Maandamano nchi nzima yatangazwa baada ya bunge kukubali muswada wa sheria wa marekebisho ya katiba

Jukwaa la Katiba latangaza uamuzi mgumu

Jijini Dar es Salaam, Jukwaa la Katiba limetangaza maandamano makubwa yasiyokoma nchi nzima, kama hatua ya kupinga hatua hiyo ya serikali baada ya jitihada zao za kuishauri serikali kwa njia za mazungumzo kushindikana.

Akizungumza mara tu baada ya uamuzi wa serikali kuruhusu muswada huo kusomwa kwa mara ya pili huko Dodoma, mwenyekiti wa jukwaa hilo, Deus Kibamba, alisema kwa kuwa wabunge wa CCM wameamua kuwadharau Watanzania na kupuuzia mawazo yao, sasa taifa litashuhudia maandamano ambayo hayajapata kuwapo nchini.

“Sasa tutawaonyesha watawala wetu ya kuwa sisi Watanzania ndio wenye nchi. Tutaagiza maandamano kutoka kila kona ya nchi kuelekea Dar es Salaam, na tutakusanyika katika uwanja mkubwa ambapo tutakaa kwa siku zote hadi serikali itakapoamua kuondoa muswada huo bungeni,” alisema Kibamba.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa ni masikitiko makubwa na mshangao kwa wapenda amani kuona jinsi serikali na wabunge wa CCM wanavyoweza kuwadharau wananchi wake katika mambo mazito ya taifa.

Mapema juzi, jukwaa hilo liliitahadharisha serikali kuwa isiposikia kilio cha Watanzania, wataamua kuandamana nchi nzima bila kukoma na wakalitahadharisha jeshi la polisi na majeshi mengine, kukaa pembeni kwa sababu Watanzania wanalilia haki yao ambayo haiwezi kuzuiwa kwa wingi wa askari, silaha na mabomu

Source: Gazeti la Mwananchi

naamini hata askari watunga mkono, watakuwa wakimaliza malindo yao kama wajibu wao unavyowataka, watakuwa wanajumika pamoja
 
CCM ndio watanzania...CCM ni chama kilichopewa dhamana ya kuiongoza nchi na wananchi. Maoni wanayoyatoa ni ya watanzania wote walioiweka madarakani. Sioni sababu ya kikundi cha watu wachache ya kutaka kuyumbisha malengo mazuri ya chama tawala.
Muda mwingine ni vizuri ukawa unatoa uvivu wa kufikiria unaposema ccm ndo mawazo ya watanzania wote una hakika na hilo? kuna watanzania wangapi waliopiga kura na kuiweka ccm madarakani ukilinganisha na wasiopiga? ina maana hao walio wengi ambao ni karibu asilimia 70 wasiopiga kura siyo watz....ww vp mbona una narrow scope? think!! unaboa mi huwa spendi kutukana masaburi wee...!
 
Naombeni mnitumie nauli na mimi... nitakuja kuwapa shule kuhusu mchakato wa katiba na kinachoendelea.. Nitakuja kuwafundisha kuhusu upotoshwaji unaofanywa na hao wanaojiita wanaharakati.
Tukusanyike kwa wingi ili somo lieleweke kwa wengi tafadhali

rejao huhitaji kusafiri ili kudai katiba mpya, unachohitajika kukifanya ni wewe na sehemu yoyote ulipo kuunga mkono kama kweli una nia ya dhati kuepusha machafuko ya WANANCHI V/S CCM/. DSM wakishatangaza utaratibu, watatutangazia mikoani nasi tutangaza utaratibu wa kudai katiba hiyo.
 
Mkome na nyinyi kuendelea kuchagua wabunge wa CCM. Mnataka mvune msichopanda?
Lakini kwa hili ni bora tusubiri tena miaka mingine 50, kuliko kupata hii katiba ambayo CCM
wanataka kutuletea.

Believe me hata wakilazimisha CCM wakaileta kwa wananchi kwaajili ya kupigiwa kura, hata
kama King pin wa uchakachuaji Makame Lewis na Rajabu Kiravu watasimamia hawawezi kupata
two third ya votes. Itakuwa kama Kenya Ndizi (banana) na Chungwa (Orange).

Lakini pia Tanzanians we are doomed, kwasababu serikali ya CCM haina nia kabisa na Katiba
mpya, hiyo ndiyo amebaki njia yao tu, kutuletea katiba ambao wanafahamu fika kwamba
wananchi tutaikataa na NENO litatimia la kutokuwa na katiba mpya.
kaka usitutukane, wewe mwenyewe unajua mazingira ya uchaguzi yalivyo kuanzia Tume ya uchaguzi, Elimu duni ya uraia, hali ya Kampeni ilivyo, ufukara tulionao yote haya yanachangia CCM kupita kwa urahisi. Ni vigumu sana tena mno kukwepa viunzi hivi. tuombe radhi mkuu...

Hatupendi wapite ila mazingira haya yanaruhusu wapate ushindi kwa urahisi.
 
Naombeni mnitumie nauli na mimi... nitakuja kuwapa shule kuhusu mchakato wa katiba na kinachoendelea.. Nitakuja kuwafundisha kuhusu upotoshwaji unaofanywa na hao wanaojiita wanaharakati.
Tukusanyike kwa wingi ili somo lieleweke kwa wengi tafadhali

Wewe mjinga sana, imefika wakati inabidi ufunguke kuwa katiba ni ya wananchi kwanini wasishirikishwe, katiba ni mali ya wananchi cyo ya rais, bravo wanaharakati, bravo prof shivji, bravo tume ya majaji, bravo NSSR na CDM
 
Mkome na nyinyi kuendelea kuchagua wabunge wa CCM. Mnataka mvune msichopanda?
Lakini kwa hili ni bora tusubiri tena miaka mingine 50, kuliko kupata hii katiba ambayo CCM
wanataka kutuletea.

Believe me hata wakilazimisha CCM wakaileta kwa wananchi kwaajili ya kupigiwa kura, hata
kama King pin wa uchakachuaji Makame Lewis na Rajabu Kiravu watasimamia hawawezi kupata
two third ya votes. Itakuwa kama Kenya Ndizi (banana) na Chungwa (Orange).

Lakini pia Tanzanians we are doomed, kwasababu serikali ya CCM haina nia kabisa na Katiba
mpya, hiyo ndiyo amebaki njia yao tu, kutuletea katiba ambao wanafahamu fika kwamba
wananchi tutaikataa na NENO litatimia la kutokuwa na katiba mpya.

Nimekuelewa kwamba, watakuja na kura ya maoni ya NDIYO au HAPANA. Kwa kuwa wananchi wengi tutakataa mawazo ya CCM, tutaikataa katiba kwa kura nyingi na CCM watahitimisha kwa kusema watanzania HAWATAKI katiba mpya, wamepitisha ya zamani na ndo utakuwa mwisho wa harakati za katiba mpya kwa vigezo vy kura za hapana.

My note is that, ikiwa itakuwa hivyo, basi vita ya wenyewe kwa wenyewe, itakuwa imetangazwa rasimi na CCM.
 
Unafiki ni kitu kibaya sana na mwisho wake huwa ni aibu...pia uoga na nidhamu ya kinafiki ya kutii kila unachoagizwa pasipo kutumia akili yako ni ujuha. Yule anayekuagiza ufanye hivyo ni kama amekushikua akili yako na ana ku-twist vile apendavyo. Ipo siku wabunge wa ccm watajiona ujuha wao kwa kukubali kutumika kwao pasipo kutumia akili zao. Watambue kuwa bunge lilikuwepo hata wakati wa mkoloni, wao si wa kwanza na pia wataliacha-wasijione kuwa ndiyo wamefika kwa kuwa wabunge...ipo siku tu
 
Nilishangazwa sana jana na Mbunge wa GAMBO wa CUF ndugu Halfa Khalfan ( hata sipendi kumuuta mheshimiwa kwani ameshindwa kutuheshimu watz) baada ya kusema kuwa mswaada ukisha fika bungeni utapita hata kama wakitoka nje, hapo ndoo niliamini kuwa CUF na CCM lao moja maana kama hata mtu kaleta kitu kibovu ila kwakuwa kimefika bungeni basi kitapita duuuu ama kweli wabunge vilaza hawana alama.

MNAJUA WATU WENGI WALIMLAUMU YULE NDUGU JAIRO WAKATI ALIPOELEZEA KUHUSU WABUNGE LAKINI WATU WENGI WALIMJADILI MTU ZAIDI(JAILO) KULIKO ISSUES ZAKE. Sasa ndio haya tunayaona,NA BADO KUNA MENGI ZAIDI TUTAYAONA!
 
Tanzania ,Tanzania nchi yangu yenye maziwa na asali ,nakupenda sana,nawapenda wana nchi wenzangu,ila naumizwa na selikali yangu ambayo haingalii maslai ya Taifa lake na wananchi wake,tupo pamoja wakubwa katika maandamano
 
Naombeni mnitumie nauli na mimi... nitakuja kuwapa shule kuhusu mchakato wa katiba na kinachoendelea.. Nitakuja kuwafundisha kuhusu upotoshwaji unaofanywa na hao wanaojiita wanaharakati.
Tukusanyike kwa wingi ili somo lieleweke kwa wengi tafadhali

Nenda MOMBASA UKAOLEWE WEWE!
 
CCM ndio watanzania...CCM ni chama kilichopewa dhamana ya kuiongoza nchi na wananchi. Maoni wanayoyatoa ni ya watanzania wote walioiweka madarakani. Sioni sababu ya kikundi cha watu wachache ya kutaka kuyumbisha malengo mazuri ya chama tawala.

Du!!!
Kama zingepigwa kura na matokeo ya haki yangesema hayo.
Pia hata hao wachache ambao hawakuichagua ccm ni wananchi na ni muhimu kusikilizwa.

Mbona Zanzibar ni wachache wana haki sawa na watanganyika walio wengi?
 
My friend you cannot equate a party with people, and not CCM of all parties...so acha kujifariji na kujaribu kuzima the obvious...maandamano ndio silaha ya weyne nchi...viva Watanzania...I am in
Maandamano kwa Tanzania siyo njia sahihi ya kudai haki. Mara ngapi wananchi wameandamana? Je wamefanikiwa? wameishia tu kupata kipigo!
Think of another alternative but siyo hii ya kuandamana

utakua una shda na pesa ya sukari!
Nije kwako utanisaidia?

ELEWA KW SAUTI YA UMMA NI SAUTI YA MUNGU!i
Duh....mungu tena?? haya mama..Inshallah

Muda mwingine ni vizuri ukawa unatoa uvivu wa kufikiria unaposema ccm ndo mawazo ya watanzania wote una hakika na hilo? kuna watanzania wangapi waliopiga kura na kuiweka ccm madarakani ukilinganisha na wasiopiga? ina maana hao walio wengi ambao ni karibu asilimia 70 wasiopiga kura siyo watz....ww vp mbona una narrow scope? think!! unaboa mi huwa spendi kutukana masaburi wee...!
Kila mtanzania anahaki ya kupiga kura...tunaangalia majority rule..kama wameichezea haki yao, let them suffer consequences
rejao huhitaji kusafiri ili kudai katiba mpya, unachohitajika kukifanya ni wewe na sehemu yoyote ulipo kuunga mkono kama kweli una nia ya dhati kuepusha machafuko ya WANANCHI V/S CCM/. DSM wakishatangaza utaratibu, watatutangazia mikoani nasi tutangaza utaratibu wa kudai katiba hiyo.
Haaa...Pole..dar kila mtu yupo busy na kutafuta maisha!
Wewe mjinga sana, imefika wakati inabidi ufunguke kuwa katiba ni ya wananchi kwanini wasishirikishwe, katiba ni mali ya wananchi cyo ya rais, bravo wanaharakati, bravo prof shivji, bravo tume ya majaji, bravo NSSR na CDM
NSSR hii ndio nini?
 
haya mambo yanafanya nchi hii isitawalike kabisa - yaani watu wameshajua haki zao basi matatizo matupu --- hii kazi ya kuongoza sasa inakuwa ngumu mno -- yaani kila kona ni moto mtupu -- wanafunzi moto, wamachinga moto, wanasiasa moto, wanaharakati moto, wabunge wa upinzani moto - kina mama niliowategea miaka yote nao moto laaahhh....... sasa nikimbilie wapi mimi CCM? mashambulizi kina kona? nafwaaaa........
 
Naombeni mnitumie nauli na mimi... nitakuja kuwapa shule kuhusu mchakato wa katiba na kinachoendelea.. Nitakuja kuwafundisha kuhusu upotoshwaji unaofanywa na hao wanaojiita wanaharakati.
Tukusanyike kwa wingi ili somo lieleweke kwa wengi tafadhali

Yaani upupu wote unaojitahidi kuutoa hapa JF magamba hawakulipi? Sikutegemea uombe nauli.
 
Kama maandamano kweli yatanza, basi wote tuimbe wimbo huu: Wewe ni unani Jamaaaa, mimi Mtanzania,Watoto wananitegemea,ndugu wananitegemea, mimi ninani jamii.*2Mimi ni Mtanzania, Taifa linanitegemea, matataifa yanaminitegemea*2 Ninyi munani Jama,sisi ni Watanzania. kisha Solidarity forever. Amani na mshikamano msingi wa katiba na demokrasia ya kweli kwa Tanzania tuipendayo.Tanznaia HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom