Maandamano ya kupinga Wamarekani kuishambulia Libya (Picha)

Kina Nani haoo? Wakamateniiiii...

Yaani watu tunaandamana kuipinga serikali ya Tanzania, wao wanaandamana kuipinga Marekani!!!
...sijaona mtu anaeandamana kuipinga serikali ya Tanzania.. sijaona!

Watu wanaandamana hapa kwetu kwa ajili ya watu!
Wengi wa waandamanaji ukiwauliza kwanini mnaandamana huwa hawajui!
Akili za kitanzania duh!

Mungu wasamehe kwa sababu hawajui watendalo, maskniii yani ukiwaangalia ukawapiga sachi mfukoni hakuna hakuna hata mwenye buku 10

Yaani wewe dada unaamini maisha ni buku 10. Maisha si pesa bali ni utu, kutofautiana kwa itikadi na imani si sababu ya kukejeli wengine. Jipigie mfano kwenye familia na jamaa zetu wote mna buku 10, au ni kuandika na wengine waone umeandika?
Kuna haja tena kubwa saana ya kujitahidi kuwaaminisha wananchi CDM haifungamani na dini yoyote, maana ili watu wajadili hoja wanaangalia ni nani kaitoa na si hoja yenyewe.

Huu ni unafiki wa hali ya juu, hatuwezi tukaendelea kwa hali hii. January waTZ walipigwa risasi kwenye maandamano halali kule Arusha hawaandamani leo libya walibya wanataka kumtoa dicteta wao eta TZ kuna watu wanaandamana. Waambieni watoe uwendawazimu.

Tuendelee na kazi ya kuikomboa TZ

Huu ni unafiki wa hali ya juu, hatuwezi tukaendelea kwa hali hii. January waTZ walipigwa risasi kwenye maandamano halali kule Arusha hawaandamani leo libya walibya wanataka kumtoa dicteta wao eta TZ kuna watu wanaandamana. Waambieni watoe uwendawazimu.

Tuendelee na kazi ya kuikomboa TZ

acha blah blah hapa unasahau haraka sana. Unakumbuka Arusha tu enh! Vipi Pemba na mwembechai waliuwawa wangapi? Nani aliandamana? Si walionekana wahuni?

Nchi hii kila Mtanzania angependa mabadiliko. Tena kwa spidi ya haraka saana si km ya sasa. Lakini tatizo nani anayeaminika kuwa anamalengo ya kuwakomboa Watanzania wote na si wachache? cDM wameingia kwenye mtego na wamenasa na watauona mwisho wao. Waliambiwa chama cha kidini wakakanusha na kweli huenda si hivyo. Lakini wafuasi wanaamini hivyo kupitia kauli zao. Ukisoma thread hii utaona wafuasi wa CDM kwao matusi halali ni kwa waislam. Ohh hawajasoma oh mara wendawazimu nk. Kumbukeni hizo kura mnazoziita za ukombozi hazitapigwa na cdm peke yake.
Bila kuonyesha na kuonekana kuwa chama ni cha watanzania wote hata waandame kila pembe, mabadiliko hayawezekana. Km wafuasi hawatajifunza kuheshimu wengine chaguzi zote zitakuwa ni km kombolela. Atafutwe nani itakuwa inategemea na dini ya mtafutwa na mtafutaji. Hoja hapa jamvini zinajengwa kwa kuangalia imani na si uhalali, hilo mpaka kwa viongozi wa dini na watawala pia.

acha blah blah hapa unasahau haraka sana. Unakumbuka Arusha tu enh! Vipi Pemba na mwembechai waliuwawa wangapi? Nani aliandamana? Si walionekana wahuni?

Tunazungumzia TZ ya Mwaka 2010 na 2015, ulikwpo kwenye maandamano ya jana nini?, Kikubwa hapa waTZ tusiwe kiherehere wa mambo ya wenzetu. tuangalie mambo ya waTZ, Umenikumbusha vizuri nilichukia sana kwa vurugu zile za pemba.

Tunazungumzia TZ ya Mwaka 2010 na 2015, ulikwpo kwenye maandamano ya jana nini?, Kikubwa hapa waTZ tusiwe kiherehere wa mambo ya wenzetu. tuangalie mambo ya waTZ, Umenikumbusha vizuri nilichukia sana kwa vurugu zile za pemba.

Ha ha ha ha yaani roho zilizopotea zina umuhim zaidi za hivi karibuni kuliko wakati ule. Huwezi ukawa unadai reaction ya wenzako lkn ya kwao huyazungumzi. Kuzungumzia kitu si lazima kuwepo, haki ya kuandamana ni haki ya kikatiba. Kwahiyo waandamanaji wana haki yao kwa kile wanachoamini na si lazima jamvi zima likubaliane nalo. Watu wanapiga kelele hawana hata hizo facts. Nchini Uingereza wananchi wengi kwa mujibu wa poll iliyoendeshwa wanapinga uvamizi huo. Vivyohivyo Marekani na Ufaransa. Hujiulizi kwanini Obama anaondoka mapema? Msikilize kwenye hotuba yake jumatatu jioni utaelewa! The logic is very simple, akiendelea na vita vile uwezekano wa kushinda uchaguzi next yr ni mdogo. Yapo maswali mengi tu! Sasa hivi inakadiriwa kuwa Ivory Coast tokea November last year wametoa wakimbizi mil 1, kuna mtu kang'angania madarakani huku ameshindwa uchaguzi kwa figures na si speculations, mbona hawamtoi? Walichokuwa wanafanya Bahrain kina tofauti gani na Libya? Au kwa sababu ya American base na possible threat from iran, the civialians are deserving the sufferings?

Hee, hapa napo pamegeuka uwanja wetu!! Tujadili jinsi ya kuingia ikulu, duh sisi ni wakare...

Ni na uhakika hawa watu watakuwa wametumwa na IKULU kwa sababu juzijuzi tuu kulikuwa na ujumbe umeletwa kutoka Libya na mwakilishi kwa Raisi J.KIkwete kwa jinsi anavyojinasibu na mambo ya udini kwa sasa hivi nadhani anaweza kuwawasilisha hoja kwa maashura na ndio maana Mufti alikwenda huko na kwenda kusisitiza umoja wa waislamu haya mambo yanatakiwa kuangaliwa kwa undani sana kuna kitu cha chini kwa chini kinapikwa kwa baraka za Ikulu zitakazo kuja kupelekea nchi yetu kubaya sana

Nilimsikia jana Kamanda Kova akisema hapata kuwepo maandamano yatakayongozwa na shura ya Maimamu ila walikubaliwa na kufanya mkutano na jeshi la polisi lilisema lingeulinda mkutano wao.

Ukiangalia hicho kinachoitwa shura ya maimamu kimejaa watu mbumbu kuliko maelezo.Hawajui kwamba jumuiya ya nchi za kiarabu tena zenye waIslamu wengi na uchumi Imara kuliko Tanzania zilishamchoka Gaddaf na uongozi wake wa miongo minne.Hawajui raia wa Libya waliingia mitaani kupinga utawala wa Gaddaf na serekali yake.Hawajui kwamba ndani ya muungano wa nchi zinazoipiga Libya zimo baadhi ya nchi za Kiarabu zilizotoa vifaa na fedha ili kumdhibiti Gaddaf.Hawajui kwamba wananchi wa nchi nyingi za kiarabu wamechoka na tawala zisizozingatia demokrasia si Libya tu nchi kama Misri,Tunisia,Baharin na sasa Syria upepo wa mabadiliko umevuma si maandamano ya Shura ya Maimamu wala upuuzi wa baadhi ya watanzania utakaozuia mabadiliko.

Taasisi kama hizi unategemea zitawaletea maendeleo waislam wa Tanzania ?.Jibu ni moja tu kamwe hakuna maendeleo eg shule,hospitals,vyuo vikuu na nk.Jaribu kufanya utafiti wa juu juu utakuta Shura ya maimam hawana shughuli zozote zaidi ya kuteka misikiti na nyumba zilizowekwa wakfu na waIslamu kwa faida ya matumbo ya viongozi.Kazi nyingine kubwa ni kutumiwa na wanasiasa uchwara muflisi kwa faida za kisiasa.

NDIO TUTEGEMEE MWENYE AKILI ATOKE KWENYE HIYO SOCIETY ATUONGOZEE NCH!! KAZI IPO TANZANIA!!

How many Black Africans have been massacred? Hatujasikia hata wakilaani, HAO WAMENUNULIWA NA WAARABU tu hakuna jingine, ndugu zao waarabu wabantu siyo ndugu zao, MENTAL SLAVERY kuisha kazi!

How many Black Africans have been massacred? Hatujasikia hata wakilaani, HAO WAMENUNULIWA NA WAARABU tu hakuna jingine, ndugu zao waarabu wabantu siyo ndugu zao, MENTAL SLAVERY kuisha kazi!

mkuu .... tulihabarishwa kwamba Mh. Membe amepokea barua yenye ujumbe kutoka kwa Col. Muamar Ghadaffi kwenda kwa JK ..... au ndiyo utekelezaji wa ujumbe huo

My curiosity ni baada ya vita ninataka kuona MUNGU mwenye nguvu i.e atakayeibuka kidedea kati ya Mungu wa Wamarekani/wa-Libya/Arab leauge na Mungu wa Gaddafi/Shura ya Maimam/Waislamu wa Tanzania waliondamana kwa upande mwingine.

1.JPG

Taifa linaendelea kupata nyufa. Mwisho wa taifa la Tanzania unakaribia endapo hatutaziba nyufa.

Kila jambo linalofanywa na binadamu linayo matokeo mawili yasiyotarajiwa, Mazuri na mabaya. Ni muhimu kukosea ukiwa umechukua tahadhari kuliko kukosea pasipo kuchukua tahadhari.

Back
Top Bottom