Maandamano makubwa

si nilisema jukwaa la katiba wametangaza rasi kuwa endapo km serikali ya ccm itasoma mswada kwa mara ya 2 wataongoza maandamano ya nchi nzima.
Naisikitikia nchi yangu Tanzania! Itapotea kwenye ramani ya Dunia na kuzaliwa nchi 2 yaani nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar
 
Binafsi nasubiri nione hayo maandamano na ntashiriki kwa nafasi yangu.
Mi naona tunaongeza chumvi au tunawa-overestimate wabongo!
Hebu kila mtu atoke nje mtaani kwake aangalie watu wake, kweli inaonekana ni watu wenye uwezo wa kuhoji kiasi hcho??
Sijui mtaani kwako ila kwangu naona sura za watu wanaowaza wale nini leo na kesho basi, tena suala lenyewe katiba!
Tutachanganya na picha ya Mbeya!
Mbeya serikali iligusa chakula cha watu ndio maana vile.
Pia hata tukijipa matumaini kuwa maeneo kama mbeya watatoa mskumo kwenye maandamano hayo bado Tz nzima sio mbeya tu,
mbaya zaidi hata hao watakaojitokeza kwenye hayo maandamano watakatishwa tamaa kwa kuonekana ni wakorofi na kuwa badala ya kufanya kazi na kujipatia maendeleo wao wanakazania maandamano amb ayo hayana faida kwao.
Sitaki kukatisha tamaa ndio maana nkasema ntashiriki kwa kadiri ya ari yangu yote, ila ni muhimu kujadili kwa kuzingatia ukweli wa watu wetu.
Tuupitie kwa umakini mkubwa zaidi muamko wa Watanzania katika siasa za mikiki
 
Dogo umekuja bila tafakuri.. Hadi lunyungu nae unadhani ni ccm. Nakushauri uwe unatumua busara kujenga hoja, wengi walikuja hivyo na matusi na kudandia treni kwambele
lynyungu is never magamba

hahahahahaha
mzazi una kazi sana na hao "vijana" wako!
 
haya yatakuwa ni maandano ya tatu kwa nchi nzima kuongelewa jamvini..ngoja tuone..

Tatizo watu wakikaa kwenye keyboard wanapanga mipango vizuri, lakini siku ya maandamano badala ya kushiriki wanakaa tena kwenye keyboard kufuatilia nini kinatokea!
 
jounegwalu kutokana na ugumu wa maisha na ufisadi mkubwa unaofanywa na serikali ya ccm, na kwa msaada wa chama cha chadema kutoa elimu ya uraia karibu kila pande ya Tanzania sasa Watanzania wa sasa wanauelewa na wanajua haki zao, na pale zinapopindishwa huwa wanazidai.
 
ole wake kova aje kama juz kati eti alshabaaaaab watalipua!!!
 
Kwa nini hasa hii serikali inataka kufanya kiini macho kwenye suala la katiba jamani. Katiba ya nchi haihitaji ushabiki wa kisiasa maana kila chama kina katina yake ambayo kikipenda kuichezea kinavyotaka inawezekana. Lakini katiba ya nchi iachwe iwe ya wananchi wote
1. WANAHOFU YA KUSTAKIWA KUFUNGWA NA KUFILISIWA MALI WALIZOWAIBIA WATANZANIA. 2. wanataka waendeleze ufisadi na unyanyasaji wa Watanzania.
 
Kuna kila dalili ya kutokea maandamano makubwa na vurugu za kutosha kama kesho mswada utapelekwa bungeni na kusomwa kwa mara ya pili na hatimaye kupitishwa kwa unafiki na wabunge [ccm]. KAMA SERIKALI YA CCM KM INA MASIKIO ISIKILIZE MATAKWA YA WANANCHI.

Dalili zinaashiria kwamba Katiba mpya itakuwa ni kiini macho tu ambayo Watanzania wengi hatutaikubali kwani itaandikwa katika mazingira ambayo yatahakikisha Magamba wanatawala Tanzania milele, kama ambavyo mmoja wa mafisadi wa Magamba alivyowahi kutamka miezi michache iliyopita.
 
jounegwalu kutokana na ugumu wa maisha na ufisadi mkubwa unaofanywa na serikali ya ccm, na kwa msaada wa chama cha chadema kutoa elimu ya uraia karibu kila pande ya Tanzania sasa Watanzania wa sasa wanauelewa na wanajua haki zao, na pale zinapopindishwa huwa wanazidai.

Yah naelewa sana, na pia wengine tunafanya kazi ya ziada huku mtaani kuwaelimisha watu.
Nimekuwepo kwenye harakati kwa kiasi changu, na mara ya mwisho nilikuwepo pale NMC hadi kinanuka pale!
Ndio maana nkasema mi ntacheza nafasi yangu kama raia huru ninayejitambua, lakini pia Angel hawa ndugu zetu wakina Kibamba wamefikia wapi kwenye maandalizi, ukitoa hayo matangazo ya kwenye tv tu?
Maandamano nchi nzima ni kitu kikubwa jamani!
 
si nilisema jukwaa la katiba wametangaza rasi kuwa endapo km serikali ya ccm itasoma mswada kwa mara ya 2 wataongoza maandamano ya nchi nzima. HAYA KM CCM HAWASIKII WAENDELEE KUJIDAI VICHWA NGUMU

Serikali taahira ndivyo ilivyo Mkuu, haisikii la jini wala la shetani wao husonga mbele bila ya kuyasikiliza na kuyafanyia kazi mawazo ya Watanzania walio wengi, lakini naamini kabisa si muda mrefu ujao watajuta kwa maamuzi yao ya kukurupuka maana kuna uwezekano wa kuzuka machafuko makubwa katika sehemu nyingi nchini na hata watu wengi kupoteza maisha yao. Hili kama likitokea wa kulaumiwa si mwingine bali ni msanii Kikwete na chama chake cha Magamba.
 
Yah naelewa sana, na pia wengine tunafanya kazi ya ziada huku mtaani kuwaelimisha watu. Nimekuwepo kwenye harakati kwa kiasi changu, na mara ya mwisho nilikuwepo pale NMC hadi kinanuka pale! Ndio maana nkasema mi ntacheza nafasi yangu kama raia huru ninayejitambua, lakini pia Angel hawa ndugu zetu wakina Kibamba wamefikia wapi kwenye maandalizi, ukitoa hayo matangazo ya kwenye tv tu? Maandamano nchi nzima ni kitu kikubwa jamani!
JIPE MOYO USIKATE TAMAA!i
 
ikiwezekana chadema waongoze na kuratibu hayo maandamano ili waongeze nguvu... hakina ukombozi umefika...
Acha ushamba what is chadema? Sisi tutaandamana kama wenyenchi na si vinginevyo........!
 
mswada ukipita naenda kujipiga moto ikulu,.kama kuna mwanaharakati yoyote yupo tayari kumtunza mke wangu na mtoto mmoja anipm

Mkubwa! Itabidi tuwe wote! Nami nasema km kuna mtu yuko tayari kukirm family yangu ya mke na watoto wanne aniPM bila ya kusita. Acha nijitowe mhanga na mshikaji.
 
na ikitokea yakatokea,itakuwa mbaya sana kwa serekali coz na wengine wenye hamu ya serekali kuondoka wanaweza kutumia mwanya huo..busara itumike tu kwenye hili

Ni kweli kwa mara ya kwanza Serakali ya jamhuri ya Muungano ya Tanzania itabidi idhibitishe maana halisi ya BUSARA tofauti na UBABE!

Kuna kila dalili ya kutokea maandamano makubwa na vurugu za kutosha kama kesho mswada utapelekwa bungeni na kusomwa kwa mara ya pili na hatimaye kupitishwa kwa unafiki na wabunge [ccm]. KAMA SERIKALI YA CCM KM INA MASIKIO ISIKILIZE MATAKWA YA WANANCHI.

Hakuna shaka, Uwezekano mkubwa ni kuwa Serekali Itafanya hivyo kwani..NI KWELI! Haiko tayari kuona kitakachotoea kama isipokuwa na busara!

Tunaelekea kwenye utamu, waliokuwa wanajadili hapo Blue Perl Hotel leo wametoa tamko lao. Tuwasubiri hao wapumbavu tuone watafanya nini hapo kesho kisha tuwe pamoja kwenda mbele na kudai haki zetu kwa nguvu zote.

Haki itadaiwa Kwa NGUVU ZOTE!! Natarajia kuwa UONGOZI stahili, Umeliona hilo na itakuwa upande wa wa Haki kwani vinginevyo, Haitakuwa Ustawi wa jamii ila ... udhoofishaji wa jamii kwani vurugu ambazo sasa zinaonekana kuzooleka ..zitatawala!! Na hakuna aliyetaari kuona TAMASHA kama lile la Mbeya na Mkesha wa NMC Arusha ..Vikitokea ..kwenye MJI KAMA DSM ... na kuungwa mkono ...mikoni ..HIVYO! Binafsi sioni kwanini Serekali ..iendelee kuogelea kuulekea mkondo wa maji yanakotoka hata kama ina misuli ya kufanya hivyo!! Yes No need at this time to go counter current!!

Bila shaka awike asiwike patakucha tu! Ngoja pakuche!!

Serekali yetu tukufu iliyoasisiwa Kusimamia na kutekeleza Uasili halisi wa mwanadamu kama utu huru, ubinadamu huru, umeyasikia hataya!! They just waiting PAKUCHE!! Whatever it means ... Utu + Ubinadamu kwa Mtanzania = Uzalendo na Utaifa. Jambo ambalo nategemea kwa fikra na moyo wangu kuwa Litaingia na kutawala Uongozi mtukufu wa Taifa hili ...Ili Kufikia MACHWEO ... Mambo yawe yamenyooka na kutupeleka salama kwenye sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Utu na Ubinaadamu wa taifa hili!
 
Mkuu unafiki umeanza lini ? Chadema hawana haja ya kuandamana ili wakubalike au wapende chart .Katiba ni ya kila mmoja wetu si Chama wala nini taasisi za dini mkuu .Wewe ingia baranarani kwa jina la Tanzania iacheni Chadema kwa hili .

yaaah, ni kweli ndugu chadema si ya hivyo.
 
hahahahahaha
mzazi una kazi sana na hao "vijana" wako!
Kaka vijana wananitoa povu hawa. Hawafanyi pembuzi bali wapo kama ngedere ni kurukaruka tu

tuna kazi sana kwani twajua tutakacho ila namna ya kupata inaletasintofahamu kabisa. Some boys think everything is political-related And forget katiba ni human right issue
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom