Maandamano ya TUCTA Januari 29

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
SHIRIKISHO la vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limeeleza kuwa watafanya maandamano ya amani Januari 29 mwaka huu kwa lengo la kupinga bei ya umeme na kuunga mkono mabadiliko ya Katiba mpya.

Hayo yalisema jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya, amabaye alidai uamuzi huo ulifikiwa Alhamisi wiki hii katika kikao cha kamati ya utendaji ya shirikisho hilo.

Alisema maandamano hayo yatafanyika nchi nzima ambapo kamati ya utendaji ya shirikisho hilo imeazimia kupinga hatua ya serikali kupandisha bei ya umeme huku kiwango cha mishahara kwa wafanyakzi kikibaki kile kile.

“Maandamano yetu ya amani yatafanyika nchi nzima kupinga serikali kupandisha gharama ya umeme huku mishahara ya watumishi ikibaki bila kuongezwa chochote, hatua ambayo inaonyesha kutaka kumnyonya mfanyakazi ambapo si haki,” alisema Mgaya.

Alisema ili nchi yoyote iweze kupata maendeleo ya kasi ni lazima mazingira ya kazi ya wafanyakazi wake yaboreshwe na kuwa na nyongeza ya mishahara.

Mgaya alisema kwa sasa wameunda kamati maalumu itakayokuwa chini yake ili kuweza kurartibu taratibu za kisheria ikiwamo kuandika barua kwa Jeshi la Polisi na kupata baraka za kufanya maandamano hayo ya amani.
 
Go gooo goo mgaya go najuaa JK anakuhofiaa sanaa maana ww pia chanzoo kupokaa kura zake nyingi sanaa toka kwa wafanyakazi ila jihadharii sana kula kulaa hovyo....wataku poison ...hatari sana hawa mafisadiii wanyonge tuko nyuma yako
 
Mi sina imani na hawa TUCTA kwani hii strategy ya kupinga ongezeko la bei ya umeme siiafiki hata kidogo,haiwezi kumshitua jk...dawa ilikuwa ni mgomo nchi nzima baasi!maandamano ni usanii tu.
 
TUCTA, kale ka-mdudu kasikokuwa na wenyewe duniani, DOWANS TANZANIA LIMITED, ndio hiyo inalipwa tupende tusipende.
 
sahii haiwezekani serikali ibaliki ongezeko la bei ya umeme wakati msharaha upo costant.
Katika hilo pamoja sanaaaaaaaaaa
 
SHIRIKISHO la vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), limeeleza kuwa watafanya maandamano ya amani Januari 29 mwaka huu kwa lengo la kupinga bei ya umeme na kuunga mkono mabadiliko ya Katiba mpya.

Hayo yalisema jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya, amabaye alidai uamuzi huo ulifikiwa Alhamisi wiki hii katika kikao cha kamati ya utendaji ya shirikisho hilo.

Alisema maandamano hayo yatafanyika nchi nzima ambapo kamati ya utendaji ya shirikisho hilo imeazimia kupinga hatua ya serikali kupandisha bei ya umeme huku kiwango cha mishahara kwa wafanyakzi kikibaki kile kile.

"Maandamano yetu ya amani yatafanyika nchi nzima kupinga serikali kupandisha gharama ya umeme huku mishahara ya watumishi ikibaki bila kuongezwa chochote, hatua ambayo inaonyesha kutaka kumnyonya mfanyakazi ambapo si haki," alisema Mgaya.

Alisema ili nchi yoyote iweze kupata maendeleo ya kasi ni lazima mazingira ya kazi ya wafanyakazi wake yaboreshwe na kuwa na nyongeza ya mishahara.

Mgaya alisema kwa sasa wameunda kamati maalumu itakayokuwa chini yake ili kuweza kurartibu taratibu za kisheria ikiwamo kuandika barua kwa Jeshi la Polisi na kupata baraka za kufanya maandamano hayo ya amani.

Naomba mwenye tetesi kuhusu maandalizi ya maandamano hayo yanaendeleaje atujulishe
 
NA wewe Mgaya usituzingue kila siku mgomo hakuna ,sasa umegeukia maandamano kama mwanaume simama sawasawa twende kazini
 
Kwa kweli hatuwaeli kabisa TUCTA licha ya ukweli kwamba Dowans ndio hiyo inakaribia kufyonza nafasi za ajira kibao, gharama ya uzalishaji kupanda na watu kupunguzwa kazini.
 
Kuna watanzania wananyima usingizi kikwete wa kwanza Dr Slaa, wa pili Mgaya. Go go go Mgaya tuko pamoja
 
Huyu mgaya naye hana jipya akishapewa mlungula anatulia kimya,,,,mi nawapa tano wafanyakazi wa reli wakiamua kitu wameamua, watu wa kuigwa kimsimamo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom