vikundi mbadala kujumuika navyo ili kupinga Operation UKUTA. Steve Nyerere bado anasaka uteule kutoka kwa magufuli wamekuja na Zoezi La kupinga UKUTA kwa jina la WASANII Tanzania.Halkadhalika nao UWASATA huu ni umoja wa wanawake wanasiasa tanzania.UKUTA umezidi kuonesha uimara wake na umaarufu wake nchi nzima kwa mfano ukiniuliza mimi kati ya Neno UKUTA na jina la Mkuu wa nchi lipi nimelisikia mara nyingi zaidi kwa mwezi huu? Nitajibu nimesikia UKUTA kwa 70% kwa kuwa Mkuu huyo amepiga kimya kwa muda sasa na kuacha UKUTA ukichukua nafasi yake katika social nets na vyombo mbalimbali vya Dola.
Policcm wametaja neno UKUTA kuliko jina la mkuu wa nchi kwa mwezi huu.
Mpaka sasa UKUTA umefanikiwa kwa 59.8 kwa Nchi nzima.
#NikoTayariKwaUKUTA sep 1.
 
Mandamano hayafanyiki na wachora katuni wataendelea kuchora!

Hizi kelele sio mpya na haziwezi kumalizika mpaka pale wapiga kelele watakapo tembea katika maneno yao kwa sababu vyama vinavyopiga kelele kuhusu demokrasia havina hata misingi ya demokrasia ndani ya vyama vyao.

CHADEMA wamechukua jukumu kubwa ambalo kwa sasa liko juu ya uwezo wao kama chama.

“...Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country. I never went to a country, saw many parties and assumed that it is democratic. You cannot define democracy purely in terms of multi-partist parties...”-Mwl. Nyerere.

Tanzania is unique country!

Jamani hili sio la chama, uhuru wa kukusanyika ni wetu sote hata ikiwa ni washabiki wa mpira na uhuru wa kuandamana ni wetu sote hata ikiwa ni wafanyakazi
 
Back
Top Bottom