Maandamano makubwa Songea!

Wakuu hii kitu ni ya kweli nimeongea na rafiki yangu amenihakikishia na amesema chanzo ni imani za kishirikina kwa kuwa watu wakishauawa wananyofolewa sehemu za siri na akasema mauaji yanafanyika hata mchana hivyo kwa sasa watu wanatembea zaidi ya moja. Kwa muda wote polisi hawajachukua hatua zozote kuzuia mauaji.
 
Hali sio nzuri manisapaa ya songea, Imani za kishirikina zimetawa mjini mzima songea, Tokea ijumaa mpaka ijumaa mpaka leo wamekufa watu wanne na kila mtu akiuliwa anachukuliwa sehemu za siri lakini jeshi linakanusha hizo habari. leo watu wameandamaana kwenye maandamano hayo mpaka sasa wamekufa watu wawili na maduka yote yamefunga.
 
Kutoka Blogu ya songea yetu moja ya marehemu ni huyu hapa na polisi wakiwa kazini



Marehemu



Mwandishi wa TBC akiwa anajihami na risasi za polisi

Hivi hawa polisi wako juu ya sheria hata wawapige risasi raia wasio na silaha? Kuwa polisi wa namna hii ni laana na aibu kwa taifa.
 
Taarifa zinazotolewa humu jamvini juu ya mauaji yanayo endelea huko songea si nzuri na haikubaliki hata kidogo.Nasema haikubaliki kwa sababu vyombo vya dola vimeamua kutumia nguvu kubwa kuliko matumizi ya busara katika kukabiliana na wananchi waliojawa na hasira kutokana na mauaji yanayoendelea katika maeneo mbalimbali mjini humo.NCHI HII haina budi kuombewa na kila raia ili kila idara iongozwe na busara kwanza vinginevyo ubabe utaigharimu hii nchi.HIVI JE HAKUNA ANAYE TAMANI AMANI YA ZAMBIA?POLISI SONGEA JIFUNZENI TARATIBU ZA KUTUNZA Amani ktk jamii mf.kujua dalili za tukio na kuwahi kulikabili nk.
 
Yaani hizo picha hapo juu zinasikitisha.


Makamanda wa Mwema wamejazana katika Gari kwa ajili ya kupambana na Waandamanaji. Lakini walipoambiwa kuwa Wananchi wanauawa kinyama, kama hawa Askari watiifu wa mwema wangelikwenda haraka kama leo. Ni matumaini yangu kuwa hao Wauaji lazima wangelikamatwa wote.

Yaani badala ya leo kushuhudia Raia wakifa basi tungepata taarifa ya kuuawa kwa majambazi Songea. Ingetia faraja sana na tungelisifia Jeshi letu la Polisi.

ACHENI NISEME....... HATA MKINI...... ACHENI NISEME. KUWA HILI JESHI LA POLISI TANZANIA INABIDI TUBADILISHE JINA NA LIITWE "JESHI LA MAJAMBAZI TANZANIA" (JMT) INGEPENDEZA ZAIDI. ACHENI NISEME............ INANIUMA SANA!!!!!!



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kwani songea mjini kuna mbunge,aende kusulushisha kama sugu alivyofanya mbeya hana jeuri hiyo,kwa sababu anajua alishinada uchaguzi kwa hila na wanamtamani kweli 2015 wamuone nchimbi.


Yaaaaniiii huyo mbunge akitia mguu ndo moto hautazimwa.... asitie sura yake .... sio Mbeya kule.
 
Taharuki iliyoko SONGEA ni kubwa sana. So far, zaidi ya watu watano washauawa na POLISI!!! Majeruhi ndio usiseme!!!
 
Kwa mliosikiliza radio na kuangalia ITV mmejulishwa kinachojiri songea asubuhi hii ni mapambano ya askari na raia

CHANZO CHA MAPAMBANO
Kuna raia wanauawa tangu juzi na matukio yanaripotiwa ila askari hawachukui hatua yeyote ile zaidi wanasema ushahidi hawajauona,usiku wa kuamkia leo limekua tukia la 5 raia kuuliwa na askari kama kawaida yao hawatoi ulinzi kwa raia wao.
Asubuhi raia(Watoto,vijana,wazee)wakaamua kuwatolea uvivu askari na kuandamana hadi kituo cha polisi kudai haki ya kulindwa na kuishi raia walikua wengi kuliko uwezo wa askari wa kile kituo hivyo waliona hapa wakiwa wakali kituo kitachomwa moto maaana walikuja na jazba raia wakawaambia taarifa ziko kwa mkuu wa wilaya raia bila simile wakaanza maandamano hadi kwa mkuu wa wilaya kufika huko naye akanawa mikono kama pilato akasema mkuu wa mkoa ndo liko mikononi mwake,raia hawakuishia hapo wakalianzisha hadi kwa mkuu wa mkoa huku wakiimba "TUMECHOKA KUUWAWA" hadi kwa mkuu wa mkoa,hapo ndo movie ilpoanzia kumbe raia wakati wanaenda kwa mkuu wa mkoa inaaminika simu zilipigwa kwa mkuu wa mkoa na askari wanaolinda(FFU) wakafunga geti hapo ndo ikawa vuta nikuvute raia wakaweka kambi nje huku wanaimba nyimbo "MKUU WA MKOA UNAWAOGOPA RAIA WAKO JIUZURU",muda si mrefu gari ya FFU likawasiri likiwa na askari wa kutosha kwa vile raia hawakua na silaha wala ugomvi wakaamua kubaki huku wanaimba askari kama kawaida yao wakawa wanazidi kusogelea huku wakitoa ishara wananchi watawanyike huku wananchi wakigoma hawatoki hadi mkuu wa mkoa naye atoke nje hapo ndo askari wakaanza kufyatua risasi za moto na raia wawili wakafa.habari zikafika mjini raia wameuliwa na askari hapo ndo mji ukazizima raia wakaingia mitaani askari waliokua mitaani walianza kupata upinzani mkali hd askari wawili wamekufa hadi hivi ss,imebidi jeshi liingilie kati na mji wote kufungwa hivi ss mjini ni makundi ya wanajeshi na askari ndo yametawala hakuna maduka wala mabenki yanayofanya kazi

VIFO
Nimeshuhudia raia wawili na askari mmoja tu kwa macho yangu kwa sehem niliyokuwepo,kiujumla inasadikiwa raia zaidi ya wa4 na askari 2 ndo wamekufa,mji umepoa kabisa na mm ndo niko nyumbani ila ntarudi later mjini kuchukua news zaidi ili niwajulishe
Nawakilisha

Ahsante kwa taarifa, kwakweli ni masikitiko makubwa kwa wananchi pamoja na hao askari waliopoteza maisha yao.

Hili suala la polisi kutumia mabavu kila mara kwa raia wasiokuwa hata na jiwe ni upumbavu mkubwa sana, na sijui kama haya ndiyo mafundisho wanayokwenda kupata chuoni CCP kwa muda wote wa mwaka mmoja.

Kama wananchi wameandamana hadi kwa mkuu wa mkoa na wanachotaka ni mkuu wa mkoa atoke kuwasikiliza, tatizo lilikuwa wapi hadi FFU wanaamua kupiga risasi za moto hadi kuua raia? kama wameshindwa kuwalinda raia hadi wanauawa kila siku bila msaada wao, huo ubabe wa kuwaua raia wema unatoka wapi? mbona wameshindwa kupambana na hao wauaji?

Kumbe Dr. Mwakyembe hakukosea kwamba jeshi la polisi la Tanzania, ndilo jeshi la polisi pekee duniani linalosubiri kuletewa ushahidi mezani kama vile mahakama zinavyosubiri kuletewa ushahidi ili zifanye kazi. Na hii tabia ya polisi kuwaonea wananchi ipo siku watachoka na wataamua kukabiliana nao bila kujali risasi za moto ama mabomu, ikizuka majimaji ya pili huko wasije kuwalaumu wananchi.
 
Ndugu yangu Temilugoda, sikio la kufa halisikii dawa ndio tunavyoweza kusema juu ya nchi hii na serikali bila kusahau idara zake.
 
Hata wapo radio dsm wameripoti muda uhu saa sita steven agustino.amesema miili mitatu imeonekana ikiwa imelala barabarani wawil wamepgwa risasi kichwani na mmoja kifuani.tanzania nakupenda sana
 
Hali ni tete kuna hiace katika harakati za kukimbia imetumbukia kwenye korongo na abiria ila hakuna aliefariki ni majeruhi tu.
Balaah na RPC anazidi kutema pumba ati hao wanaouana ni watu na wapenzi wao.
 
Back
Top Bottom