Maandamano Kumpinga Kikwete

Just for curiosity,... Mtoto akichukia au kama anadai kitu analia. Watazania kwa ujumla wao wanachukua hatua gani kama hawaridhiki na watawala wao??

Kuwaondoa madarakani. Watawala siyo kama wazazi, kelele zetu kwao haziwa sumbua as long as wanaendelea kuwa madarakani. Dawa ya cancer ni kuing'oa kabisa ndiyo uanze tiba ya kuiponya. Vidonda walivyo tuwekea haviwezi kupona mpaka waondoke wanaozidi kuzi tonesha kila kukicha.
 
Mmmh!! Asante mjomba tumekusikia.....Lakini mjomba kubeba gunia la misumari wakati una upara huo ni ujinga mjomba, sawa na nazi kuvunja jiwe...
 
Wakuu,

Mkishaandamana musisahau kutuwekea picha na yaliyojiri hapa hapa JF.
 
Lini wana JF tusioridhishwa na utawala wa JK tutashika mabango na kuandamana kuupinga utawala huu ulioshindwa kufanya kazi tukimtaka aondoke pale magogoni? Aachie ngazi.

Mbona maandamano yamepangwa 2010?! Kura yako na za wale utakaowaelimisha ndiyo maandamano yenyewe. unataka maandamano ya kutembea kwa miguu hadi jangwani? yatasaidia nini? Tunataka maandamano yenye tija bwana.
 
Lini wana JF tusioridhishwa na utawala wa JK tutashika mabango na kuandamana kuupinga utawala huu ulioshindwa kufanya kazi tukimtaka aondoke pale magogoni? Aachie ngazi.
Unapokwenda kulewa kumbuka kuacha pesa ya supu asubuhi...otherwise unaamka na mawazo ya kilevi namna hiyo.!
 
Mkuu Kaniki,
JK na serikali yake ni binadamu, hata tukisema hawezi! bado hatuwezi kupata malaika waje washike madaraka. bado tutahitaji watu kati yetu letsay Mengi, au Slaa au Zitto nk ambao nao ni binadamu (wanamapungufu). hivi Mengi akiwa Raisi si atahitaji mawaziri, makatibu wakuu wakuu wa mikoa na wilaya unategemea atapata wote wazuri? si rahisi kutakuwepo wengine wabovu.
nafikiri ni vizuri tu narrow down hizi issue, tutafute penye tatizo na kucheza napo instead ya kufikiria utawala mzima kwani is a huge thing.
halafu hivi mfano kama ungenufaika na utawala huu wa JK ungekuwa bado na hiyo position uliyonayo say umepewa u Director general au cheo kingine tu.
Samahani mie sipingi najaribu kufikiria tu kama walio jirani na keki ya taifa wanamawazo gani isije kuwa tunalalamika tu sie tulio nje
 
Ng'azagala;458104 ;;;;;;;;;;;;;;; mie sipingi najaribu kufikiria tu kama walio jirani na keki ya taifa wanamawazo gani isije kuwa tunalalamika tu sie tulio nje[/QUOTE said:
NG'AZA,
Umetoa changamoto nzuri.
Yawezekana mawazo ya watu ni kulingana na uhusiano walionao na hiyo serikali.
Hao wala KEKI, wanaweza kuwa hawaoni kama baadhi yetu tunavyoona.
 
Tuhamasishe upatikanaji wa viongozi bora kwa njia ya kura 2010,maandamano yatatugharimu kwani yatawapa mafisadi visingizio kuwa ni vurugu,tusubiri tuu ili tufanye kweli 2010.
 
Naona tunapiga mayowe tu hapa.
Je kuna maandalizi gani kuelekea 2010? je tutarudia makosa ya kupiga kura huku tumefunga macho tangu 1995 hadi sasa?

Nadhani ni budi kuwakomboa kifikra wengi zaidi kisha maandamano yatakuja yenyewe bila shaka
 
Unaweza vipi kusema Kikwete ameshindwa kazi? Nimeona katika gazeti,jana au juzi kwamba inflation imepungua[a fraction of a percent] mwezi huu. Huko ndiko kushindwa kazi?
 
Unaweza vipi kusema Kikwete ameshindwa kazi? Nimeona katika gazeti,jana au juzi kwamba inflation imepungua[a fraction of a percent] mwezi huu. Huko ndiko kushindwa kazi?
kima cha chini na bei ya kilo ya unga kuna uwiano??
lete vigezo shekhe na si kupiga porojo. naamini walio wengi humu si kwamba wanapinga kwa hoja binafsi au chuki au wivu bali kwa uhalisia wa maisha ya leo.
Unaposema inflation imepungua halafu bado sukari kilo ni shs 1,300/- then mshahara ni ule ule alfu 83 sijui. ni kejeli ndugu.

Umeme wanapandisha bei kinyemela, maji ndo usiseme wanakutumia bill ilhali wanajua haauna huduma hiyo miaka kadhaa.

njoo na data tutakuelewa shekhe
 
Kwakweli yakiitishwa mimi nitakuwa mstari wa Mbele, maana nchi inakwisha kabisa! Sifa zake utasikia amekuwa Rais wa kwanza mwafrika kukutana na Obama!!! So what?
 
Naona tunapiga mayowe tu hapa.
Je kuna maandalizi gani kuelekea 2010? je tutarudia makosa ya kupiga kura huku tumefunga macho tangu 1995 hadi sasa?

Nadhani ni budi kuwakomboa kifikra wengi zaidi kisha maandamano yatakuja yenyewe bila shaka

Mkuu,
Hujachelewa kujipanga lakini unatakiwa uwe umeshafanya maamuzi hadi kufikia sasa.
Mimi nimeshakata shauri kura yangu ninampatia JK kwa mara nyingine tena.
 
Sio rahisi kumpinga Kikwete kwa vile wengi tumefunikwa na blanketi zito la CCM. Hivyo, woga umetutawala.
__________________________________________________________
Do not conform any longer to the pattern of this world, but be transformed by the renewing of your mind. Then you will be able to test and approve what God’s will is—his good, pleasing and perfect will. Rom 12:2:
 
Usidhani wote ni wenzio hapa, hebu sema Malecela au Mengi ni fisadi uone moto utakavyowaka. Nani kasema nini ndio mtindo wa kisasa, watu bendera fuata upepo. Waoga kusimamia facts, wanasimamia maneno ya kusikia na uzoefu. Sio sheria na kanuni.

Jaribu kuitisha maandamano 'ya kumpinga Kikwete'.

Umekwishasema. Tunaungojea moto.
 
mambo ya maandamano wanayajua sana waislamu......hebu tuwaombe inaweza kuwaje hii..
 
Lini wana JF tusioridhishwa na utawala wa JK tutashika mabango na kuandamana kuupinga utawala huu ulioshindwa kufanya kazi tukimtaka aondoke pale magogoni? Aachie ngazi.

JF ikianzisha chama na kukiita JF party hapo tunaweza kufika magogoni kumpinga kabla ya kutoka moja kwa moja 1/11/2010
 
Back
Top Bottom