Maandamano makubwa kumpongeza Jakaya Kikwete!

Kweli Watanzania tumefika pabaya kama tunafikiri rais kufukuza na kuwawajibisha wazembe na wezi wa mali ya umma sio wajibu wake ni uamuzi mgumu basi tena! Watakaoandaa na kushiriki maandamano haya ni lazima wana matatizo ya kichwa hawapo kawaida kwenye jamii!!
 
Maandamano makubwa yanatarajiwa kufanyika nchi nzima kumpongeza rais kikwete na kamati kuu ya ccm kiujumla kwa kufanya kuchukua maamuzi magumu ya kulifanyia mabadiliko makubwa baraza la mawaziri.

Rais kikwete ameamua kufanya maamuzi magumu hayo licha ya kwamba kuna jukumu zito la maandalizi ya bajeti za wizara na kwa hiyo ni changamoto kubwa kuingiza watu wapya kwa maana ya nafasi za mawaziri, lakini hata hivyo, hao wapya itabidi wategemee zaidi mihtasari ya watendaji watakaokuwapo katika kila wizara husika itakayoguswa na mabadiliko.

Wananchi mbalimbali nchini wamepongeza hatua hiyo ibnayotarajiwa kuchuliwa na rais kikwete huku wakisema kwamba hatua hiyo itaifanya ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iwe na nguvu kubwa ya kuisaidia serikali kupambana na ubadhirifu unaofanywa na mawaziri kwa kushirikiana na watendaji wa serikali wasio waaminifu.

Naye mbunge zitto kabwe ambae alishikia bango hoja ya kutaka bunge lipige kura ya kutokua na imani na waziri mkuu,akizungumza bungeni wiki juzi aliwapasha mawaziri kwa kuwaambia ''Mawaziri msimsingizie Raisi na kumchafua kwa uzembe wenu na ubaridhifu wenu wa kushindwa kusimamia mali na pesa za walipa kodi kwa manufaa yenu binafsi i lazima muwajibike na mchukuliwe hatua stahiki''
Kwani Mawaziri ndo wanaoandaa budget?????????????????????
 
Turudi kwenye mada. Mtoa taarifa una uhakika na maandamano kuwa yatafanyika, au unapendekeza maandamano yafanyike? Kama yatafanyika, tueleze ni nani wanaoandamana, hata kama ni ya nchi nzima lakini yanaanzia wapi? Tujuze habari kamili, acha jazba.
 
Maandamano makubwa yanatarajiwa kufanyika nchi nzima kumpongeza Rais kikwete na kamati kuu ya CCM kiujumla kwa kufanya kuchukua maamuzi magumu ya kulifanyia mabadiliko makubwa baraza la mawaziri.

Rais kikwete ameamua kufanya maamuzi magumu hayo licha ya kwamba kuna jukumu zito la maandalizi ya bajeti za wizara na kwa hiyo ni changamoto kubwa kuingiza watu wapya kwa maana ya nafasi za mawaziri, lakini hata hivyo, hao wapya itabidi wategemee zaidi mihtasari ya watendaji watakaokuwapo katika kila wizara husika itakayoguswa na mabadiliko.

Wananchi mbalimbali nchini wamepongeza hatua hiyo ibnayotarajiwa kuchuliwa na rais kikwete huku wakisema kwamba hatua hiyo itaifanya ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iwe na nguvu kubwa ya kuisaidia serikali kupambana na ubadhirifu unaofanywa na mawaziri kwa kushirikiana na watendaji wa serikali wasio waaminifu.

Naye mbunge zitto kabwe ambae alishikia bango hoja ya kutaka bunge lipige kura ya kutokua na imani na waziri mkuu,akizungumza bungeni wiki juzi aliwapasha mawaziri kwa kuwaambia ''Mawaziri msimsingizie Raisi na kumchafua kwa uzembe wenu na ubaridhifu wenu wa kushindwa kusimamia mali na pesa za walipa kodi kwa manufaa yenu binafsi i lazima muwajibike na mchukuliwe hatua stahiki''

Inanishangaza sana, maandamano? maandamano ya kumpongeza kwa lipi la maana alilofanya?? au kwa lipi la maana aliloshinikizwa kuamua kufanya?? kidogo ungesema kuipongeza CC lakini kumbuka JK alishasema urais wake hauna ubia na mtu, baadaye akapuuza taarifa za CAG kwa kuwatia viburi mawaziri wezi kwa kusema msijiuzuru acheni ni upepo utapita, sasa leo tunakuja kumpongeza kwa lipi??? kwa kushauriwa na CC?? kwa kujipendekeza kwa rais??

Ok andamaneni kwangu itakuwa fursa ya kuangalia idadi ya wajinga Tanzania, wale wanaopelekwa pelekwa kama bendera

Nitampongeza Rais kama atawachukulia hatua za kinidhamu sawa sawa na alivyochukuliwa Liyumba, hatua zichukuliwe kabla ya kuteua Baraza jipya vinginevyo sina Imani na hilo baraza, sina imani na rais, sina imani na serikali nzima itakuwa imejaa wezi na matarajio yangu ni kushuhudia wizi mwingine mkubwa kuliko hizo Trillion 11 zilizofananishwa na Upepo.
 
Naweza kuunga mkono maandamano kwa ujasiri wa JK kukubali kuukata mkono wake mwenyewe kwa kuwa anaona unamfanya atende dhambi, ni hilo tu. Nasema kwa sababu mkono hauwezi kukwapua bila dhamira kutoka moyoni. NI SAWA NA ALIYEKATA NYETI ZAKE KWA SABABU ZILIMPELEKEA KUPATA UKIMWI. Kama akiri itatumika sawa sawa nadhani ni bora kufanya maandamano ya kumpongeza CAG kwa kuwa jasiri kufichua uovu na pia kuipongeza CDM kwa shinikizo lake lililozaa matunda. Nadahani CAG atakubaliana na mimi kuwa CHADEMA imemfanya afurahie kazi yake.

Watanzania msije mkadanganyika kwa lolote kila wizi uliofanywa na waziri yeyote JK yuko nyuma yake. Ndugu zangu Ikulu inamacho kuliko unavyodhani wewe, huwezi kuvusha hata sisimizi Ikulu isikuone. Ni vibali vya Ikulu vinavyovusha madini, ni vibali vya ikulu vinavyouza maeneo nyeti, ni vibali vya Ikulu vinavyo uza vitalu, ni vibali vya Ikulu vinavyohalalisha ufisadi wa aina zote. Kama utaamua kukataa kataa lakini ukweli huo nimekupa. Kama huamini muulize EL kwa matatizo yaliyompata, JK alichangia 60% EL 25% Lost hamu 15%. Ujasiri alionao ni wakuwaruka wenzie na kuwaacha kwenye mataa. Hebu jiulize huyo mtoto wake Riziwani mtaji wa malori lukuki na vituo vya mafuta kaupata wapi? Watu tunaona bwana. JK ndiye kichwa cha maneno yote.

Mwizi hawezi kuibia nyumba kabla ya kumteka mwenye nyumba bwana. :nono::nono:
 
Mmmh mpaka mtishiwe na Mh. Zitto na CDM ndo mchukue maaamuzi magumu, labda yawe maandamano ya kuwapongeza kwa kuwa wasikivu kwa CDM ambao ndo walioanzisha mada na kupiga sana kelele bungeni. Katika maandamano hayo msisahau kuwapongeza pia Zitto, Tundu Lissu, Filikunjombe, Lugola na CAG kwa mchango wao mkubwa katika hilo. ingawa kwa mtazamo wangu, JK hastahili pongezi na sifa hizo
 
kuna vitu vingine ukivisoma unaweza kutapika...huku ndiko watu wanakokuita kuhesabu vifaranga vya kuku wakati bado havijatotolewa...wameshaliona hilo baraza jipya la mawaziri na makatibu wake?uadilifu na utendaji wao ukoje? mawaziri, makatibu wa wizara,wakurugenzi wa halmashauri na watendaji wote wa serikali waliohusika na ubadhirifu huu wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua? haya maandamano ni sawasawa na mtu anayepaka poda kuficha jipu kubwa kwenye paji la uso...!
 
mnachekesha sana yhamna kazio za kufanya? Simwokote makopo muuze? Eti maandamano ya kumpongeza nani? Kwanini? Kwa lipi? Acheni siasa ebu fanyeni kazi jengeni uchumi kama ni kulaani wezi na kuwafikisha mahakamnaii siku wanapanda karandinga tutaandamana kama idadi yao wote watapelekwa kisutu mahakamani

Read between the lines mkuu utaelewa nimechomaanisha.
 
Mkuu, kwa kuwa maneno ya Mh.Zitto umeyapa umuhimu napendekeza maandamano hayo yalenge kumpongeza Mh.Zitto na bunge ambalo limesababisha jambo hili lifanyike.Lakini nashauri hao wakereketwa wa maandamano ya kupongeza wasichokijua mwanzo wake, wasubiri baraza jipya la mawaziri litangazwe zijekuwa sarakasi za sakata la jairo.
 
sioni cha kumpongeza huyu raisi kwani kuwasambaratisha na kuwawajibisha wasiotekleza majukumu yao ni wajibu wake mtu hapongezwi kwa wajibu wake. haswa anayefanya majukumu hayo akiyafanya kwa kulazimishwa.
 
Wewe kim kadashian na hao watakaoshiriki ayo maandamano lazima mtakuwa wendawazimu, yani kuchukua hatua dhidi ya wezi /mafisadi ambao mwenyewe jk aliwaapisha kwa mbwembwe na kuwasifia kuwa wachapa kazi ni ujasiri??
Hapa ujue anasafisha uozo alou create yeye mwenyewe, hana maamuzi yoyote bali kaogopa nguvu ya umma, apa chadema kapata credit nyingi na za kutosha, mbona jk alidai huo ni upepo na utapita, hii ni si maamuzi yake bali ni shinikizo la chadema ndugu kama haujui, credit zote to chadema
mbona tukiichukua nchi ata jk tutampeleka mahakamani kwa kuchangia upotevu wa mali ya umma, kim you might be crazy, ondoa mada zako maji taka apa
 
Back
Top Bottom