Maandamano ya kumpokea Nundu yapigwa stop!

Huu ujinga unaotaka kuota mizizi kwenye nchi hii usipokemewa, adui umaskini na maradhi itakuwa ngumu sana kupigana nao, maana nilishangawa kuona mashabiki wa Simba walipokwenda uwanja wa ndege na matarumbeta kuipokea timu yao eti imetolewa kiume kule Sudan!! huu ni zaidi ya ujinga.
ni kwa sababu wakishafukuzwa uwaziri wanabaki huru kuendelea kutanua na zile walizoiba ingekuwa leo umetimuliwa kesho upo lupango kesho kutwa mahamani huu ujinga wa maandamano ya kupongezana kwa kuuibia serikali ungetoka wapi??ila habari ya simba sio ya kisiasa acha kuchanganya mambo mazee!!
 
Vipi Tanga kwetu kunani tena jamani? yaani kweli hawana ubomgo wa kuwaza kiasi hicho? nipo hapa Tanga Majestic subiri ntapitia kwa Mheshimiwa nimjulie hali
Mimi niko hapa makorora napaka rangi na kuandika mabango ya kumsifu mheshimiwa. Nitasononeka sana kama wanaintelijensia watakuwa wamezuia maandamano yetu ya kuonyesha upendo kwa Mb wetu.
 
labda yamezuiliwa ili asije kudhurika na wananchi wenye hasira kali dhidi ya wizi aliotaka kuufanya!
 
Wanajamvi Heshima mbele..

Miongoni mwa habari iliyoandikwa sana na magazeti ya leo tarehe 21 Mei ni ile ya Polisi Mkoani Tanga kuzuia maandamano ya kumpokea Omari Nundu jimboni kwake. Imekuwa ni tabia ya wanasiasa kujiandalia mapokezi makubwa kwenye majimbo yao pale wanapokumbwa na masahibu ya kisiasa. Kumbukumbu zangu zinanirudisha nyuma kwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu EL na Endrew Chenge ambao walifanyiwa maandamano makubwa ya kuwapokea walipojiuzulu.

Kitendo cha mtu kupokelewa kwa maandamano kinaashiria ushujaa wa mtu huyo na imani kubwa watu waliyonayo dhidi yake. Kwa mfano Deo Filikunjombe alistahili mapokezi makubwa na ya heshima kwa yale aliyoyatenda na kuyaongea alipokuwa bungeni. Je kuna lipi la maana ambalo linamfanya Omari Nundu astahili mapokezi makubwa.. At least EL na EC wao walijiuzulu (labda ni ushujaa). Lakini Omari Nundu amepigwa chini kwa kushindwa kuwajibika! Naamini mapokezi haya wanayaratibu wabunge wenyewe ili kujaribu kuwazuga watu kwamba wao bado wanapendwa!

My take: Wanasiasa mnaoshindwa ku-deliver msiwababaishe watu kwa mbwembwe za mapokezi ambayo hayana tija zaidi ya kuwapotezea muda watu! Na kwa hili la Nundu, nawapa Big Up Polisi....
 
Hivi jamani kweli hao watu wanao kwenda kuwapokea wana uelewa gani. Hivi kweli mtu mwenye akili timamu let say mtu mwenye uelewa tu hata kama hajasoma anaweza kwenda kumpokea kiongozi aliye pigwa chini kwa wizi. Mimi nina mashaka na hao wapokeaji kama hawapewi chochote au kwa namna moja au nyingine walinufaika na utawala wa Nundu vinginevyo wanamatizo makubwa ya kuelewa.
 
N ikumbukwe wengine walijiuzulu huyu kafukuzwa so he is more villain than wenzake waliojiuzulu!
 
I guess kuna somo serikali inajifunza kwamba huu sio wakati wa kuendekeza sherehe na mashangilio ya kuwafumba watu macho wakati kila kitu kiko wazi, inawezekana sana huko juu wamewaambia Polisi kwamba waipige Stop hiyo kitu. Ukifikiria sana huwezi kuona RPC anaweza kukurupuka akazuia hili, itakuwa kapewa maelekezo kwamba hiyo sasa si nzuri tena kama ilivyokuwa zamani. Picha inaanzia pale JK alipokubali kwamba mabadiliko wanayoyataka wananchi yanastahili na akakubali kwamba atalitekeleza, sasa haiwezekani yeye JK akung'oe halafu uende mtaani kwenu ukashangilie. Unashangilia kufukuzwa au unamzomea aliyekufukuza? It doesn't make sense..!
 
..mara ya kwanza kusikia maandamano ya wana CCM yamezuia!!



Tatizo siyo maandamano, huyu bwana haaminiki anaweza akalipua mabomu yaliyobaki siku alipoongea na vyombo vya habari. Huyu Mh. Hana cha kufichaficha sijui alitaka kuongea nini baada ya hayo maandamano.
 
Vipi Tanga kwetu kunani tena jamani? yaani kweli hawana ubomgo wa kuwaza kiasi hicho? nipo hapa Tanga Majestic subiri ntapitia kwa Mheshimiwa nimjulie hali
Elli mpwa leo kuna picha gani hapo?
 
Last edited by a moderator:
hIVI mANI MNAFANYEJE HAKO KAMCHEZO KAKU-MENTION
Elli unatakiwa uanze na @ bila kuacha space halafu ndio unaandika ID ya mtu unaetaka kum mention, na siku hizi hapo juu kuna option ya kutag watu unaowataka waione thread yako au hata hii kwa kuclic hapo na kutumia maelekezo haya haya kwenye kutag.
 
Huu ujinga unaotaka kuota mizizi kwenye nchi hii usipokemewa, adui umaskini na maradhi itakuwa ngumu sana kupigana nao, maana nilishangawa kuona mashabiki wa Simba walipokwenda uwanja wa ndege na matarumbeta kuipokea timu yao eti imetolewa kiume kule Sudan!! huu ni zaidi ya ujinga.
Matola Kumbe ndio maana timu zetu haziendelei na mpira wetu haukui..kutokana na watu wenye akili mgando kama ya kwako!! kwa hiyo wakifanya vibaya wasipokelewe? mnataka kila siku washinde? mbona timu za ulaya wanakuwa wamefungwa lakini mashabiki wanaimba hadi mwisho......nao ni wajinga???
 
Last edited by a moderator:
Matola ngoja nijaribu kaka
Elli unatakiwa uanze na @ bila kuacha space halafu ndio unaandika ID ya mtu unaetaka kum mention, na siku hizi hapo juu kuna option ya kutag watu unaowataka waione thread yako au hata hii kwa kuclic hapo na kutumia maelekezo haya haya kwenye kutag.
 
Last edited by a moderator:
Matola ngoja nijaribu kaka
Elli umefauru kazi kwako sasa, na usisahau pale juu kuna option ya thread tag, ukitaka Members fulani waione thread yako unapaswa uwatag na hata kwenye thread hii unaweza kumtag mtu unayemtaka then atapata notification.
 
Last edited by a moderator:
na tatizo wapo wabongo ambao wakiambiwa 'serikali imesema' wanakuwa kama mbwa mbele ya chatu...

Mkuu MM ningetarajia uwaase Vijana na wengineo tuheshimu Serekali
. Sijui wewe unatakaje kwenye hili?
Ukumbumbuke Serekali ni Serekali, Haina Mkono mrefu tu na Mkubwa pia!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom