Maandamano UDSM sasa yaongozwa na 'AL-SHABAAB'?

Guyz,
Naombeni mnielewe, msione kama mimi napinga kila kitu. Na mimi nilisoma kwenye chuo hicho hicho na migomo ilikuwepo. Ukijaribu kufanya analyis ya migomo ya miaka hii, yote ni yakitoto, kwanza hawapo organized. Wanajigomea tu, hawana common objective!Wanaogoma ni kikundi tu cha wanafunzi. Migomo imekuwa inafanywa kila siku kudai vitu ambavyo hata havina msingi. Haipose threat yoyote kwa serikali. Miaka yetu ilikuwa ukisikia chuo kikuu wamegoma(miaka hiyo kilikuwa kimoja tu) kila mtu alikuwa anatetemeka. Siku hizi imeshakuwa routine! Tumeshaona ni kitu cha kawaida, ndio maana mwaka jana UD waligoma 3 dayz mfulululizo lakini chuo hakikufungwa wakati kisheria ingetakiwa kifungwe!

Kipindi kile mlikuwa na common objectives kwa kuwa majority mlikuwa ni watoto toka vijijini, uchumi wenu ulifanana na hali ya kiuchumi ya taifa ilikuwa inawafanya hata matajiri waonekane maskini hivyo mlipmbana kama wamoja.

Rejao wewe siku hizi ni matawi ya juu, uchumi wako uko juu, tayari ulisha mwandaa mwanao kufikiria kibepari kwani pesa unazo, na mwanao kwa ujinga uliomlisha na kuona yeye ana hela za kutosha, huwezi kumwondoa kwenye thinking hiyo.

Kinachofanyika, ni kwa wale majority ambao hali zetu bado ziko chini kuwalazimisha hata mwanao akubaliane na matakwa ya maskini, na akigoma, lazima kiboko achapwe kumlazi9misha kufikiria waliowengi maskini kazi ambayo wewe uliitelekeza kwa kumlea mwanao atambue pesa/nafasi uliyonayo imetokana na uwezo wako wakati ukweli siyo
 
Natamni nikuone ukimaliza chuo utakavyokuwa unahangaika kwenye maofisi na vibahasha vya kaki

Kwani kugratuate Moro Muslim kunatatizo gani? chamuhimu ni cheti na maisha bora baada ya hapo!

kumbe umeaandika uongo kuwa enzi zenu mligoma. Moro muslimu hawajawahi kugoma,na wana miaka si zaidi ya mitano
 
Kipindi kile mlikuwa na common objectives kwa kuwa majority mlikuwa ni watoto toka vijijini, uchumi wenu ulifanana na hali ya kiuchumi ya taifa ilikuwa inawafanya hata matajiri waonekane maskini hivyo mlipmbana kama wamoja.

Rejao wewe siku hizi ni matawi ya juu, uchumi wako uko juu, tayari ulisha mwandaa mwanao kufikiria kibepari kwani pesa unazo, na mwanao kwa ujinga uliomlisha na kuona yeye ana hela za kutosha, huwezi kumwondoa kwenye thinking hiyo.

Kinachofanyika, ni kwa wale majority ambao hali zetu bado ziko chini kuwalazimisha hata mwanao akubaliane na matakwa ya maskini, na akigoma, lazima kiboko achapwe kumlazi9misha kufikiria waliowengi maskini kazi ambayo wewe uliitelekeza kwa kumlea mwanao atambue pesa/nafasi uliyonayo imetokana na uwezo wako wakati ukweli siyo
Comment yako imenigusa sana! but kama ni kugoma amueni mnagoma kweli..na wote muwe na lengo moja! Pia migomo isiwe ya kila mara.
soma hii comment hapa chini

Wanafunzi wa UDSM wamegoma tena! Hivi wana soma saa ngapi? Kazi kujadili watagoma lini. Kwa kweli sifurahii migomo. Kwa wanaokumbuka Mwalimu alikuwa anawadhibiti vikali viongozi wa migomo. Wengine walikuwa wapelekwa na mbu sehemu fulani pale Oyster Bay na kuminywa gololi zao! Ubaya wengine ni watoto wa wakulima, wazazi wao wamejipiga wapate visenti ili watoto wao wawe na maisha bora kuliko wao.


Hatimaye, mtoto anafukuzwa chuo hata kazi ya maana hawwezi kupata maana kawa black sheep, yule mtoto wa mkubwa aliyeshiriki anapelekwa kusoma kwingine au nje ya nchi. Hebu mfikirie Kwanza jamani! Hakuna baraza la viongozi wa wanafunzi? Fanyeni Dialogue. Hakuna faida kwa wote Chuo kikifungwa. Nilishapambana na hiyo teargas na mafarasi wa FFU Dar si mchezo! Kuna hatari ya mtu kupoteza maisha yake.
 
wewe umesoma wapi ??? SOLIDARITY FOREVER @UDSM, mara zote wanafunzi wa udsm wanamshikamano na umoja na ndio maana hawakubali kuendelea na masomo while wenzao wako mahabusu...tuliosoma udsm hatushangai hili...big up sana...kama kugoma mligoma wote lakini kwa bahati mbaya wamekamatwa wachache sasa kwanini nyie muendelee kusoma ile hali wanzenu wapo mahabusu.....!

siungi mkono hili la Alshabab, but naunga mkono mgomo kuendelea kushinikiza waachiwe huru wote walofungwa.....


Utoto unashida sana. Jamani tuwafunze hawa wenetu na wadogo zetu. Hawajui walifanyalo
 
Watu wana akili FINYU...AL-SHABAB ni neno la kiarabu linalomaanisha Kijana shupavu....kuna tatizo mtu kujiita kijana shupavu.....ila sishangai sana hizi ni zile akili za KUSHIKIWA...!!!
 
Kijana shupavu wa kuua wasio na hatia??? Huo ndo ushupavu??? Kijana shupavu kuvamia mall Kenya na kuua watoto?? Huo ndo ushupavu?? Kijana shupavu wa kuuwa watu wa dini nyingine kana kwamba mungu wake hawezi kujitetea?? Nadhani ni aibu kujiita kijana shupavu ktk mazingira hayo!
 
Yupo wapi alshabab,?
Baada ya wanaharakati kuwekwa ndani, wamejitokeza vijana wengine wenye nguvu na utashi kuongoza maandamano hayo, kikosi hicho kinaongozwa na kijana machachari ambaye amejipa jina la ALSHABAAB kijana huyo amesikika akisema "maboko na mkandala kama mnataka kufukuza wanafunzi, mnifukuze mimi kwanza.

mimi Alshabaab niko tiyari kufukuzwa, niko tiyari kufungwa Ikibidi kufa nikiwatetea wenzangu walioko maabusu" kijana huyo amesikika akisema. Kijana huyo inasemekana anatafutwa na polisi kwa kujiita Alshabaab. Hadi sasa hali ni mbaya, polisi walivamia na kutawanya wanafunzi, maeneo yote ya chakula yamefungwa na masomo hakuna.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom