Maandamano nchi nzima yatangazwa baada ya bunge kukubali muswada wa sheria wa marekebisho ya katiba

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
646
1,174
Jukwaa la Katiba latangaza uamuzi mgumu

Jijini Dar es Salaam, Jukwaa la Katiba limetangaza maandamano makubwa yasiyokoma nchi nzima, kama hatua ya kupinga hatua hiyo ya serikali baada ya jitihada zao za kuishauri serikali kwa njia za mazungumzo kushindikana.

Akizungumza mara tu baada ya uamuzi wa serikali kuruhusu muswada huo kusomwa kwa mara ya pili huko Dodoma, mwenyekiti wa jukwaa hilo, Deus Kibamba, alisema kwa kuwa wabunge wa CCM wameamua kuwadharau Watanzania na kupuuzia mawazo yao, sasa taifa litashuhudia maandamano ambayo hayajapata kuwapo nchini.

“Sasa tutawaonyesha watawala wetu ya kuwa sisi Watanzania ndio wenye nchi. Tutaagiza maandamano kutoka kila kona ya nchi kuelekea Dar es Salaam, na tutakusanyika katika uwanja mkubwa ambapo tutakaa kwa siku zote hadi serikali itakapoamua kuondoa muswada huo bungeni,” alisema Kibamba.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa ni masikitiko makubwa na mshangao kwa wapenda amani kuona jinsi serikali na wabunge wa CCM wanavyoweza kuwadharau wananchi wake katika mambo mazito ya taifa.

Mapema juzi, jukwaa hilo liliitahadharisha serikali kuwa isiposikia kilio cha Watanzania, wataamua kuandamana nchi nzima bila kukoma na wakalitahadharisha jeshi la polisi na majeshi mengine, kukaa pembeni kwa sababu Watanzania wanalilia haki yao ambayo haiwezi kuzuiwa kwa wingi wa askari, silaha na mabomu

Source: Gazeti la Mwananchi
 
naungan mkono hoja! watupe utaratibu na sisi wa arusha tutaanzia wap na kuishia wap! tupo tayari kwa lolote...
 
Naombeni mnitumie nauli na mimi... nitakuja kuwapa shule kuhusu mchakato wa katiba na kinachoendelea.. Nitakuja kuwafundisha kuhusu upotoshwaji unaofanywa na hao wanaojiita wanaharakati.
Tukusanyike kwa wingi ili somo lieleweke kwa wengi tafadhali
 
Nadhani imefikia wakati tusimame kama watanzania. Sioni kunatatizo gani bunge la CCM kukubaliana na Kile wananchi wanachikitaka. Ifikie wakati tufahamu katiba ni Mali ya watanzania na si kikundi cha wajinga wachache. Count me in the demonstration rally
 
wakuu kuna kitu kinanishangaza'kama katiba ni mali ya watanzania kwa nini ccm iingize sana mamikono yao???kwa nini wasiwape watanzania nafasi ya kufanya watakayo''maandamano lazima mpaka yule mkweree mwenye ngoma aone nyotanyota?
 
Nadhani imefikia wakati tusimame kama watanzania. Sioni kunatatizo gani bunge la CCM kukubaliana na Kile wananchi wanachikitaka. Ifikie wakati tufahamu katiba ni Mali ya watanzania na si kikundi cha wajinga wachache. Count me in demonstration

Nilishangazwa sana jana na Mbunge wa GAMBO wa CUF ndugu Halfa Khalfan ( hata sipendi kumuuta mheshimiwa kwani ameshindwa kutuheshimu watz) baada ya kusema kuwa mswaada ukisha fika bungeni utapita hata kama wakitoka nje, hapo ndoo niliamini kuwa CUF na CCM lao moja maana kama hata mtu kaleta kitu kibovu ila kwakuwa kimefika bungeni basi kitapita duuuu ama kweli wabunge vilaza hawana alama.
 
Naombeni mnitumie nauli na mimi... nitakuja kuwapa shule kuhusu mchakato wa katiba na kinachoendelea.. Nitakuja kuwafundisha kuhusu upotoshwaji unaofanywa na hao wanaojiita wanaharakati.
Tukusanyike kwa wingi ili somo lieleweke kwa wengi tafadhali
Acha na mimi nikaombe lifti kwa Shibuda
 
Kibamba acha kuwadanganya watanzania, wewe ni kati ya Wa watu wachache mnaonufaika na mchakato wa katiba! Nani asiyejua kwamba mchakato Wa katiba ukikamilika ndo kifo cha jukwaa lako!
 
wakuu kuna kitu kinanishangaza'kama katiba ni mali ya watanzania kwa nini ccm iingize sana mamikono yao???kwa nini wasiwape watanzania nafasi ya kufanya watakayo''maandamano lazima mpaka yule mkweree mwenye ngoma aone nyotanyota?
CCM ndio watanzania...CCM ni chama kilichopewa dhamana ya kuiongoza nchi na wananchi. Maoni wanayoyatoa ni ya watanzania wote walioiweka madarakani. Sioni sababu ya kikundi cha watu wachache ya kutaka kuyumbisha malengo mazuri ya chama tawala.
 
Naombeni mnitumie nauli na mimi... nitakuja kuwapa shule kuhusu mchakato wa katiba na kinachoendelea.. Nitakuja kuwafundisha kuhusu upotoshwaji unaofanywa na hao wanaojiita wanaharakati.
Tukusanyike kwa wingi ili somo lieleweke kwa wengi tafadhali
We mwenyewe huelewi halafu uelimishe wengine itawezekanaje hii. Rejeo ungekuwa unaelewa ungetoa elimu ya kutosha sana hapa JF kwanza hata ktk Uzi huuu huu kama unaogapa kuanzisha wa kwako
 
Kwa situation ilipofikia sasa hiki ndicho kinachotakiwa!
Juzi niliona mchango wako ulikuwa unabadilishana mawazo na Director1 nikakukubali. Actually najua hujakurupuka kusema kilichobaki ni maandamano ili kuishinikiza serikali itambue udhaifu wa muswaada huo.
 
Naombeni mnitumie nauli na mimi... nitakuja kuwapa shule kuhusu mchakato wa katiba na kinachoendelea.. Nitakuja kuwafundisha kuhusu upotoshwaji unaofanywa na hao wanaojiita wanaharakati.
Tukusanyike kwa wingi ili somo lieleweke kwa wengi tafadhali

Tatizo la kuzoea kutumiwa usafiri kwenda mikutanoni (ili mkutano uonekane umejaza) limekuharibu mkuu, ona sasa unaomba nauli hadi kwenye sehemu ambazo kimsingi ungepaswa kuchangia kwa nauli yako mwenyewe na mawazo yenye kujenga!!
 
Yeah, mpango mzima! Tunaanza lini?

Na katika hili mimi ntamnyonya mtu kamasi endapo atajitokeza mjingamjinga fulani akatuletea habazi za vibali vya mandamano.
Maanake hawakawii kusema tunavuja amani, watatuambia hiyo amani ipo kwa ajili ya nani.
She....nzi.. type.
 
Pia nimesikitika sana Spika anaposema kuwa hii si katiba bali ni sheria tuu ya mwanzo ya kuwezesha kuunda kamati ya kukusanya maoni, jamani hivi nini maana ya sheria. Japo sijasoma sheria ila najua sheria yoyote inatungwa ili ifuate kukamilisha kitu fulani na endapo mtu ataenda tofauti na ilivyo maana atakuwa anaenda tofauti na hataruhusiwa.

Sasa kama spika mwenyewe hajui nini maana ya huu mswaada na utatumika vipi ina maanisha amepungukiwa sifa za kuwa rais, kama rais ataamua kwachagua watu wake ili kuendesha huu utaratibu maana yake hakuna atakayempinga kwa kuwa rais atafuata sheria iliyotungwa na bunge na hapo ndoo tutaona kuwa tatizo la katiba mbovu tutakayopata itatokana na hii sheria ambayo SPIKA NAMWENYEKITI WA BUNGE NDG SIMBACHAWENE wanaona kuwa ni kitu kidogo,

SISI watanzania siyo wa kudanganywa kiasi hicho tunajua sana kile kinachofanyika huko bungeni ni kwa ,masrahi ya nani...
 
Back
Top Bottom