Maandamano ya CHADEMA yaanza kutoa matunda, makali ya maisha sasa kupunguzwa!

Bei ya petrol inapanda kila kukicha, huo unafuu utatoka wapi? Hawa watu ni wasanii sana, tunasubiria treni ya umeme Kigoma.
 
Hapa suluhisho la kudumu na la maana ni kuhakikisha serikali inapunguza matumizi yasiyo ya lazima na anasa na wakati huo huo kuongeza pato la taifa kupitia uzalishaji bora na wa kutosha kutoka katika rasilimali zetu.
Pia wazingatie ulinganifu wa thamani ya pesa wanazolipa kwa wazabuni na wakandarasi na huduma wanazotoa kama kweli zinaridhisha. Wengi wa hao wazabuni na wakandarasi ni walanguzi, matapeli na wezi watupu. Wanatuibia fedha nyingi na kutusababishia hasara kubwa sana kwa huduma zao feki na mbovu.
 
Eti twaambiwa hali ngumu tumeiridhi toka awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi yetu, hivyo tusilaumu kwa awamu ya sasa kuwa imeshindwa kutatua kero za wananchi ikiwamo kupanda kwa gharama za maisha....kama vipi wabwage manyanga CHADEMA waonyeshe uwezo...:embarassed2:
 
Cement??? Ishushwe bei maana hata mali ghafi zinapatikana hapa hapa Tanzania.

Nini kinasababisha bei ya cement iwe juu?


Haya Elimu bure,,,, Tudai

CHADEMA GO, MAANDAMANO KWA KWENDA MBELE.

Mapambano bado yanaendelea
 
yale maandamano ya chadema sasa yameanza kutoa matunda baada ya Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya M Kikwete kuagiza msamaha wa kodi katika bidhaa mbalimbali utolewe lengo likiwa ni kupunguza ukali wa maisha kwa watanzania,ikumbukwe vizuri kwamba ukali wa maisha ilikuwa ni ajenda kubwa ya chadema hivi karibuni na sasa kero hiyo na nyinginezo sasa zitaanza kuwa na ahueni kama sio kwisha kabisa,

habari kamili kama ilivyoripotiwa na magazeti ya leo

RAIS Jakaya Kikwete ameingilia kati bei ya bidhaa kupanda nchini, hivyo kuiagiza Wizara ya Fedha na Uchumi kupunguza mfumuko wa bei. Amesema ikiwezekana, wizara itoe msamaha wa kodi ili kuwapunguzia wananchi makali ya maisha.

Rais Kikwete alitoa agizo hilo jana, mjini Dar es Salaam, alipotembelea makao makuu ya wizara hiyo na taasisi zilizo chini yake, ambapo alizungumza na watendaji. Alisema licha ya wizara kufanya vizuri katika makusanyo ya kodi, inapaswa kuangalia namna ya kupunguza mfumuko wa bei, ili kutoa nafuu ya maisha kwa Watanzania.

"Ikiwezekana angalieni namna ya kupunguza kodi, ingawa hilo linaweza kutupunguzia mapato lakini inafaa kufanya hivyo ili kutoa ahueni ya maisha kwa wananchi," alisema.

Katika ukusanyaji kodi, alisema wizara imefikia lengo la serikali, ambapo Desemba, mwaka jana ilikusanya zaidi ya sh. bilioni 500. Hata hivyo, alisema ni vyema ikageukia katika kuinua uchumi wa nchi, hususan kupunguza mfumuko wa bei ili mwananchi wa kawaida apate nafuu ya maisha.

Aliitaka pia wizara kujikita katika kuzipa nguvu sekta zenye mchango mkubwa katika ukuaji uchumi.

MADENI YA WASTAAFU
Rais Kikwete ameitaka wizara hiyo kumaliza malipo ya madeni ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), ili serikali iondokane na mzigo wa kudaiwa na wazee hao.

Alisema juhudi kubwa zimefanywa na wizara katika kuwalipa wastaafu hao na kwamba, waliosalia ni wachache.


Kutokana na hilo, alisema ni vyema
wakalipwa haraka ili kuondokana na mzigo wa kudaiwa.

"
Hili la wastaafu wa Afrika Mashariki nalo limalizeni, hatuwezi kuendelea nalo siku zote, walipeni," alisema.

MALIPO YA WALIMU

Akizungumzia malipo ya walimu, rais Kikwete aliitaka wizara kuwa na utaratibu mzuri wa kuwalipa, hususan wanaoripoti vituoni kwa mara ya kwanza, ili kuepusha usumbufu wa kudai stahili zao.

Kwa mujibu wa rais Kikwete, wizara imeweza kurekebisha kwa kiasi kikubwa kasoro ya ucheleweshaji mishahara ya watumishi wa umma.

Hata hivyo, alisema bado tatizo la walimu wapya kutolipwa kwa wakati linaendelea, hivyo linapaswa kushughulikiwa ili lisijirudie.

Alirejea agizo la kuzuia uhamisho wa watumishi, pale inapokuwa hakuna maandalizi, ikiwemo fedha. Alisema ofisa yeyote wa serikali atakayehusika kufanya hivyo bila maagizo achukuliwe hatua za kinidhamu, ikiwemo kukatwa mshahara.

Kuhusu maslahi ya watumishi wa serikali, aliiagiza wizara hiyo kuangalia uwezekano wa kuwadhamini wafanyakazi katika taasisi za fedha ili wapate mikopo kwa urahisi.

Rais Kikwete alisema ili kuwasaidia watumishi hao kujiongezea kipato, ni vyema wizara ikaandaa utaratibu wa kuwadhamini katika taasisi za fedha, hususan wale wenye muda mrefu wa kuendelea kuitumikia serikali.

Aliagiza kuharakishwa mchakato wa kupatikana Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali, atakayehusika na usimamizi wa fedha za halmashauri, ili kukabiliana na ubadhirifu.

Rais Kikwete alisema Naibu Mhasibu Mkuu atahusika moja kwa moja katika usimamizi wa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri.

Wizara pia imetakiwa kuongeza uwezo wa wakaguzi wa ndani na idara za serikali, ili wafanye kazi kwa uhuru bila kuingiliwa.

"Wakaguzi wa ndani wasiwe wanawajibika kwa makatibu wakuu, kwa kuwa wao nao ni miongoni mwa wanaochunguzwa, hivyo wakiwa wanawajibika kwao watakosa uhuru wa kufanya kazi vizuri," alisema.

ZIARA TRA

Akiwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), rais Kikwete alipokea taarifa ya utendaji kazi kutoka kwa uongozi wa mamlaka hiyo.

Katika hatua nyingine, akiwa mlangoni akitoka ofisi hizo, alilazimika kusimama kuwasikiliza watu waliokuwa wakipaza sauti kumuomba asikilize kilio chao.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Joseph Mwakalinga, aliyejitambulisha kuwa mfanyabiashara ya magari kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, alimuomba rais kuingilia kati suala la kutozwa ushuru mara mbili.

Mwakalinga alisema TRA huwatoza kodi wanapoingiza gari kutoka Zanzibar, licha ya kuwa lilikwishalipiwa visiwani humo.

Rais Kikwete aliwataka kuunda umoja na aliahidi kukutana nao wiki hii ili kusikiliza matatizo yao.

Je, ameziogopa siku tisa?!!!!!!!!!!!!!
 
hawezi kushindana na nguvu ya ummma,kama kawaida kuvuja kwa pakacha furaha kwetu raia,
 
Anajaribu kuwatuliza tu...mabadiliko ya kweli yanatakiwa kuanza kwenye ishu kubwa kama kuwakaba mafisadi na kutochezea kodi za wadanganyika kulipa makampuni yasiyoeleweka!
 
Angalizo,ningeanza na kupunguza starehe serekalini.economy may go offroad! anyway, hata hizo kodi zipungue tu maana huwaga twamkusanyia ra tu ora tu
 
Joyce utetezi wako ni dhaifu na hauna maslahi kwa taifa! Rais wetu ni mwepesi sana haonyeshi uelewa wa mfumo wa kodi na haonyeshi ubunifu wowote katika kutoa muongozo kodi zipi zipunguzwe na zipi sipunguzwe! Mapato ya serikali yanatokana kodi mbalimbali rais alipaswa kuonyesha uongozi (ukizingatia ni mchumi kitaaluma) kwamba ni kodi zipe zipunguzwe na zipi zibaki. Kwa yeye kuwaambia wizara wapunguze kodi bila ya kutoa maelekezo specific ni dhairi anauelewa mdogo wa mfumo wetu wa kodi na uchumi kwa ujumla!agizo hili lingeweza kutolewa na mwanafunzi wa uchumi wa kidato cha sita! Rais wetu hatukumjua vizuri ni mwepesi tusingempa kura zetu!
 
Ndio kazi ya upinzani,kuisukuma serekali,hasa iliyolala kama yetu hii itekeleze majukumu yake!
 
Back
Top Bottom