Maandamano ya ajabu - polisi wapelekewa maiti

Babu Lao

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
2,043
179
JESHI la Polisi Mkoani Mara jana lililazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wananchi wa Bunda mkoani Mara ambao walikuwa wamechukua jeneza la mtu ambaye alidaiwa kufa kwenye mazingira ya kutatanisha.

Tukio hilo limetokea jana jioni mkoani humo. Wananchi wa eneo hilo, kwa nyakati tofauti, walidai kuwa baada ya kuifunua maiti hiyo iliyokuwa ndani ya jeneza walikuta ikitoa machozi, hali ambayo ilizua hofu kwa waombolezaji na kudai kuwa kuna mkono wa mtu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, maiti hiyo ilianza kutoa machozi mara baada ya mama mdogo wa marehemu huyo kufika eneo hilo na kuanza kuiangalia na ndipo ilipoanza kudondosha machozi.

Kutokana na kitendo hicho, ndugu wa marehemu hawakukubaliana nacho ndipo walipotaka hatua za kisheria zifuatwe ili wamfahamu aliyehusika na tukio hilo.

Hali hiyo ilisababisha baadhi ya waombolezaji kufanya maandamano huku wakiwa wamebeba maiti yao kwenye mkokoteni hadi kituo cha polisi kwa ajili ya hatua zaidi.

Polisi baada ya kuona umati wa watu umezingira katika kituo chao huku wakileta vurugu walilazimika kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi.

Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja mama mdogo huyo alitoweka katika mazingira gani.
 
Sasa wa TZ tunakoelekea ni kubaya sana, Sasa police watamjuaje mchawi?
Jaman hao watu wote walioenda police kweli kwa kichwa ni salama?
 
yAANI SIJUI TUTAELIMIKA LINI HUU UJINGA NDIO UNATUFANYA TUENDELEE KUAMINI UCHAWI MPKA LEO,KILA TUNDU LA MWANADAMU HUTOA MAJI MTU ANAPOKUFA NDIO MAANA HOSPITALI HUFANYA LAST OFFICE HUZIBA MATUNDU YOTE KWA PAMBA MDOMO MACHO PUA MASKIO ,UKE NA NJIA YA HAJA KUBWA WANATAKIWA KUPEWA ELIMU TUU
 
mtuhumiwa alifichwa na police mahabusu ili asuwawe.wananchi wakaamua kupeleka maiti hukohuko police aifufue
 
Inasemekana huyo mwanamke anayedaiwa kumroga marehemu ana mwenzake waliyeshirikiana kufanya huo ulozi hivyo akatakiwa kumtafuta ili waje kumfufua ndipo baadhi ya wanachi waliamua kupiga simu polisi kuhofia uvunjifu wa amani.Maiti ilipelekwa Mortuary lakini jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu walikabidhiwa polisi.....
 
yAANI SIJUI TUTAELIMIKA LINI HUU UJINGA NDIO UNATUFANYA TUENDELEE KUAMINI UCHAWI MPKA LEO,KILA TUNDU LA MWANADAMU HUTOA MAJI MTU ANAPOKUFA NDIO MAANA HOSPITALI HUFANYA LAST OFFICE HUZIBA MATUNDU YOTE KWA PAMBA MDOMO MACHO PUA MASKIO ,UKE NA NJIA YA HAJA KUBWA WANATAKIWA KUPEWA ELIMU TUU

Nadhani elimu tuyoipata haitusaidii chochote mpendwa.. sababu kila tukio katika jamii tunalihusisha na uchawi tu!!!!:help:
 
Sasa wa TZ tunakoelekea ni kubaya sana, Sasa police watamjuaje mchawi?
Jaman hao watu wote walioenda police kweli kwa kichwa ni salama?

Ah! Mkuu unashangaa hilo!, watu wameacha ma hosptl na madaktari bingwa. wako kwenye vichuguu samunge wanamsubiri Babu aamke anaongea na Mungu. Hiyo ndio Tz.
 
Hii kali.....imani za kishirikina zimetujaa hadi tunashindwa kutumia akili ya kawaida!
 
Badala ya kumpeleka maiti hospitali akafanyiwe uchunguzi kama tayari amekuwa maiti au bado au ndio anaelekea kuwa maiti wanaenda polisi. Inadaiwa kuwa mtu ufa taratibu yaani mpaka brain yote izimike na sio kusimamam kwa moyo tu ndio maana mpaka leo 'bull dozer' wa Wayahudi yuko hai!!
 
Hii inaonyesha jinsi watanganyika tusivyomjua Mungu. Maiti itatoaje machozi? Watheolojia wapeleke injili huko.

Back
Top Bottom