Maandamano makubwa Songea!

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma (Kamuhanda) analalamikiwa kwa kulea majambazi ambao wanaua Raia kila kukicha na kuwaibia,wanachi wakienda kumlalamikia anawambia hakuna kitu kama hicho sasa wanasongea wanasema liwalo na liwe hadi kieleweke.
 
Jamani nimepata habari kuwa songea hali sio nzuri, kuna vita kubwa katika ya FFU na Bodaboda chanjo kuuwawa kwa dereva mmoja wa bodaboda. Aliekaribu atujuze jaman.

Nawakilisha.

Nimepata hiyo kupitia TBC1 kwenye taarifa ya habari kwa ufupi saa nne.Inaonekana hali si nzuri maana wanadai vurugu ni kubwa na wananchi wanasema mpaka polisi wachukue hatua ya kuzuia mauuaji yanayofanywa na majambazi kwa takribani wiki moja.
 
watu wawili wameua na wengi kujeruhiwa asubuhi hii songea. raia hao walikuwa wakiandamana kushinikiza jeshan la polisi lichuke hatua kwa mauaji yanaendelea kila siku mijini hapa. taarifa zaidi na picha za matukio tembelea songeayetu.blogspot.com
 
mpaka sasa raia 6 wameuawa na polisi ktk maandamano ya amani kupinga mauaji
 
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma (Kamuhanda) analalamikiwa kwa kulea majambazi ambao wanaua Raia kila kukicha na kuwaibia,wanachi wakienda kumlalamikia anawambia hakuna kitu kama hicho sasa wanasongea wanasema liwalo na liwe hadi kieleweke.

Hapo songea wangempata afande Zelota steven!
Dodoma pale wamesahau kila kitu.
 
kumekuwa na vita kubwa ya polisi na askari katika mji wa songea baada ya wananchi kupamba moto na kushindwa kuzuia hisia zao kwa kile wanachokisema polisi hawatoi ushirikiano kwa mauaji yanayoendelea katika manicipal ya songea. taarifa ambazo ninazo wananchi wawili wamepigwa risasi na polisi na wananchi wamempiga mawe polisi ambayo yupo katika hali mbaya.

wapi tunakwenda?
 
Redio one Breaking news inasema hadi sasa raia wema wawili tayari washa pigwa risasi,hali inazidi kuwa tete.
 
Hali ni tete, maduka, benki na biashara zote zimefungwa. Polisi wametanda mji mzima. Breaking news Star TV

My Take.
Jmaaa wa Songea wameshindwa kuadapt strategies za Wanambeya
 
Wanafunzi wanashindwa kusoma kutokana na hawa jamaa(ffu) wanavyo furumusha mabomu ya machozi.walimu na nao wametoka nje kila mmoja na njia yake.
 
Kweli hiiiiiiiiii ni hali zaidi,nguvu zaidi,na kasi mpya ya wanaccm kwa kuua raia wasio kuwa na hatia.
 
Hali inadhidi kuwa tete,wanafunzi wanalia,wengine wanakimbia,wametoka madarasani,mji mzima umejaa polisi,hali ni mbaya sana sana,hakuna maelewano kwa sasa,kijana alipigwa risasi kwa sasa amekimbizwa hospitali ya mkoa anatokea sehemu moja naitwa matarawe.
Jamani jamani jamani!
 
Nimuda sasa muafaka kwa wanasongea kuachana na hawa wanyang'anyi wa haki za binadamu,wanao waua raia wao kwa kuwapiga risasi.
 
Back
Top Bottom