Maandamano makubwa ya Madaktari yaja (wiki ijayo)

Chadema watakuwepo kwenye hayo maandamano.
Ritz...sasa tutapendekeza hao chadema wakuteue msemaji wao ili usiendelee kuwa mpotoshaji wao...hoja inayojadiliwa ni maandamano ya madaktari....sasa ya chadema yanaingiaje hapo?
 
Point yangu mimi kama kweli wao(Madaktari) ni waelimika watafanya maamuzi sahihi, kwanza wajiulize tu ni kwanini baadhi ya viongozi walioko nyuma ya hilo saga lao majuzi walijiapiza kuwa piga ua galagaza hawataitikia wito wa Polisi lkn jana wakaitikia kwa kujisalimisha wenyewe,akili kichwani mwao.
 
Chadema watakuwepo kwenye hayo maandamano.

mkuu umaarufu hautafutwi kwa kuonyesha upeo mkubwa wa ujinga.Hakuna aliyekatazwa kwenda kwenye maandamano,
1.Polisi hupewa taarifa(KISHERIA) ili kulinda waandamanaji
wasilete fujo na vivyo hivyo waandamanaji wasiingiliwe
na watu wengine...Lakini kwa muda mrefu imekuwa
ikichukuliwa kuwa "WANATOA KIBALI"

2.Mtu yeyote anaweza kuwa katika maandamano kwa
kufuata tu utaratibu wa waandamanaji,(katika hili uwe na
kitambaa cheupe kama si daktari na koti jeupe ukiwa
daktari)

3. Ushabiki wa vyama, ujinga wa kuongea bila kufanya
uchunguzi,hausaidii.

4. Unaweza kuwa unafanya kazi yako kwa bidii sana
ukidhani uko sahihi, na kuwa unakisaidia "hicho chama"
lakini unazidi kukididimiza kwa "mawazo mazuri" lakini
njia mbaya za utendaji.

5. Naamini kuwa katika jumuiya hii ya madaktari au kwa
ujumla wao 1500(madaktari wafanyao kazi ktk hospitali
za serikali nchi nzima) kuamua kutoweka itikadi zao za
kivyama na kuweka kipaumbele cha taaluma! Kwani ktk
idadi hii kuna madaktari wengi wa kila itikadi za vyama,
dini, kabila n.k.
 
Mkirua, Kwa hiyo wewe ndio una haki ya kuisema CCM, CUF, NCCR Mageuzi, TLP, utakavyo halafu utaki Chadema isemwe vibaya na unataka kuwafunga watu mdomo wasiseme chochote usichokipenda kuhusu Chadema...hivi hunajua maana ya forum? JF sio mali ya Chadema usiwapangie watu vitu vya kuandika kama post zangu zinakuchukiza zipotezee.
Tatizo sio kuchukizwa na post ila upotoshaji ulio kwenye hoja unayoisimamia........nitaendelea kukupinga hadi utakapothibitisha unayotaka kuwaaminisha watu hapa...CHADEMA wamesema hawahusiki....wewe kwanini unalazimisha??

source ya taarifa zako ni ipi au kwakuwa pro CHADEMA wengi hapa wanasupport kwahiyo wewe unataka kuaminisha watu kuwa hiyo ni agenda ya chadema?? Ndio maana mlimng'oa daktari wa watu meno bure mkimlazimisha aseme kama CHADEMA wanahusika??

Kwamba najua maana ya forum naijua vizuri sana ila sidhani kama forum ni sehemu ya kupotoshana kwa personal interest...nitajibu chochote utakachoandika na kukutaka utoe uthibitisho usinitishe eti nipotezee...once ukipost utajibiwa...
 
UN wana mambo ya msingi wameishaambia hatuna uwezo wa kuingilia mambo ya ndani ya nchi.

hawataki kuingilia kwa sababu hakuna faida watakayoipata mbona kwingineko hupenda kuingilia. labda waseme tu kuwa jambo hilo halijawa zito kwa wao kuliingilia lakini swala la ndani ya nchi ni uongo.
 
mkuu umaarufu hautafutwi kwa kuonyesha upeo mkubwa wa ujinga.Hakuna aliyekatazwa kwenda kwenye maandamano,
1.Polisi hupewa taarifa(KISHERIA) ili kulinda waandamanaji
wasilete fujo na vivyo hivyo waandamanaji wasiingiliwe
na watu wengine...Lakini kwa muda mrefu imekuwa
ikichukuliwa kuwa "WANATOA KIBALI"

2.Mtu yeyote anaweza kuwa katika maandamano kwa
kufuata tu utaratibu wa waandamanaji,(katika hili uwe na
kitambaa cheupe kama si daktari na koti jeupe ukiwa
daktari)

3. Ushabiki wa vyama, ujinga wa kuongea bila kufanya
uchunguzi,hausaidii.

4. Unaweza kuwa unafanya kazi yako kwa bidii sana
ukidhani uko sahihi, na kuwa unakisaidia "hicho chama"
lakini unazidi kukididimiza kwa "mawazo mazuri" lakini
njia mbaya za utendaji.

5. Naamini kuwa katika jumuiya hii ya madaktari au kwa
ujumla wao 1500(madaktari wafanyao kazi ktk hospitali
za serikali nchi nzima) kuamua kutoweka itikadi zao za
kivyama na kuweka kipaumbele cha taaluma! Kwani ktk
idadi hii kuna madaktari wengi wa kila itikadi za vyama,
dini, kabila n.k.

Kama wewe unaendika hii post ndio kiongozi wa madaktari basi kazi mnayo, mie nitafute umaarufu wa nini hunijui sikujui na wala siitaji kujuana na wewe hizo kauli zako za majigambo zinazidi kukupoteza...nakutakia maandamano mema.
Kutofautiana misimamo basi nimekuwa mjinga haya tuone nyie waelevu watu wenye akili nyingi kuzidi watu wote duniani kama mtafanikiwa.
 
Mimi nasubiri nione,zao la wafaulu mitihani kwa kutumia nyenzo naamini ndo watakaoandamana kesho...waliwaponza Ma'interns wakafutiwa usajili badala ya kuwapigania juzi Chitega sijui Chi' nini akautangazia Uma kuwa eti wamewaachia Viongozi wao(wa ma'interns) washughulikie issue hiyo wakati wao wanendelea kula bata na leseni zao,period!
watu mnaotumiwa ni hatari sana
 
I dont support the doctors!

wauaji wakubwa hawa, wanaringia taaluma zao, wamejaa majivuno, wanajiona bora kuliko binadamu wengine wote. hakika hawa wanahitaji kutubu!

mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!

Ms Judith,

Bora na wewe dada yangu umesema mie nimeambiwa mjinga natafuta maarufu sijui umaarufu gani wakati hata hatuaji.
 
Last edited by a moderator:
Ms Judith,

Bora na wewe dada yangu umesema mie nimeambiwa mjinga natafuta maarufu sijui umaarufu gani wakati hata hatuaji.

mpendwa Ritz,

Kweli kuna madai ya maana na madai ya kijinga. nathubutu kusema kuwa hawa madaktari wana madai ya kijinga!. hawa wamejaa kiburi wakijidanganya kuwa taaluma yao iko juu ya nyingine.

Huu ni ujinga na upumbavu. taaluma zote ni sawa na kama mie ndiye nigekuwa na maamuzi ya mwisho, ningeishawafundisha adabu siku nyingi sana.

Kwa kweli nakereka sana na katabia kao haka ka kijinga ka kuwatesa wananchi wenzao pasi na sababu yoyote ya kueleweka. natamani niwe rais wa tz hata kwa dakika moja tu, niwashikishe adabu!

Namtakia kila la heri rais kikwete kwa hatua anazochukua

Mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!
 
mpendwa Ritz,

kweli kuna madai ya maana na madai ya kijinga. nathubutu kusema kuwa hawa madaktari wana madai ya kijinga!. hawa wamejaa kiburi wakijidanganya kuwa taaluma yao iko juu ya nyingine. huu ni ujinga na upumbavu. taaluma zote ni sawa na kama mie ndiye nigekuwa na maamuzi ya mwisho, ningeishawafundisha adabu siku nyingi sana. kwa kweli nakereka sana na katabia kao haka ka kijinga ka kuwatesa wananchi wenzao pasi na sababu yoyote ya kueleweka. natamani niwe rais wa tz hata kwa dakika moja tu, niwashikishe adabu!

namtakia kila la heri rais kikwete kwa hatua anazochukua

mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!

Ni kweli unachosema dada yangu hawa madaktari wetu kwanza ni wabinafsi sana ata ukingalia madai yao 95% ni maslahi yao binafsi na 5% ndio wagonjwa wangejaribu kutumia njia ingine kudai maslahi yao sio kutumia vifo vya raia hivi tujiulize kwenye huo mgomo ni nani muathirika kama sio masikini na watu wa kipato cha chini kuna kiongozi yeyote anayeathirika hakuna, wanakuwa kama magaidi wanateka watu ili matakwa yao yakubaliwe zaidi ya hapo wanawauwa.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom