Maandamano ya Januari, Tuvae Fulana za Dr. Slaa

Haya sasa tuangalie uwezekano wa kuzipata sasa, naomba kama kuna mwenzetu mwenye access na wakuu wa CDM awasilishe hoja yetu kwa niaba ya sisi wote tuliotayari...sio lazima tukubaliane na kila mtu.

Kwa kweli wazo hili ni zuri,

Fulana zitengenezwe, ziingizwe sokoni tuko wengi tunazingoja.

Please, ujumbe huu naamini umewafika walengwa tunaomba utekelezaji.
 
na wale wana ccm wanaohitaji mabadiliko ya katiba wavae nn? sioni kama ni wazo zuri. natamani katika swala la katiba mpya, tuweke siasa pembeni.
 
na wale wana ccm wanaohitaji mabadiliko ya katiba wavae nn? sioni kama ni wazo zuri. natamani katika swala la katiba mpya, tuweke siasa pembeni.

Ishu ya katiba ni tofauti kidogo, maandamano yatakuwa ni kupinga ONGEZEKO YA BEI UMEME, na Kubebesha mzigo watanzania kuubeba wakati makampuni ya wawekezaji wanasamehewa kodi.

Dr. Slaa amekuwa mstari wa Mbele kutetea Maslahi ya Wanyonge na matumizi mabaya ya pesa za umma

watu kuingia mikataba mibovu kwa makusudi, wanafungamanisha hiyo mikataba kuwa ni ya maisha isiyo na kikomo, halafu et sie tusiifahamu kwa kuwa ni siri, wakati huo huo haina tija kwa nchi.

Baada ya Maandamano Mziki wa Katiba ndiyo unasambaa nchi nzima tena.
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia zaid ya 100.
Ila itapendeza zaid pakiwa na bendera za vyama mbali mbali vya upinzania pamoja na CUF , NCCR n.k kuonyesha tupo pamoja kwenye ishu za maslahi ya Taifa.
 
Katika nchi za kiarabu watu huwa wanaandamana kuipinga Israel kwa kukalia maeneo ya Palestina na pia kuipinga Marekani kwa kuunga mkono ukatili wa Israel.
Huwa wanabeba bendera za Marekani na Israel na kuzichoma moto.

Hivyo tusisahau viberiti...
Yote ni kuonyesha UCHUNGU na HASIRA za wananchi dhidi ya Serikali isiyojali wananchi hata kidogo.
 
Hili ni wazo la hovyo.

Mnaounga mkono hamna jinsi ya kutumia muda wenu vizuri zaidi?

Bado mtalalamikia umaskini wenu wakati muda mnaupoteza kwa mambo ya kipuuzi?

Haya ni mambo ya kitoto ....hata hivyo mkikua mtaacha!
 
Katika nchi za kiarabu watu huwa wanaandamana kuipinga Israel kwa kukalia maeneo ya Palestina na pia kuipinga Marekani kwa kuunga mkono ukatili wa Israel.
Huwa wanabeba bendera za Marekani na Israel na kuzichoma moto.

Hivyo tusisahau viberiti...
Yote ni kuonyesha UCHUNGU na HASIRA za wananchi dhidi ya Serikali isiyojali wananchi hata kidogo.

Sidhani kama ni wazo linalofaa kwa maandamano hayo.
Ingefaa tuihoji serkali juu ya Hatma ya Mikataba kama hii:
RICHMOND/DOWANS

IPTL
RITES
ALLIANCE AIR
ALEX STEWART
TICTS
LOLIONDO
RADAR
NDEGE YA RAIS
MISAMAHA YA KODI KAMPUNI ZA KIGENI
KUONGEZWA GHARAMA KUBWA ktk UMEME bila kujali ATHARI ktk BIDHAA na uhalisia wa kipato chetu
MEREMETA
Tutahoji matumizi mabaya ya mali ya umma
KUJENGA BARABARA KUZUNGUKA MLIMA KILIMANJARO wakati kuna nyani,swala,twiga nk
KUJENGA BARABARA MBUGANI SERENGETI badala ya kupitia HYDOM,BARIADI HADI LAMADI
KODI ZETU KUWALIPA WAKUU WA WILAYA/MIKOA WAKATI NI WATUMISHI WA SI SI EM:whoo:
 
Hii akili yangu bana iko jaa ugoro mtupu...........MIMI NILIELEWA MAANDAMANO YA MTOTO WAKE NA KATIBU MKUU WA CCM.
 
naunga mkono kwa 100%.Watanzania tujiulize,kama wakati wa kampeni za uchaguzi,serikali ya ccm iliweza kununua mabango yaliyotosha hata miti na mbwa wakavaa,je,hawa wanashindwaje kutatua tatizo la umeme.wizi mtupu.Tuandamane tuwapashe habari kwamba watanzania wanauwezo wa kufahamu mambo hata kuwaangalia sura zao la kifisadi.
 
Sidhani kama ni wazo linalofaa kwa maandamano hayo.
Ingefaa tuihoji serkali juu ya Hatma ya Mikataba kama hii:
RICHMOND/DOWANS

IPTL
RITES
ALLIANCE AIR
ALEX STEWART
TICTS
LOLIONDO
RADAR
NDEGE YA RAIS
MISAMAHA YA KODI KAMPUNI ZA KIGENI
KUONGEZWA GHARAMA KUBWA ktk UMEME bila kujali ATHARI ktk BIDHAA na uhalisia wa kipato chetu
MEREMETA
Tutahoji matumizi mabaya ya mali ya umma
KUJENGA BARABARA KUZUNGUKA MLIMA KILIMANJARO wakati kuna nyani,swala,twiga nk
KUJENGA BARABARA MBUGANI SERENGETI badala ya kupitia HYDOM,BARIADI HADI LAMADI
KODI ZETU KUWALIPA WAKUU WA WILAYA/MIKOA WAKATI NI WATUMISHI WA SI SI EM:whoo:

Kuchoma kiambaa/nguo ni 'symbolic' tu.

Pia naongezea kwenye maelezo/maswali yako kwa Serikali:

Pia Serikali hii iulizwe kwanini haitaki kununua Mitambo yake yenyewe ya kuzalisha umeme? imilikiwe na Serikali/Tanesco?

Kwanini viongozi wa Serikali wanang'ang'ania kuanzisha makampuni yao binafsi (Richmond/Dowans/IPTL etc.) badala ya kununua na kumiliki mitambo kwa niaba ya watanzania?

Kwanini hawataki kufanya haya wakati wanajua kuwa kumiliki mitambo kutaondoa malipo ya kifisadi yanayoitwa 'Capacity charge?'

Nini imekuwa hatima ya lile gari Land Cruiser V8 'alilolikataa' Pinda (thamani sh milioni 280)? Je ni V8 mpya ngapi zimemwagwa? Zapo nyingi sana sasa. Kwanini Serikali inatumia matrilioni kununua magari haya ya gharama sana badala ya kuboresha huduma za ELIMU na AFYA?
 
Back
Top Bottom