Maandamano ya Kumsapoti JK Washington DC

Mpwa mimi sishabikii lolote ila niulize tu kuwa na wewe busara yako iko wapi unapotumia lugha chafu/kali namna hii? Kweli waweza kumuonya mtoto asitukane kwa kumtukana tena? Yaani kwa mfano; Wewe Mbwa (mtoto) acha kufanya ujinga wako hapo.

No nilitegemea kitu tofauit sasa kwa hali hii sioni chizi ni yupi na mwenye akili ni yupi unless ubadilishe lugha yako Mpwa, ni hilo tu na wala sipo kwenhye malumbano maana sina mpango wa kwenda kuishi ughaibuni kisha tulumbane kwenye nchi za watu.
Waraka huu ni kwako wewe hasidi wa upendo, utulivu, na amani ya taifa letu la Tanzania unayejiita Eliakim Mallya na wapuuzi wenzako. Sina uhakika kama kweli jina hilo ulilotoa ni lako, maana kina cha woga na ujinga ulionao, havikuwezeshi wewe kuwa na ushujaa wa kutoa jina lako la kweli. Ninasikitika kwamba imebidi watu wenye heshima zetu tukae chini kutoa kauli kuhusiana na upumbavu uliowekwa kwenye mtandao na mtu asiyekuwa na heshima wala adabu kama wewe, na wapuuzi wenzako wengine mlioko katika kapu moja.
Kwanza, tendo la kumvunjia heshima kiongozi wa taifa letu kwa kutoa kashifa iliyotolewa, pia ni tendo la kulivunjia heshima taifa letu na watu wake, jambo ambalo linakufanya wewe Eliakim Mallya na wote mnaohusika na kashifa hii kuwa mahayawani, maana hayawani hana aibu.

Pili, ukosefu wa utimamu wa akili yenu nyie mhusikao na kashifa hii, pia unajidhihirisha kwa jinsi mlivyojaribu kukosea heshima Watanzania tunaoishi Marekani kwa kujifanya kutuwakilisha wakati nyie ni vivuli. Ni mtu gani awezaye kusikiliza maneno yatokayo kwenye vinywa vya wapumbavu? Ninawajutia kuwa mmesoma kwa kiasi fulani lakini hamkuelimika hata kidogo.

Tatu, ninyi ni viumbe msiokuwa na tone la shukurani kwani pamoja na kwamba Tanzania iliwasomesha na kuwafikisha hapo mlipo (hamwezi kulikataa hilo), mnaanza kuisaliti na kuibeza. Hali kadhalika ninyi ni wasaliti wa utamaduni, mila na desturi za taifa letu na watu wake. Hadhi ya Watanzania iko katika kauli zao njema nyumbani na hata ughaibuni-mahali popote walipo. Taifa letu limepata sifa kubwa sana kutokana na ubora na mwenendo wa tabia za watu wake dunia nzima. Leo hii, watu wachache mliochanganyikiwa mnataka kuupaka matope ubora wetu; hatutaruhusu wala kukubali vitendo na mienendo ya kihuni.

Nne, wahenga walisema debe shinda haliachi kutika, na debe tupu haliachi kuvuma; ninyi mlionena na kuchapisha uvundo wenu huu, ni mifafano dhahiri ya methali hizo. Kwa vile Eliakim Mallya na wenzako mmetota, endeleeni kutota katika tope la ujinga na utovu wa adabu kama walivyo wahaini wa aina yenu.

Mwesigwa. Blandesi
 
Sasa Rais anawalinda mafisadi kivipi? Kazi ya kuwakamata wezi ni ya polisi, sasa wao ndiyo wanatakiwa wafanye kazi yao. Kama kuna FISADI anaechukua hela za nchi kwa njia ya wizi, hizo ni kazi za Usalama wa Taifa, ambapo Nyerere ndiye alikuwa mkuu wao kwa muda mrefu.<br />
<br />
Tuache lawama za kijinga kwa Rais kwa kila kitu. Nchi haiendeshwi na Rais peke yake. Kuna Waziri Mkuu, na mawaziri wengine waliojaa na kukaa maofisini bila ya kazi yoyote zaidi ya mikutano isiyoisha. Halafu kuna Wakuu wa Mikoa. Hawa ndiyo wanatakiwa walaumiwe zaidi.

Masaburi yako ww, mpumbavu usie na akili. Yani unakataa Jk hawalindi mafisadi?kwa taarifa yako kuwalinda ni pamoja na kuwaacha madarakani, na kuwaacha ndani ya chama chake! Acha kutumia masaburi kufikiri.
 
Back
Top Bottom