Maandamano makubwa ya Madaktari yaja (wiki ijayo)

Wagonjwa wanapelekwa india kwakuwa hospital hazina vifaa mfano Muhimbil hakuna Ct scan..rudishen lesen zao ili muone mbona mnazing'ang'ania si mtafute za kwenu sasa
Sio kila ugonjwa unaofanya watu waende India unahitaji CT Scan.
 
hofu ya u-ccm wako itakuua wewe, kenya, waliandamana, israel na portugal the same, sasa unashangaa madaktari kuandamana!! halafu unakurupuka kusema chadema, kwenye matangazo umesikia wameomba chama cha siasa yoyote?!au kwa kuwa wewe hupaswi kuwepo pale kwa sababu ya ruhusa ya bosi wenu aliyewatuma kuwahadaa wananchi?..gluteal thinking,..period.

Wewe mbona unalia lia sana humu JF serikali imeishasema hawana uwezo wa kuwalipa mshahara mmnaotaka kwa nini uanzishe mgogoro na muajiri wako wakati kaishasema hana uwezo huo, wewe si daktari unataka maslahi yako na mshahara mkubwa nenda wanapolipa vizuri TMJ, Aga Khan, Regency, Hindu, au Marekani achana serikali, siku Chadema wakichukuwa nchi mtalipwa milioni 10, kubali usikubali Chadema wamewaalibia mnaonekana wana siasa tu.

Usijifananishe na Kenya au Israel hao wanajitambuwa nyie wenyewe sio wamoja kila daktari anaangalia maslahi yake.
 
Sio uamuzi sahihi kufukuza madaktari,,tatizo hatuna vingozi makiin,,,kwani Ndo tatizo limekwisha?????

Wagonjwa waataumia sana Kwa mtindo huu,mi nawashauri madaktari waachieni hospital yao watbu wenyewe mi serikali hii inanikra sana
 
hakika madaktari wanajitahidi kutokubaliana na oppression ya watawala wetu......

All is needed ni sapoti ya wananchi kwa ujumla wake lakini pia panahitajika muungano wa kada zingine katika. I think

we need all to be strong katika kuwaambia watwala wetu kwmaba mambo haya hayafai

haiwezekani serikali wakati ikijuua kwa uhakika kwamba watanzania wana upungufu mkubwa wa human resource kwa kada za afya (madaktari, manesi.....) at the same time inafutia madaktari registration. Huku ni kutatua tatizo kwa kutengeneza another tatizo, this translates into serious crisis

me hate this 4 sure
 
Upepo huo ushapita tengenezeni mwingine wa manesi,Jk mpaka November 2015.Kilichowaponza ma dr ni kusaidiwa kufikiri na wale walotumia Elimu ya Certificate kupata Phd!
 
Sasa naona professional imewekwa pembeni na sasa....

maneno mengi toa SOLN, Watafanyaje kama serikali pia inakiuka taratibu kila wakati, from no where unafuta lesen ya dr 319 pasipo kufuata hatua stahiki . BINAFSI NAUNGA MKONO HADI PALE SERIKALI ITAKAPOONYESHA NIA YA DHATI KUSHUGHURIKIA MADAI YAO
 
Hawaogopi mabomu ya machozi na maji ya kuwasha? kama hawaogopi bai tunawatakia kila kila la kheri.
 
hakika madaktari wanajitahidi kutokubaliana na oppression ya watawala wetu......

All is needed ni sapoti ya wananchi kwa ujumla wake lakini pia panahitajika muungano wa kada zingine katika. I think

we need all to be strong katika kuwaambia watwala wetu kwmaba mambo haya hayafai

haiwezekani serikali wakati ikijuua kwa uhakika kwamba watanzania wana upungufu mkubwa wa human resource kwa kada za afya (madaktari, manesi.....) at the same time inafutia madaktari registration. Huku ni kutatua tatizo kwa kutengeneza another tatizo, this translates into serious crisis

me hate this 4 sure

Suala ni kuzuia magonjwa, sio kutibu tuuu. Mnataka daktari kila kijiji, nani kasema watanzania wote wagonjwa? Hili suala ni la mkakati. Nchi za wenzetu, jiji lenye wakazi milioni sita, hospitali ni moja, na wanaona wagonjwa wasiozidi 200 kwa mwezi. Unahitaji madaktari wangapi hapa? Tunainvest kusiko!!
 
Mara ngapi? wasitese wananchi, wao kwa wao wameshindwa kuungana, Hizi habari za madaktari zinatupotezea muda uku JF
 
Wewe mbona unalia lia sana humu JF serikali imeishasema hawana uwezo wa kuwalipa mshahara mmnaotaka kwa nini uanzishe mgogoro na muajiri wako wakati kaishasema hana uwezo huo, wewe si daktari unataka maslahi yako na mshahara mkubwa nenda wanapolipa vizuri TMJ, Aga Khan, Regency, Hindu, au Marekani achana serikali, siku Chadema wakichukuwa nchi mtalipwa milioni 10, kubali usikubali Chadema wamewaalibia mnaonekana wana siasa tu.

Usijifananishe na Kenya au Israel hao wanajitambuwa nyie wenyewe sio wamoja kila daktari anaangalia maslahi yake.

Sijui ni kwanini unalazimisha kuwa CHADEMA kinahusika wakati viongozi wameshakataa kuhusika.
 
....Tatu wamesema madaktari bingwa wameanza kuacha kazi na wengine wanahangaika kutafuta kazi nje ya nchi.

Source:CHANEL TEN

Si JK alishawashauri mtafute muajiri atakayewalipa vizuri? Sasa maandamano ya nini tena!
 
WTF! ..... bora kutoa hizo billions kwa dr from Iran kuliko hawa dr uchwala wa Tz, wanaotoa dawa za maumivu tu kwa kila ugonjwa. TUMEWACHOKA fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!![/QUOTE ....

Taratibu mkuu kama huna hoja si uendelee tu kucheza bao na akili mgando wenzio kuliko kuanika utupu wako hapa. Kama serikali haleti dawa zinazohusika ulitaka wakuandikie dawa gani? N kama hauna complain ya pain sidhani kama utapewa pain killer. mwisho sema nimewachoka sio tume.
 
Hawa vijana sasa wanazidi kutapatapa. Serikali haiwezi kuruhusu hayo maandamano
 
Sijui ni kwanini unalazimisha kuwa CHADEMA kinahusika wakati viongozi wameshakataa kuhusika.

Chadema kukanusha si ndio jadi yenu? Pamoja na umma kushuhuia uzinifu wa Dr. Slaa bado mnakusha kwa mantiki hiyo hakuna jipya.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mara ngapi? wasitese wananchi, wao kwa wao wameshindwa kuungana, Hizi habari za madaktari zinatupotezea muda uku JF

Nakubaliana na hoja yako kimsingi kabisa!Ubabe huu wa serikali dhidi yao ni kwa sababu wameshindwa kuwa wamoja mwanzo mpaka mwisho!Kama wangekuwa wamoja nadhani serikali ingeufyata tu,lakini imewagawa makundi na inawaendesha inavyotaka!hizi ni mbinu zinazotumika hata vitani lakini mara nyingi zilikuwa zikitumiwa na mkoloni na jina lake mtindo huu uliopata umaarufu uliitwa ''DIVIDE AND RULE''! Mwalimu Nyerere aliushinda kwa kuja na kauli mbiu ya umoja ni NGUVU!Kuliko kuendelea kuhangaika hapa Jamvini ni bora Madaktari wakaonyesha kuwa ni wamoja hapo hata wananchi watawaunga mkono!lakini kwa utenganifu huu hakuna kitakachofanikiwa!
 
Sasa naona madaktari akili zimeanza kuwarudia, kwa sababu hiki ndio kitu kilitakiwa kufanyika muda mrefu sana. Nilishangaa kusikia madaktari wamekataa kuongea na wizara ya afya eti kwa kuwa wanadhani wizara "haiko serious".

Naunga mkono maandamano na kwenda kuishinikiza wizara kuwarudisha interns kazini. Intern kuadhibiwa kwa mgomo ambao ni wa madaktari wote si sahihi hata kidogo. Zifanyike jitihada zote za kuwrudisha interns kwenye program zao na jitihada hizo zinapaswa kufanyika mapema. Asiyetaka kupractice afanye hivyo by choice na siyo kwa kunyimwa leseni.

lakini, najiuliza, hivi hawa viongozi wa madaktari wanapoongea na media huwa hawapati ushauri kwanza? Huyu kiongozi ananukuliwa hivi "Daktari mmoja hadi anafikia hatua hii anatumia zaidi ya Sh30 milioni kwa ajili ya kupata elimu, je, ni shilingi ngapi kwa madaktari zaidi ya 380? Haya ni mabilioni ya fedha za walipa kodi ambayo Serikali inapoteza kwa kuwafukuza madaktari,". Hapa anatoa ujumbe kuwa madaktari wanasomeshwa kwa pesa za walipa kodi. Anajaribu kutumia siasa ili awavutie wananchi kuwa anajali matumizi mazuri ya pesa zao za kodi. Lakini anasahau kuwa wananchi wengi ambao hawaungi mkono madaktari wanaegemea hapohapo kuwa madaktari wanalazimika kuwatibu kwa sababu wamesomeshwa kwa pesa za wananchi. Kwa lugha nyingine anakili kuwa kugoma kuwatibia wananchi ni kugoma kulipa fadhila.
Hawa inabidi wajifunze jinsi ya kutoa matamko ili wawe consistent.

Pia nimefurashishwa na pale Katibu wa MAT aliposema "maandamano hayo yatafuata taratibu zote za kisheria, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa polisi saa 48 kabla ya kuandamana na madaktari wote watavaa makoti meupe na wasio madaktari watatakiwa kuwa na vitambaa vyeupe". Hii inadhihirisha kuwa kiongozi huyu anatambua kuwa wasomi hawapaswi kufanya mambo kichekibobu. Wasomi wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na jamii na katibu huyu amedhihirisha hilo.
 
Back
Top Bottom