Maandamano ya kihistoria shinyanga

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,780
3,227
Wanafunzi wa shule ya msingi Jomu wakiwa katika maandamamo ya Chama cha Demokaria na Maendeleo yaliofanyika mjini Shinyanga jana huku wakiwa wameshikana na kuonesha alama ya VIDOLE VIWILI.


Wana JF sasa naanza kuamini saa ya ukombozi imefika Watanzania tuko pamoja bila kujali rika

maandamano%2Bjomu%2Bshy.JPG




maandamano%2Bshy.JPG

Viongozi wa Chadema na wabunge wa chama hicho wakiwa wanaandamana mkoani Shinyanga huku akiwa ametanguliwa na vijana wa chama hicho Redbriged



mfumuko%2Bwa%2Bbei%2Bndiyo%2Bmaisha%2Bbora%2Bkwa%2Bkila%2Bmtanzania.1.JPG



Mabango mbalimbali ya waandamanaji wa mkoa wa Shinyanga yakionekana kuwa na ujumbe mbalimbali kwa rais Kikwete.


shilembi%2Bmagadula.JPG


Aliyekuwa Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini Shilembi Magadula Shilembi ambaye kutotangazwa kakwe mshindi kulisababisha vulugu kubwa katika mji wa Shinyanga na kuchomwa moto kwa ofisi za Halmashauri


mbowe.JPG


Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe akisisitiza kuendelea na maandamano kumjibu Rais Jakaya Kikwete


 
nassisimkwa na mwili hasa baada ya kuona picha hizo, jamani ukombozi unawadia na wajibu wetu kuhamasishana na kumpinga mkwere kwa nguvu zootna hakika tutamtoa hadi watoto wa shule ya msingi wameona mapungufu ya mkwere kweli kiama chake kipo karibu haijawahi tokea katika historia ya Tanganyika. Mungu ibariki Tanganyika yetu.
 
Imekaa vizuri hiyo ya madenti.... ila nina shaka sana na kibarua cha Mwalimu mkuu wa shule hiyo.
 
safi,acha vijana wafanye kile wanachoona kifaa kwao,siasa zetu hazilazimishi nani awe chama gani
pongezi kwa wanafunzi,huu ni wakati wa kufanya maamuzi
 
Kama wanafunzi wamediriki kufanya hivyo, wafanyakazi vipiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii? TUCTA tunasubiri reaction yenu kwani nchi inateketea na watoto wa shule ya msingi wamebaini hilo upande wenu TUCTA VIPI??? au shwari tu??
 
Maandamano ni mbinu mojawapo ya kupeleka ujumbe kwa serikali!!!! Peoples Power!!! Achana nayo kabisaaaaaa, tujifunze kaskazini mwa Afrika! Sisi siyo kisiwa!
 
Darasani wanakaa muda gani hao???? Paper ikija si watafeli tena????

Wanafunzi wanakaa darasani ili wapate mafunzo, kama waalimu hawapo wapo kutafuta mshahara wao halmashauri hakuna faida ya wanafunzi kukaa darasani na ndio maana wanaona afadhali nao waandamane kuwaunga mkono wazazi wao wanaoshindwa kuwapatia mahitaji yao kwa sababu ya uchumi mbovu unaosababishwa na viongozi wasanii!!
 
Nataka kuwaarifu Vijana wa Chadema kwamba Muasisi wa chama chenu anajisikia vizuri sana kuona jinsi wananchi wanavyotuunga mkono katika maandamano haya ya amani yanayolenga kufafanua na kueneza ujumbe na hoja zetu.

UZI NI HUO HUO!!!! HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
maandamano%2Bjomu%2Bshy.JPG


Wasukuma wana tabia kwamba wakitosa wanakutosa kweli kweli, familia nzima au ukoo mzima wanakususa na ndivyo inavyoonekana katika picha hiyo kwamba sasa CCM wameitosa jumla.Miaka ya nyuma CCM waliwekeza kwa wasukuma kuzoa kura, safari hii mambo kinyume.


Wasukuma ni moja ya makabila yanayoamini kanuni ya RISK TAKER.wao wana misemo yao inayothibitisha kuwa ni risk taker mfano; nduhu makoye, JAFA BUJIKU, MAGUZU MASESE, MAHELA MABONWA( hamna shida) na mengine mengi.
Leo hii wasukuma wameamua ku-take risk kwa kukihama CCM wao na familia zao kama unavyoona watoto wao wako mstari wa mbele kukiunga mkono CDM, watoto hao wamepewa maelekezo na wazazi kuwa; neendeni shule lakini maandamano msikose.


Mheshiwa Regia ni shahidiwa haya kwani kwake kilombero hawa jamaa kina ngosha wako sana na kule wamekimwaga CCM

sUBIRINI MTASHUHUDIA MENGI.
 
Inahamasisha na inatia moyo kwani matumaini ya ukombozi yanaonekana na haya ndio yanaowapa wazimu watawala wanyonyaji tulionao
 
Mwanafunzi wa pili kutoka kushoto yupo peku, lakini anaonekana kuamasika sana kwa vidole vyake viwili juu!!!!! Mungu awasaidie waweze kumaliza shule zao vizuri!
 
Back
Top Bottom