Maandamano ya Kumsapoti JK Washington DC

Ukweli ni kwamba JK anakuja kwenye mkutano wa UN ambao unafanyika kila mwaka mwezi wa tisa hivyo haji kwasababu ya Diaspora. Balozi alilengesha muda wa mwezi wa tisa kwasababu viongoizi wengi watakuwa hapa USA kwenye mkutano wa UN na ingekuwa rahisi kuwaalika kama inawezekana.

Mimi navyoona hii drama ni bora JK asije kwenye mkutano wa diaspora!. Na ni wazo baya kuchanganya huu mkutano na Ubalozi kwasababu inaleta siasa wakati kila mwaka tunafanya huu mkutano bila siasa za aina yeyote.

Kuliko hii drama ni bora tusimwalike JK tena!!
 
Huku Tz hatumtaki Jk...kwahiyo hata kama mtampa sapoti huko, ila dunia kwa sasa inajua kwamba dhahabu ya Tanzania imejaa damu za wananchi kama ninyi mnaona sawa kumsapoti jk basi mjue pia mnasapoti mauji haramu ya raia
 
Jamani tafuteni vibatari mmebe kuashiria nchi iko kwenye giza nene wakati rais kala suti smart utadhani yupo peponi.

Natamani ningekua huko maana huko hakuna risasi wala maji washa ...sana sana mtapata support mpaka kutoka kwa wazungu.
 
Kuna jitihada kubwa zinafanyika kuhakikisha Rais JK anapokewa kwa heshima atakapokuja Washington. Watanzania mnaombwa kushiriki kwa wingi ktk Ubalozi wa TZ uliopo Washington DC kumpa Support na changamoto Rais JK ambaya alishinda uchaguzi 2010. WTZ mliopo Marekania mnaombwa mjitokeze kwa wingi kumpa Support Rais JK.

Mpenda Haki, na Ukweli.
NY, USA

maandamano ya mashosti
 
Mimi nafikiri huyu blandesi ni house boy huko marekani hana muda wa kufahamu ulimwengu umefikia wapi katika suala la demokrasia na mengine.

Mawazo yake bado ni ya kikoloni ukizingatia kwamba bado anawatumikia wakolono huko usa kwa jinsi ambaypo inatofautiana kidogo sana na babu zetu waliouzwa utumwani.

Demokrasia haiwezi kuzuiwa kwa maneno ya vitisho, wakati wake umekuja kwa Tanzania, hakuna atgakayezuia!
 
Kama kuna watu 3 wataandamana kumsapoti Jua Kali...watapoteza muda wao maana watu 300 wataandamana kumpinga na kwa sababu hawa ndio watakuwa wamesimama upande wa haki kwa hali iilvyo watapata support kubwa hata kwa wamarekani maana msifikiri mataifa mengine hayajui hali ilivyo TZ..mtoa mada endeleza upupu wako ila ni wajinga tu unaoweza kuwapata si watu wenye kujitambua na wasioshobokea magamba na ngonjera zao
 
Waraka huu ni kwako wewe hasidi wa upendo, utulivu, na amani ya taifa letu la Tanzania unayejiita Eliakim Mallya na wapuuzi wenzako. Sina uhakika kama kweli jina hilo ulilotoa ni lako, maana kina cha woga na ujinga ulionao, havikuwezeshi wewe kuwa na ushujaa wa kutoa jina lako la kweli. Ninasikitika kwamba imebidi watu wenye heshima zetu tukae chini kutoa kauli kuhusiana na upumbavu uliowekwa kwenye mtandao na mtu asiyekuwa na heshima wala adabu kama wewe, na wapuuzi wenzako wengine mlioko katika kapu moja.
Kwanza, tendo la kumvunjia heshima kiongozi wa taifa letu kwa kutoa kashifa iliyotolewa, pia ni tendo la kulivunjia heshima taifa letu na watu wake, jambo ambalo linakufanya wewe Eliakim Mallya na wote mnaohusika na kashifa hii kuwa mahayawani, maana hayawani hana aibu.

Pili, ukosefu wa utimamu wa akili yenu nyie mhusikao na kashifa hii, pia unajidhihirisha kwa jinsi mlivyojaribu kukosea heshima Watanzania tunaoishi Marekani kwa kujifanya kutuwakilisha wakati nyie ni vivuli. Ni mtu gani awezaye kusikiliza maneno yatokayo kwenye vinywa vya wapumbavu? Ninawajutia kuwa mmesoma kwa kiasi fulani lakini hamkuelimika hata kidogo.

Tatu, ninyi ni viumbe msiokuwa na tone la shukurani kwani pamoja na kwamba Tanzania iliwasomesha na kuwafikisha hapo mlipo (hamwezi kulikataa hilo), mnaanza kuisaliti na kuibeza. Hali kadhalika ninyi ni wasaliti wa utamaduni, mila na desturi za taifa letu na watu wake. Hadhi ya Watanzania iko katika kauli zao njema nyumbani na hata ughaibuni-mahali popote walipo. Taifa letu limepata sifa kubwa sana kutokana na ubora na mwenendo wa tabia za watu wake dunia nzima. Leo hii, watu wachache mliochanganyikiwa mnataka kuupaka matope ubora wetu; hatutaruhusu wala kukubali vitendo na mienendo ya kihuni.

Nne, wahenga walisema debe shinda haliachi kutika, na debe tupu haliachi kuvuma; ninyi mlionena na kuchapisha uvundo wenu huu, ni mifafano dhahiri ya methali hizo. Kwa vile Eliakim Mallya na wenzako mmetota, endeleeni kutota katika tope la ujinga na utovu wa adabu kama walivyo wahaini wa aina yenu.

Mwesigwa. Blandesi
pili pili ya shamba imekuwashaje hacha umbea wewe
 
Nashauri JK awe anapitia kwenye hii forum ili ajionee mwenyewe jinsi raia tena wale wenye uelewa wa mambo yaani wasomi wasivompenda tena hata kumwombea mabaya kwa ukimya wake na maamuzi ya kusuasua au kushinikizwa. Kweli tumechoka maana ataongea hiki na yatatendeka mengine, hakika tunae rais rahisi.
 
Yaani mngejua waafrika hususan watanzania walioko marekani wanaishije...wala msingepoteza muda...Unadhani Dr. ASHA ROSE MIGIRO yuko huko USA kwa bahati mbaya eeh? Huko marekani mna uraia kwa kuukataa uraia wa nchi yenu leo hii mnajifanya watanzania?

Ni wamarekani wenye asili ya Tanzania. Na mtatumikishwa huko mpaka mkome mangusutu buthelezi ninyi.
 
Kama hukumchagua wewe wenzio walimchagua...maana alishinda ushindi mkubwa sana. Kama hujui wenzako wsnakusaliti...pole samaki...
 
Unaona ulivyokuwa huna nidhamu...kuna wazee wangapi makamanda wa jeshi la polisi nchini wenye vyeo na mafunzo ya kisasa ya kila aina..wasomi wa kada mbalimbali unawaita sungusungu.

Asante sana, lakini nakwambia utanasa tu
 
nilidhani waishio abroad wamepevuka fikra,lakini labda ni woga wa kutegema govnt sponsorship
 
Huna lolote wewe mwanaharamu kibaraka.Ni matatu,aidha wewe ni accessory to ufisadi (ndugu,rafiki,mnufaika , wa umafisadi),au ni walewale vijana wa Othman (which is most likely),au ni kale kaugonjwa ka kujikomba (which I doubt kwa vile ungetumia jina lako halisi ili hao unaojikomba kwao wakuone).

Mpuuzi wewe unataka kuturejesha zama za chama kimoja ambapo kiongozi ni Mungu-mtu.Kwanini unalazimisha matakwa yako yawe ya dunia nzima?Kama ni haki kwako kumpenda Kikwete basi ni haki pia kwa mwingine kutompenda.Maandamano dhdi ya Kikwete hayalengi kumdhalilisha wala kumchafulia jina.Ni harakati za Watanzania wenye uchungu na nchi yao wanaodai kilicho bora kwa taifa lao.Sasa kosa lao hadi hapo ni lipi?

Lugha unayotumia ni kama anayotumia Riz One huko Twitter.Imejaa ngebe,kejeli na matusi.Ni uwendawazimu kumkalia kooni Bwana Mallya kwa madai ya kumdhalilisha Rais ilhali na wewe unafanya kilekile kuwadhalilisha Watanzania wenzako wenye mawazo tofauti na yako.
Anyway,pole na swaum bwana kiseo

Mkuu ndo kawaida ya wapambe anaona nisahihi wtz kudhalilishwa na jk
kwa kupigishwa foleni kwenye vituo vya mafuta,wajawazito kununuliwa bajaji,
kumwomba bush msaada wa vyandarua,kudhuriwa na maji ya mto
tigite,watoto kupewa net huku wazazi wakiachwa waugue malaria,
safari za kichama nje ya nchi zinazolipiwa na serikali n.k.

Mtu anayepinga wananchi kumwonesha hisia zao Rais akiwa ugaibuni
ujue naye nisehemu ya taizo.Tunawaunga mkono ndugu zetu
andamaneni na ktk mabango mtakayo beba moja liandikeni JK YAKO
WAPI MAISHA BORA ULIYOWAAHIDI WATANZANIA?

Tupo pamoja.
 
Back
Top Bottom