Maandamano UDSM sasa yaongozwa na 'AL-SHABAAB'?

Leonard Robert

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
11,059
7,189
Baada ya wanaharakati kuwekwa ndani, wamejitokeza vijana wengine wenye nguvu na utashi kuongoza maandamano hayo, kikosi hicho kinaongozwa na kijana machachari ambaye amejipa jina la ALSHABAAB kijana huyo amesikika akisema "maboko na mkandala kama mnataka kufukuza wanafunzi, mnifukuze mimi kwanza.

mimi Alshabaab niko tiyari kufukuzwa, niko tiyari kufungwa Ikibidi kufa nikiwatetea wenzangu walioko maabusu" kijana huyo amesikika akisema. Kijana huyo inasemekana anatafutwa na polisi kwa kujiita Alshabaab. Hadi sasa hali ni mbaya, polisi walivamia na kutawanya wanafunzi, maeneo yote ya chakula yamefungwa na masomo hakuna.
 
Baada ya wanaharakati kuwekwa ndani, wamejitokeza vijana wengine wenye nguvu na utashi kuongoza maandamano hayo, kikosi hicho kinaongozwa na kijana machachari ambaye amejipa jina la ALSHABAAB kijana huyo amesikika akisema "maboko na mkandala kama mnataka kufukuza wanafunzi, mnifukuze mimi kwanza, mimi Alshabaab niko tiyari kufukuzwa, niko tiyari kufungwa kibidi kufa nikiwatetea wenzangu walioko maabusu" kijana huyo amesikika akisema.kijana huyo inasemekana anatafutwa na polisi kwa kujiita Alshabaab.hadi sasa hali ni mbaya, polisi walivamia na kutawanya wanafunzi, maeneo yote ya chakura yamefungwa na masomo hakuna.

bado wanadhan watamaliza matatizo kwa kukamata watu, kupiga mabomu na risasi?
 
Kwanza Mimi siwapendi Al-Shabab maana ni Magaidi hawana Ubinadamu kabisa hivyo hata mtu akijiita hivyo jua ni wale wale waliokunywa uji Wa Mgonjwa.
 
huyo anayejiita Alshabab, asubil kinachomfuatia atasimulia hadi wajuu zake..amekosa jna jngne la kujiita la watu wanaharakati?? Mbona meng sn na walikuwepo na bdo wapo...
 
Hivi kumbe niingia ndani ya eneo la chuo kikuu niko juu ya sheria ni kama bungeni au niliwaelewa wanafunzi wa UDSM vibaya kuwa waliokamatwa walikuwa ndani ya eneo la chuo? ukiwa ndani ya chuo hukamatwi?

Jana niliongea na baadhi ya wanafunzi wkiwa wametanda pale utawala wakaniambia wenzao wamekataliwa dhaman na wao wanavuruga masomo na shughuli zote za chuo ili utawala uishinikize mahakama kuwaachia wenzao kabla ya saa moja jioni ikishindikana leo asubuhi. Baada ya hapo nilikutana na afisa mmoja nikajaribu kudadisi akaniambia "kaka hapa toka Ijumaa uongozi wa chuo unahangaika kuwatoa waliokamatwa shida ni kwamba lazima ufuate utaratibu na mahakama haiingiliwi kwa asira au jazba za kundi fulani au itikadi ya mtu au chama au dini nk.

lakini jana jumatatu hakimu mkazi amekubali ombi la mwanasheria wa chuo la vijana kudhaminiwa na chuo na hivyo leo jumanne hati ya kuachiwa (release order) itatolewa ili kesho wanafunzi wetu wapelekwe mahakamani tayari kwa dhamana. Matumaini yangu kesho jumatano watatoka na taratibu nyingine za kisheria zitafuata wakiwa nnje".

Maswali yangu ni kuwa kwa nini wanaharakati wasipitishe bakuli kupata mwanasheria ili kama ni kuishurutisha mahakama iwe rahisi maana inaonekana hawauamini utawala wala viongozi wao yaani wabunge na serikali ya DARUSO?

Kama vipi maprofesa na uongozi wa chuo ufanye maamuzi magumu chuo kifungwe mpaka wanafunzi wote watakapopata mikopo wahitaji na wasiohitaji ndiyo chuo kifunguliwe.

Tupeane ushauri jamani
 
Mwaka huu polisi wana kazi. Mijarada itajaa mahakamani mara utasikia
1.Wamekiuka amri halali ya polisi
2.Wachochezi
3.Wamekusanyika visivyo halali
4.Manyara wamekamatwa na bendera za Chadema kinyume na sheria
5.Wameandamana wakitokea Mahakamani kinyume na sheria
6.
.
.
.
.
.
8613.Wachochezi hawataki nchi itawalike
 
Kama Syria wanalalamikiwa kwa kutumia nguvu dhidi ya raia hii ya Tz imekaaje?
 
Aaah ndugu leo kila wanayemhisi afisa usalama wanamdunda na kwa taarifa za uhakika toka eneo la tukio walimkamata askari kanzu na kumpa kichapo kuwa kwanini anawasikiliza akawaambia naye ni mwanafunzi lakini hakusikilizwa wakamlazimisha atoe simu ila katika harakati wakatokea askari na kipira wakipiga king'ora kila mmoja akatawanyika wakati wanausalama wengine wa chuo wakiwa wameshamuondoa afisa huyo mikononi mwa maalshabab hao.

Kwa sasa vijana wako chini ya mdegree wanahamasishana kuwa hawasomi bila wenzao wakati huohuo kumbi mpya za mihadhara lecture zinaendelea.
 
Utoto unashida sana. Jamani tuwafunze hawa wenetu na wadogo zetu. Hawajui walifanyalo
Huu ndo uwezo wako? unataka kuniambia wanafunzi wote wa UDSM ni wenetu na wadogo zetu? Ikitokea kesho na kesho kutwa Rejao unaenda kupiga kozi fulani pale utaingia kwenye kundi la wenetu na wadogo zetu?
 
Mimi natamani sana chama kingine kichukue nchi au yaliyotokea nchi nyingine yahamie hapa ili tuonje ladha nyingine ya utawala au maisha tusiambiwe tu itakuaje bali tuonje wenyewe radha halisi.
 
Busara nyingi zainahitajika kwenye mambo kama haya. tatizo viongozi wetu wamekosa hizo busara. Hatuna viongozi bora tuna bora viongozi.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom