Malaria Sugu
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 2,653
- 264
Jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislam, JUMIKI, imeandaa maandamo ya amani ya kupinga rasimu ya muswaada wa katiba ya Muungano.
Maandamano hayo yanayotegemea kufanyika kesho baada ya swalah ya Ijumaa yataanzia msikiti wa Ijumaa malindi na kumalizikia kwenye viwanja vya Lumumba.
Hadi tunafika kutoa taarifa hii kibali bado hakijapatikana, lakini waandalizi wamesema wapo kwenye subira na hawaoni sababu ya Polisi kuwanyima kibali cha kufanyia maandamano hayo ya amani